Katika Kijiji cha Halukumbi Tarafa ya Katunguru kata Chifunfu wilayani Sengerema wanafunzi 18 kati ya 37 waliokuwa wakisafiri ziwani Victoria kwa Mtumbwi kwenda shule leo asubuhi majira ya saa 1:45 walizama na kufa maji. Mpaka sasa miili 12 ya watoto hao waliokufa imekwsiha patikana huku mingine 6 ikiendelea kutafutwa ndani ya ziwa Victoria.
Home
Unlabelled
wanafunzi 18 wafa maji ziwa victoria leo
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
jamani,jamani nyie viongozi wa tanzania mnaokula mapesa wenzenu waliotoa kodi wanakufa kesho kwa Muumba mtasema nini,mpaka leo nchi ina uhuru miaka zaidi ya 40 katika karne ya 21 ya sayansi na teknologia na ari mpya kasi mpya bado matumia mitumbwi kama usafiri wa kud=safirishia watu...tukisema mnasema watu wa nje wanalonga sana ila kama hali ni hii wacha niendelee kupiga box tu...Mungu awalaze marehemu mahali pema peponi...na nyinyi viongozi siku yenu inakuja hamuwezi kuendelea hivi milele,remember you can fool some people for some time but you can't fool all people all the times...na wewe michuzi ibanie hii kwa kuwa umezoea kubana wakati tunakosoa wapumbavu fulani fulani.
ReplyDeleteWapumzike kwa amani...Inasikitisha...Huku viongozi wana mwaga pesa kugombea watoto wanakosa hata maboya ya kusafiria ziwani...
ReplyDeleteserikali haiwezi kukwepa lawama hii ni nini kinafanyika wakati ni wiki chache tu zimepita toka watu 9 wafe kule rufiji ktk tukio km hilo??? hii haiwezekani sumatra mkowap, mmekabidhiwa kuangalia eneo hili linakwendaje ikiwa ni pamoja na kuangalia mambo ya usalama,mnafika maeneo husika au mnaishia hapo dzm tu? jitihada zifanyike tusiendelee kupoteza mawaziri na wabunge wajao wajameni?? inasikitihsa sn.
ReplyDeletemungu awalaze mahali pema amen....
terrible, poleni wazazi, ndugu na jamaa.
ReplyDeleteWajualo ni kukusanya ela za uchaguzi mengine wanafumbia macho sio kama hawaoni
poleni wazazi Mungu awatie nguvu katika kipindi hiki kigumu
ReplyDeletenyie viongozi jamani acheni kula hela za kodi na kusahau watu kiasi hiki
Afu wenyeji tuking'ang'ania kuishi kwenye nchi za watu wanasema turudi home tulijenge taifa, taifa lenyewe ndo hilo halina hata boti ya kubebea watu, lol! inasikitisha sana. swali bro Michuzi hivi hii serikali inasoma malalamiko yetu through this blog au tunalia tuu bure..
ReplyDeletekwa kweli natumaini kwa sasa hawa sumatra wanatakiwa wabinafsishwe, unajua hakuna kitu kibaya kama utakuwa huna mbinu mpya ya kuweza kudhibiti matukio hasa ambayo yanawezekana kutatuliwa, leo hii kuna magari ambayo hayana mikanda lakini kwa kuwa ni ya fisadi fulani ambaye yupo serikalini basi hakuna wa kumfanya lolote.
ReplyDeletewizi na ubadhirifu wa rasilimali zetu ndio chanzo cha matatizo yote haya, viongozi wao wapo kwa ajili ya kuiba tu na sio kuangalia usalama wetu.
poleni wafiwa na mungu yupo nanyi
Poleni wafiwa
ReplyDeleteRoho za marehemu zipate rehema kwa Mungu na zipumnzike kwa amani. Amina
Hivi we unaesema hutaki kurudi nyumbani kwakuwa hakuna maboya kweli umemaanisha au?
Tusiwe wabinafsi tuwe na upendo kwani siajabub wewe ukirudi nyumbani ndo utakuwa mwenyekiti mzuri wa kijiji