Pole kwa kazi.
Hivi karibuni nilisafiri kutoka Bukoba kuja Mwanza kwa MV Victoria. Kilichonishangaza ni wahusika melini kutozingatia umuhimu wa kuacha wazi eneo kunakohifadhiwa "life jackets" kama ilani inavyoelekeza. Ikitokea ajali (Mungu apishie mbali) mpaka mizigo ihamishwe ndo mlango wa life jackets ufunguliwe!
Nawasilisha.
Makame
Hivi karibuni nilisafiri kutoka Bukoba kuja Mwanza kwa MV Victoria. Kilichonishangaza ni wahusika melini kutozingatia umuhimu wa kuacha wazi eneo kunakohifadhiwa "life jackets" kama ilani inavyoelekeza. Ikitokea ajali (Mungu apishie mbali) mpaka mizigo ihamishwe ndo mlango wa life jackets ufunguliwe!
Nawasilisha.
Makame
Katika hili sii mara ya kwanza kuliona ndani ya meli hiyo ya MV Victoria. Tenahapo mizigo haikuwa mingi. Mara nyingi hujazwa ndizi hadi kule juu sehemu ya kupandia Life boats. Tena eneo hilo ni pembezoni mwa quaters za mabaharia na nikaribu kabisa na chumba cha Nahodha Capt Mwasa kama bado atakuwa anacomand meli hiyo. Ni vyema watu wa sumatra wakawa na kaguzi za mara kwa mara nyakati hizi maana sidhani kama watu woote wanaopanda chomboni wanakuwa na tahadhari ya hali gani?
ReplyDeleteTunakushukuru sana mdau kwa kutuelimisha na kutupa taswira halisi
ACHA UNOKO, ILI WATU WASIWEKE MIZIGO WAKOSE NAULI ZA MIZIGO, ACHA KUFUATILIA KAZI ZA WATU
ReplyDeleteAnony wa pili yaonekana unamazowea ya kusafiri kwa punda ama baiskeli. Hujawahi kupanda melini ukakutana na dhoruba. Huo sii unoko wala kufuatilia kazi za watu ni suala la tahadhari tu!
ReplyDeleteajali haina kinga banaaa!!!!
ReplyDeleteNYIE MNASHANGAA NINI SASA HEBU NENDENI MV MAGOGONI NA MV KIGAMBONI MJIONEE LIFE JACKETIS ZIMEFUNGIWA NA VIRO,SOLEX HADI KUFURI ZIMESHIKA KUTU.SINA KAMERA NINGEWALETEA PICHA ,KAMA YUPO MWENYE KAMERA AKAPIGE HATA SASA.SIKU AJALI IKITOKEA NI YALE YALEEEEEEEE
ReplyDeletemimi kaka misoup ndizi hizo tu mimi hoi na miss kweli kweli, Nshamba kwetu
ReplyDeleteHuyo Anony no 2. Nenda kanunue kitabu "Sitasahau MV Bukoba" Ndio utajua ukiwa makini, ajali inakingika. Tunasubiri mpaka watu wafe ndio mamlaka husika ianze kusema meli ilijaza kupita kiasi.
ReplyDeleteKINGA IPO UKICHUKUA TAADHALI
ReplyDeleteAnon wa pili na wa nne nyie kweli ndo wale wajinga wajinga hamjali maisha na usalama wa watu.Eti ajali haina kinga,mtaendelea kufa kijinga jinga sababu ya mentality kama zenu.Anon wa pili hujawahi sikia tahadhari yakinga ajali? Watu wengine kweli ni mambumbu.Kama ajali haina kinga mbona unasubiri magari yapite ndipo uvuke barabara?
ReplyDeletenadhani hamna haja ya kubishana na anony wa pili,sababu nimegundua kwamba hata life jacket hajui ni nini,na inakazi gani,so mtu wa hivyo mtabishana mpaka asubui,sidhani hata kama anakumbuka issue ya mv bukoba tulivyopoteza wapendwa wetu,yes kifo hakiepukiki lakini lazima tuweke tahadhari,tusikae kusema tu mungu atasaidia,tukumbuke usemi kwamba JISAIDIE NAMI NITAKUSAIDIA.the thing is tahadhari imetolewa na wahusika sababu ni watu wenye akili zao ujumbe wataupata na wataufanyia kazi,keep it up mr,michuzi blog yako inatupa mambo mazuri.BIG UP MEN!!!
ReplyDeletewhy I bother you never publish my comment!!!
ReplyDeleteanoni (2) na (4) mna vichwa??
ReplyDeletendani ya vijichwa vyenu kuna kitu?? basi kama huna la kusema si ukae kimya tuuuuu??
kakulazimisha nani kuandika uchafu??
tumieni akili zenu.
Ajali ikitokea watu wengi watakufa shauri ya kukosa life jackets! Jamani, hii si mchezo, wenye meli wapigwe faini kali kusudi iwe fundisho. Pesa za haraka au maisha ya mtu nini ina thamani zaidi?
ReplyDeletekuna mijitu ya ajabu inapenda kutoa comment kukamilisha ujinga wao.
ReplyDeleteyani mtu na akili zako timamu huwezi kuona umuhimu wa hii post?
iki ni kitu cha kusikitisha naona hatujajifunza chochote baada ya ajali ya MV Bukoba including Nahodha wa meli ya Victoria ambaye anapaswa kuchukulia maisha ya abiria wake seriously. Tanzania hatutabadilika mpaka hapo tutakapoelimika kujua haki zetu asilimia yetu kubwa tunafikiria haki inanunuliwa.
ReplyDeleteNINA MSHUKURU SANA HUYU ALIYETULETEA HIZI PICHA. I HOPE WAHUSIKA WATA LISHUHULIKIA HILI JAMBO. HII NDIO SABABU AJALI ZETU HU UWA WATU WENGI KWASABABU YA UZEMBE KAMA HUU. WALE WENYE KUTOA COMMENTS ZA KUONA HILI JAMBO NI SAWA NINAFIKIRI WANATOA HIZO COMMENTS ILI WAKASIRISHA WATU. MY DEAR THIS IS NOT FUNNY.
ReplyDeleteNajua michuzi utaibana tu hii! Ila ukweli lazima usemwe na utasemwa tu!
ReplyDeleteHapa ajali ikitokea na watu wakashindwa kuingia na kuchukua hayo maboya ya usalama, na wakafa.
Tutasema wametolewa kafara! Au upepo mbaya sana ulipita pale! Au watu wamechukuliwa na majini! Au....
Watanzania sijui lini tutaamka na kujua sasa ndio wakati wa kua na heath and safety na sio kusema eti "ajali haina kina banaa!"
Tatizo letu ni elimu na kuchukulia mambo kienyeji enyeji tu!
Na ndio jibu la umaskini wetu!
Na ndio maana hata CCM hawana wasiwasi, wanajua pamoja na ufisadi, ufujaji wa mali ya umma na kutokuwajibika, bado tu tutawachagua!
Mimi Hapa Nakuja na Solution Tatu!!
ReplyDelete1. Tuna haki ya kuwaponda hawa wasioelewa na kusema ajali haina kinga sijui ulaji hawa ndio ni watovu wa Mawazo na Hawastahili katika Jamii yenye kuhitaji mabadiliko ila wanaowapond pia watoe mawazo yao juu ya mada sio mtu anakuja kuponda tu!!
2. Wenye mizigo wawajibishwe na wahudumu wa meli ikiwa ni pamoja na faini au kutaifishwa mizogo yote inayokutwa eneo hilo hii ingewastua hata wale wanaojifanya kutia pamba masikio yao!!
3. Kama wahudumu wa meli wanashondwa kuwawajibishwa hawa wazembe wachache basi wao wawajibishwe na mamlaka husika (sumatra)Ikiwa ni pamoja na faini au kuachishwa kazi kabisa.
ahsanteni.
Halafu meli ikibinafsishwa na mwenye meli akiajili wakenya, hawa wazalendo watakaofukuzwa kazi kwa kuufumbia macho uzembe huu wataanza kulalamika kwamba "ooh... kwanini wanaajiri wakenya". Wakati ni dhahiri kwamba uwajibikaji unawashinda.
ReplyDeleteNinachopenda kusema ni kwamba kuna kitu kimoja ambacho nadhani watu wengi wanshindwa kuelewa, kwamba hakuna ethics in work place, hakuna msisitizo wa ethics mhalia popote kwenye mafunzo. Sasa unatarajia nani atamkaguwa nani, nani atamlipa nani kma akyna ajali, wakati nahodha ni mtoto wa ??????. Na kingine hakuna shirika la uma linafuta ethics za kazi, kama kungekuwa na hilo tungekuwa na umeme kila siku, tungekuwa na maji kila kitongoji, wezi wangekuwa jela na siyo majumbani. Majambazi ndiyo wanioendesha miji, hakuna haki kwa wananchi. Ni saa ngapi mtu atajali kwamba anabiria na ni muhimu kuwatunza vyema na kuwaheshimu. Michuzi usibanie hii. Watu wengi tunanyanyasika kila kona tunahitaji msaada lakini wengine tutakufa hata haki hatutaziona. Mungi ibariki nchi yetu tuangalie sisi walala hoi labda kuna siku mtu atasimama na kusema imetosha tunahitaji kizazi chenye mwelekeo.
ReplyDeletena wakenya twanazidi kumiminika tanzania yenu,,,nyie ngojeni tutawafunza adabu na kazi kisawa tu
ReplyDeletelol iyo miche ya miti ni mizuri sana made in BK
ReplyDelete