Warembo washiriki wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakipita kando ya daraja la mto Wami lililopo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani leo walipokuwa safarini kuelekea mikoa ya Kilimnjaro na Arusha katika mbuga za Wanyama na vivutio vingine vya Utalaii
Baadhi ya Warembo washiriki wa Vodacom Miss Tanzania 2010 wakipiga picha kando ya daraja la mto Wami lililopo Wilayani Bagamoyo Mkoani Pwani leo walipokuwa safarini kuelekea mikoa ya Kilimanjaro na Arusha katika mbuga za Wanyama na vivutio vingine vya Utalaii.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Ankal!
    Pole na kazi. Mie naomba ubandike kwenye globu ya jamii wagombea ubunge toka chama cha CHADEMA ambao ndo wapinzani wakubwa wa CCM. Ulibandika wagombea kupitia tiketi ya CCM hivyo usitubanie wagombea toka CHADEMA tunataka kujua chama kipi kilicho na wasomi na watu wenye busara watakao weza kupiga jeki maendeleo ya nchi yetu.

    ReplyDelete
  2. Mwe mapozi mpaka mbugani! Ngoja siafu wawaingie ndani ya sarawili zenu!

    Na wewe nawe hao Chadema sana sana viti vya kwenye majimbo wakipata ni 10 basi! Wagombea wagombea nani ana shida nao bwana, yaani nyie mkilala siasa, mkiamka siasa, maisha yenu yanaevolve kwenye siasa mpaka mnaboa sasa. Hao hapo juu ndio wagombea wa Chadema oops sorry wagombea wa Miss Tanzania! Mambo mengine mnayatafuta wenyewe!

    ReplyDelete
  3. No future after this.

    ReplyDelete
  4. We Anon wa pili acha uchizi,nyie ndo wale wale.

    ReplyDelete
  5. We Anon wa Fri Aug 20, 11:32:00 PM

    hivi hujui tayari viti 80 CHADEMA mmeisha kosa kati ya 239 wakati hata mechi yenyewe bado haijaanza. Kivipi? Wagombea 10 wa CCM wamepita bila kupingwa. Viti 70 hamkuweka wagombea. Ndiyo mnategemea mshinde. Hebu acha hizo wewee!! Hee!! Umeona siku Slaa anarudisha form kaja na mbwembwe za kimarekani. Wakati CCM ilikuja na wananchi wa kawaida grass roots. CCM imejipanga bwana.

    Tayari mMnyuka kaanza kulia oh sijui watu wetu wamefanywa nini.

    ReplyDelete
  6. Astakafiluraahh!!

    Jamani mwezi mtukufu huu!! duh!mbona mwatuhatarishia ndoa zetu ..ebooo!

    ReplyDelete
  7. nchi kila siku ukiamuka ni mambo ya miss tu..mmh nchi hii sio siri inakoelekea ni kubaya sana. hivi hakuna mambo mengine ya kijamii ya kufanya? je jamii na vizazi vyenu mnavifundisha nini/?/
    ]tuko nje ya nchi ambazo zimeendelea lakini hawana mambo yya miss kila siku..
    hata wanapokuwa navyo havipewi kipaumbele kamataifa letu linavyofanya...
    jamani tubadilike mendeleo hayaji kwa kuendekeza mamiss..huu ni uchafu mtupu..

    ReplyDelete
  8. Kama warembo wenyewe ndo hawa basi kwa mara nyingine mwaka huu hatuambulii chochote miss World

    ReplyDelete
  9. ANKAL BLOG YAKO ANABIDI UKAZE BUTI KWA SANA ANGALIA MAMBO YA MSINGI AMBAYO YATATAKIWA WATU WACHANGIE MADA ILI KUWEZA KUSUKUMA GURUDUMU LA MAENDELEO.
    ANGALIA KAMA STESHENI YA REDIO YA CLOUDS WAO WAPO KIMASLAHI YA WATANZANIA.
    BADILIKA SIO KUTULETEA MAMBO YASIO KUWA NA MSINGI, WAREMBO WANAZALISHA NINI?

    ReplyDelete
  10. Watu wansema kwamba mkoloni alipokuja babu zetu walidanganywa na kioo wakatowa kila kitu, je kuna tofauti gani ya enzi za mababu zetu na sasa, kwani kila mtu anaiga tu hata kama hakina maana kinapewa kipaumbele. Je tunatofauti gani kati ya enzi hizo na sasa. Kwa sababu mkolino huwa natafura nzia ya kuzubaisha watu ili achote zaidi, sasa nyie mnatangaza wanawake wamevaa vusuruali ndiyo urembo, wakati mkoloni umesahau umeshamkaribisha nyumbni kwako anchota tu taratibu, ankazana kusema ngoja tuwakelee hawa wa kuja hawajawhi kuona wanawake wamevaa vizuruali. Sisi huku tufanye haraka tuchote zaidi wakija kushtuka ni machimo tu yamebakia.

    ReplyDelete
  11. watu woooote mliotoa mada hapo juu naona mnamapungufu makubwa sana....
    kumbukeni hii globu inadhaminiwa ili iweze kuendelea sasa wadhamini wenyewe lazima watangaze mambo yao kwa jamii pia......
    acheeni lawama zisio za msingi na acheni kila mtu afanye yake.... kama ufurahishwi na mamiss usisome acheni unafiki....
    Michuzi endelea na kupost habari za kila kona ndio kinachofanya blog inoge zaid achana na watu hao wasio na uelewa wa mambo majunguuu tuuu kama walivyooo

    ReplyDelete
  12. Hawa "warembo" wote wajinga tu na hawajiheshimu. Kazi kupitishwa hadharani kushindana kama ng'ombe katika mashindano ya kilimo. Kama haya ndiyo maendeleo na "burdani" tuipe pole Afrika yetu.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...