Mtoto Bwaga Abdallah akipokea mfuko wa sukari kutoka kwa Maafisa wa Vodacom Foundation Grace Lyon kulia na Mwamvua Mlangwa wa pili kutoka kulia huku akisaidiwa na Sheikh Mohamed Khalili kushoto kutoka Tanga mjini na Sheikh Khamis Rashid Mwakilishi wa Sheikh wa Pangani wa pili kutoka kushoto, katika msaada huo pia Vodacom Foundation iligawa Mchele, Maharage, mafuta ya kula pamoja na vifaa vya shule.
Mwamvua Mlangwa Mratibu wa Uhusiano Vodacom Foundation akimkabidhi madaftari mtoto Mohamed Mtoo Ally wa Madrasat Tarba Mwera Pangani mara baada ya futari iliyoandaliwa na Vodacom Foundation mwishoni mwa wiki mjini Pangani na kufuturisha wakazi wa mji huo na kugawa misaada ya vyakula na vifaa vya shule kwa watoto wa vituo vya watoto yatima na Madrasa, wanaoshuhudia tukio hilo ni Sheikh Mohamed Khalili Mwakilishi kutoka Tanga Mjini na kushoto na Sheikh Khamis Rashid mwakilishi wa Sheikh wa Pangani.
Wakazi wa mji wa Pangani wakipata futari mwishoni wa wiki ambapo Vodacom Foundation iliwafuturisha na kugawa vyakula na vifaa vya shuleni wa watoto yatima na madrasa mbalimbali mjini humo ambavyo ni Mchele, maharage, mafuta ya kula, sukari na vifaa vya shuleni kwa ajili ya wanafunzi.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 6 mpaka sasa

  1. asalaamu alaykum bro misupu,

    Unajua lugha huwa shida pale ambapo baadhi ya maneno huleta maana nyingine pale yanapotamkwa visivyo. Mara nyingi hususan mwezi huu wa ramadhani utasikia fulani au taasisi fulani inafuturisha pahala fulani. Tendo la kuwaalika watu wakala futari kwako huitwa "kufutarisha" siyo vinginevyo. Hilo neno lililozoeleka lina maana tofauti kabisa na tendo lenyewe.

    ReplyDelete
  2. mungu awazidishie kheri kwa kufuturisha wasiojiweza,hivi ndivyo ilivyoamrishwa ktk uislamu,sio wafanyavyo viongozi wa serikali kufturisha viongozi wenzao wasio na shida yoyote,ufisadi du hata ktk msaada.haifaiiii

    ReplyDelete
  3. Shukrani Ankal Michuzi kwa habari za nyumbani. Picha ya sheikh wetu wa Tanga imenikumbusha mbali sana. Nadhani ni sheikh Mohamed Hariri wa pale Ma-awal Islam-Ngamiani- Tanga na si Mohamed Khalili.
    Mdau wa Konya-Uturuki.

    ReplyDelete
  4. father BenedictusAugust 31, 2010

    hii vodacom wenzao wamekazana na kujenga mabweni na majengo ya maabara za shule wao kila siku na vilemba nakufuturisha..lol..

    ReplyDelete
  5. Grace unapendeza na hiyo hijabu. Mashallah utadhani hajati au ustadhati au shekhati fulani. Kwa kweli imekukaa.

    ReplyDelete
  6. @mdau wa konya-uturuki.
    sawa kabisa ni sheikh mohamed hariri mohamed wa ma awal islam Tanga, na si mohamed khalili kama alivyoandika kaka michuzi.
    mdau wa Poland.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...