Mshauri wa Kamati ya Miss Tanzania DK.Raamesh Shah (kulia) akitoa mafunzo kwa warembo wanaoshiriki shindano la Miss Tanzania katika semina inayoendelea katika Hoteli ya Giraffe iliyopo Mbezi Dar es Salaam. jumla ya warembo 31 wapo katika kambi hiyo (wapilI) Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania Prashant Pater, Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania George Rwehumbiza na Mkurugenzi Mtendaji wa Hoteli ya Giraffe Charles Bekon.
Baadhi ya Warembo wanaoshirikia katika shindano la Vodacom Miss Tanzania 2010 wakimsikiliza Mshauri wa kamati ya Miss Tanzania DK.Ramesh Shah hayupo (pichani) wakati alipokuwa akiwapa ushauri juu ya kuweza kujiamini katika semina inayoendelea Hotel ya Giraffe.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 12 mpaka sasa

  1. Uongozi wa tasnia hii ya ulimbwende nchini Bongo uhodhiwa na midume tu (mfumodume). Je, wakiwezeshwa wanawake kuiongoza au kushikishwa katika uongozi, si inaweza kufanikiwa zaidi?
    Ni hoja ya haja/haja ya hoja tu

    ReplyDelete
  2. Hii ni biashara binafsi ya watu, akina Hashim Lundenga. Hakuna chama cha kitaifa wala wakala wa serikali. Kama kuna mwanamke anataka kufanya na yeye aanzishe ya kwake. Msipende siasa kwenye kila jambo.

    ReplyDelete
  3. gud idea, kwanini wanawake wasiongoze huko? tena hata rushwa za ngono zitapungua, wizara ya wanawake na watoto waingilie kidogo

    ReplyDelete
  4. Duh! Huyu mrembo wa kwanza hapa kulia ni shughuli. Sijui wa wapi? Macho na kifua viko sawa hasa. Namtakia kila la kheri mwaka huu.

    ReplyDelete
  5. we anony unayesema ni biashara binafsi, hata kwenye biashara binafsi serikali inatakiwa kuweka sheria inayojali haki sawa kwenye ajira sio tu kuajiri wanaume kisa ni binafsi.au wewe hujui maana ya equal opportunities?? na sex discrimination at work?? kwenye hii tasnia ya urembo kuweka mwanamke ingekuwa ni lazima ili kupunguza shutma za ngono baina ya viongozi na mabinti wanaoshiriki. na pia kuwapa mabinti confidence kwa vile mabinti wengine wanapoteza confidence wanapo ongozwa na wanaume tu.tena wanaume wa umri sawa na baba zao.

    ReplyDelete
  6. Hashim Ludenga taratibu tafadhali, waumini tuko kwenye mfungo.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  7. jamani Brother Lundenga sio kuwa anashiriki na hao watoto, ni imani tu ya kiswahili, kitu kingine hao watoto toka huko walikotoka uliza tabia zao na hapo ndipo utapata cha kuchangia, kuna walio tulia na wale maisha yao ndio yanakwenda kwa hayo matokeo.
    Brother Lundenga kajitaidi sana kuwasaidia lakini wao wakiisha kupata kajina basi utakuta ndio anataka kuwa mtu maarufu hapa TZ na matokeo yake kuambulia kichwa cha habari cha magazeti

    ReplyDelete
  8. Wanaume ndio wanajua uzuri wa mwanamke. Wakiwekwa wanawake hapo wataharibu na kuchagua mijitu isiyo na mvuto eti kisa ina tabia nzuri.

    ReplyDelete
  9. yaani watu wanadharau hata mwezi mtukufu naamini kuna waislam kibao wanashiriki haya mambo ndio maana ZANZIBAR MARUFUKU.

    ReplyDelete
  10. ANGALIA HIYO MIJIZEE HAPO MIDENDA INAVYOWATOKA UTADHANI FISI KAONA MFUPA NYIE VIBINT NYIE MH HAYAAAA.............SIE TWASEMAA ALAFU TWABAKI KUANGALIA HATUWEZI WASHIKIA FIMBO! wENYEWE MWAJIONA VILE MWAJIINGIZA MDOMONI MWA MIMAMBA HUKU MWACHEKELEAA TUU

    ReplyDelete
  11. Miss Tanzania na Ramadhan vinahusiana nn??msilete ushamba wenu hapa kama vp kaishini Saudia tuone kama hamjarudi baada ya sku mbili tu!!

    ReplyDelete
  12. anonymous 12:20pm, hakuna mshamba hapa, kasome Quran utaelewa nini maana ya mwezi mtukufu. Uwe mstaarabu acha kukashifu dini za wengine. Ushamba au la, tutajua siku tutakapofufuliwa. Asante

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...