Pole na kazi kaka Michuzi,
Nilikua naangalia maeneo mbali mbali ya utalii Tanzania, ila nilisikitishwa nilipokutana na hii "clip" ya Ngorongoro. Ukiifungua hii clip utasikia wimbo unaimbwa ambao unawakaribisha watu Kenya.

Kwa wadua nadhani mnaufahamu ule wimbo wa "Jambo.. wageni mwakaribishwa Kenya yetu hakuna matata" Hebu wape wadau waone nadhani huu ni wizi...kwa mtu asiyejua anadhani hiyo Ngorongoro ipo Kenya.

Mdau Australia

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 22 mpaka sasa

  1. Ankal naomba mjomba KAMAU aweke Comment hapa ikibidi mpigie hata simu tumsikie ufisadi unaofanywa na watu wa jamii ya kwao..

    ReplyDelete
  2. MIKOPO MINGINE NI KIINI MACHO SERIKALI ISITUGHILIBU.HAWA JAMAA KAWAIDA YAO NI KUKUNUNUA ARDHI KUBWA NAKULIMA KILIMO CHA KISASA NA MAZAO YOTE WANAPELEKA KWAO,HAWA NDIO WALIO SABABISHA MACHAFUKO MORTIUS MAPAKA DJ AKACHUKUWA NCHI,ENZI ZA MWALIMU PASPORT YETU ILITURUHUSU KUSAFIRI DUNUA NZIMA ISIPOKUWA SOUTH AFRICA(DURING APATHIERD)NA KWA HAWA JAMAA LEO TANZANIA MNASHINDWA HATA KUANZISHA HOJA AU KUUNGA MKONO KUONDOLEWA KWA VIKWAZO VYA KIUCHUMI KWA NDUGU ZETU WA CUBA WALIOJITOA MUHANGA KWA AJILI YETU BADALA YAKE KAZI KUONYOOSHA MIKOPNO KUPOKEA CHENU KWA NJIA YA DANGANYA TOTO THIS IS TIME BOMB.

    ReplyDelete
  3. Tusikurupuke tu na kuanza kuwatupia madongo Watani wa Jadi. Nadhani tag na jina la video vinasema "Tanzania Ngorongoro." Na aliyetengeneza filamu ni mtu kutoka Ulaya (Czech?) (kaweka picha na contacts zake mwishoni).

    Alichofanya ni kuweka wimbo, ambao (bahati mbaya) umeimbwa na Watani wa Jadi. Kosa..

    Anyway, kuna clips nyingine kutoka kwenye mbuga zetu hapa:

    http://vijana.fm/tag/tourism/

    ReplyDelete
  4. MIMI NASHANGAA SANA WANAO UNGA MKONO SISI KUSHIRIKIANA NA WAKENYA WALE WATU SIYO WAZURI KIHIIIIVYO!

    ReplyDelete
  5. This is a lovely clip of Ngorongoro...It also shows that Ngorongoro is indeed in TANZANIA. The one who made the clip erred in using the "jambo" song which talks about Kenya. I don't see any WIZI here from our watani...ni ulimbukeni tu wa watu wengine kutokufanya analysis ya which song befits the video clip.

    ReplyDelete
  6. Mimi hapo sioni tatizo sana maana hiyo clip inavyoanza kuna maandishi wanasomeka Ngorongoro-Tanzania so nadhani huo wimbo siyo ishu sana.

    ReplyDelete
  7. Jamani, kabla ya kuanza kuwalaumu watani wetu, hebu tujiangalie sisi wenyewe tumefanya nini kutangaza nchi yetu. Sisi kazi yetu ni kula nchi tu. blah Blah nyingi lakini hakuna kazi.

    ReplyDelete
  8. Kiswahili ndiyo kabisa. Wanasema ni chao na Wabongo tumezubaa tu. Jamani tuitetee nchi yetu, hawa watu ni wezi. Nashangaa kwa nini hata tunawaendekeza kwenye Jumuiya ya Afrika Mashariki?

    ReplyDelete
  9. TATIZO NI KUWA WENYEWE TUKO NYUMA SANA TENA SANA KWENYE KUJITANGAZA! KAMA TUKIWEZA KUJITANGAZA WATAACHA KUFANYA HIVYO!

    ReplyDelete
  10. Badalal ya kulalamika tuchukue hatua kutangaza kuwa ngorongoro ni Tanzania na tundengeneze clip kama hii... tuache kulalalamika jamani kenya kenya ahahhaha inachosha..njia pekee ni sisi kujitangaza period...unasema huu ni ufisadi wakati watu ndio wako marketing hapo .. watanzania tutoke kwenye ujamaa jamani dunia ya ubepari haona cha huruma huruma tulizozoea kwenye faulo watu wanancheza na sisis tujifunze kuwa sharp kidogo kaaa

    ReplyDelete
  11. Wabongo tunapenda kulalamika sana. Mimi hapa sioni ufisadi wowote wa wakenya. Kwanza inaonekana aliyeshuti hii video na kui-publish wala si mkenya, ni huyu mzungu ambae amejitambulisha mwishoni mwa hii video. Inawezekana yeye mwenyewe ndio alikurupuka na kuweka huu mziki ambao unaweza kuununua hata hukohuko Ngorongoro na serengti. Kaseti hii ya bendi ya Safari Sound ya Kenya yenye nyimbo hizi inauzwa sana kwenye mbuga zetu za wanyama hata zaidi ya kaseti za miziki ya Tanzania. Nyimbo zake zimekaa kitalii zaidi na zinavutia na wauzaji wa kaseti wa huko wanafaidika sana nazo. Pengine jamaa mzungu kashoot video, kanunuwa kaseti na aliporudi kwao ndipo akaimix na hizi nyimbo. Wabongo tuache kulalamika ovyo kwa kila kitu, tuchangamke na tuchape kazi.

    ReplyDelete
  12. What the ***k?!!!!! Who the hell did this crap???? Awajibishwe haraka, tena kwa hasira kabisa!!!

    ReplyDelete
  13. Wewe mdau wa Hausitilaria na mchangiaji wa kwanza wchenihuo wivu wenu usio na akili. Widhara inayousika na hutarii TZ wamerara 4.4.4. Wenzenu wakijitangazia vivutio vya kuwafanya wapate watarii mnaanza kuria na kuraramika, hoo sijuhi wanatangaza vivutio vyetuu, hooo sijuhi niniii! Wacheni izoo, endereeni kurara, na kugawana pesa zinazotorewa na steti kwa hajiri ya kuhendereza hutarii. Mtambaki kuraramaa wee sinku nzote!

    Nawasirisha!

    Chiaz Mchiiiz!

    ReplyDelete
  14. Shame on u kenyans. I thing it's time for these stuffs to be discussed ktk hiyo East african communuty. This's not being smart, ni wizi kwa sababu wakenya wanawapotosha watu. I MUST SAY THEY ARE JEALOUS OF WHAT WE HAVE. How is it possible??

    ReplyDelete
  15. Ngorongoro imeongezwa kwenye World Heritage sites na UNESCO hivi karibuni.

    Sasa ninyi watiziii kama hamuwezi kuitangaza kwa dunia mnalalamika nini?? Na kawaida mwamba ngoma uvutia kwake!!

    Hivyo hakuna haja ya kulalama, ni kuitangaza kwa nguvu zote tu!! Uongo utajitenga na ukweli, na dunia itajua mulongo ni nani!!

    ReplyDelete
  16. Wakati mwengine hadi naona aibu kujitambulisha kuwa ni mtanzania mbele ya wakenya kwasababu ya mtu kama huyu aliye tuma hii clip. sasa hapo kuna kosa gani, kwasababu hii clip iko kwenye youtube na imetumwa na mzungu mmoja anaitwa Libor O. Novotný, kutoka Szech Republic. youtube channel yake ni hiihttp://www.youtube.com/user/libornovotny#p/a/83EDC2602D967EE8/2/FDi5C3CCwRw Tena inawezekana hata kiingereza hakijui vizuri.
    Huo wimbo unaoimbwa ni maarufu sana kwa watalii ndio maana huyo jamaa kaamua kuuweka. ambao nikweli ni wa Kenya, lakini sio Mkenya aliye rekodi hiyo video.
    Watanzania wenzangu, hebu tuache kulalamika ovyo. Natukubali kwamba wakenya wametuzidi ujanja linapokuja swala la kujitangaza na kufanya biashara.

    ReplyDelete
  17. Mara nyingi tunalilia kuitangaza Afrika, kama moja kwa muktadha wa “pan-Africanism”. Leo hii, ndoto hiyo iko juu (Muammar Khaddafy wa Libya).

    Je, kuna uwezekano wa nchi moja kuvalishwa joho la nchi nyingine, kwa minajili ya kufanikisha ndoto hiyo?

    Kwa nini ninauliza swahili hilo? Najaribu kuchangi jibu kwa kero iliyojitokeza katika video hiyo.

    Video hiyo ilitengezwa na Mzungu mmoja, Libor Novotny, wa huko Czechoslovakia ya zamani.

    Jamani, kuwasakama wa-Kenya eti ni wezi katika video hii, ni mawazo mafinyu sana, tena sana!

    Ingawa huyo Mzungu anatangaza utalii wa Tanzania katika video zake nyingi, kama hiyo video, huu ni umbumbu wa wa-Ulaya kuiangalia Afrika, kama ni nchi moja!

    Naandika nikiwa New York. Hapa New York, kuna tawi la kampuni ya kutengeza muziki ya Sterns (makao makuu yake ni mjini London).

    Siku moja nilikuwa hapo dukani Barabara ya Chambers huko down town. Nikutana na Mzungu mmoja aliyekuwa akitafuta “background” muziki kwa ajili ya filamu ya Hannibal iliyokuwa inatengezwa wakati huo.

    Mzungu huyo aliniuliza endapo ninatoka Afrika na ninajua wimbo mzuri ambao ungeoana na hadithi ya Hannibal katika filamu hiyo!

    Mimi nilimweleza Afrika ni Bara kubwa tena la pili duniani. Kuniuliza kama ninajua muziki wa Afrika unaooana na Hannibal itakuwa ni vigumu sana. Ni sawa na kutafuta muziki wa "European" unaooana na hadithi ya "Robin Hood"!

    Endapo nitakushauri muziki wa kutoka, kwa mfano, Tanzania, na wewe unataka mkitadha wa Hannibal, ni sawa na kupata muziki wa ki-Italia kwa ajili ya filamu ya Robin Hood, the Robber!

    Natamati kwa kutamka kuwa kuwalaamu wa-Kenya katika video hii, sio jambo zuri! Hata hivyo, tuamke kuitangaza Tanzania yetu! Bado kuna ombwe kubwa katika kuitangaza Tanzania yetu ulimwenguni. Tusipoliziba hilo ombwe, wengine (kama Libor Novony) wataliziba!

    Kuna usemi tuliokuwa tunautumia katika somo la fizikia kuhusu hewa: Air abhors vacuum!

    ReplyDelete
  18. WANA HAKI YA KUTANGAZA KUWA UPO KENYA,KWA KUWA KENYA NI SEHEMU YA EAC,PILI NILISHAWAHI KUCHANGIA HOJA YA TANZANIA KUJIUNGA NA SOKO LA EAC,UKWELI NI UPO PALE PALE KWANZA MAKAMPUNI YA KITALII YA TANZANIA YATAPOTEA AU KUFA KABISA WATALII WATAHUHUDUMIWA NA MAKAMPUNI YA KENYA,SABABU >MFANO" UWANJA WA JOMO KENYATTA KWA SIKU UNAPOKEA NDEGE ZA ULAYA NA ASIA ZINAZOLETA WATALII KATI YA 35-40 KWA SIKU KILIMANJARO INAPOKEA 2-3 KWA SIKU.HIVYO WATALII HAWA WATAHUDUMIWA KWA KUINGIZWA BILA KULIPA CHOCHOTE KWA TANZANIA,MAKAMPUNI YA KENYA NDIYO YATANUFAIKA

    ReplyDelete
  19. Asahihishwe mara moja!! Period!! Hatutaki hadhithi ndefu hapa. Unaweza kupima athari za hii clip??

    ReplyDelete
  20. mnapiga porojo tu.tengeleza clips yenu na wekeni hapo.musiki bongoflava
    full stop

    ReplyDelete
  21. kama hamchangamki unategemea nini.tuimbe kilimanjaro.watanzania.swala la kujitambulisha.kibiashara badoooo
    kabisa......come on kenya...

    ReplyDelete
  22. Nafikiri tunalalamika bila kujua linalotufanya kulalamika, watanzania lazima tukubali kwamba wakenya na waganda wapo juu hasa biashara ya ytalii na viwanda, sisi tunatatizo la utangazaji kwasababu ya kila mtu kujijua na maisha yake huku akiwa kwenye ofisi za serikali na hili ndilo lililoleta rushwa Tanzania, mfano katika world cup Tanzania walitangaza nini? jibu hakuna lakini huo ulikuwa muda mzuri wa kutangaza mbuga zetu kama serengeti, ngorongoro na kadharika.
    Katika hili kenya wanafaidi airport fee, landing fee, hoteli kwa muda ambao wageni watakuwa pale, lakini hawezi kupata entrance fee katika oluduare gate kuingia Ngorongoro au kukosa kulipa fee ya kuingia ngorongoro crater pamoja na hotel za ngorongoro wildlife, sopa lodge, crater lodge, simba camp site na nyinginezo, na hizi hotel zinalipa tax serikalini kama levy, sasa hapa kuna tatizo gani? ila nimefurahi sana kuona hii clips kwasababu nimefanya ngorongoro wildlife lodge kama steam engineer kati 1991 mpaka 92, hii sehemu kama nyumbani na kila mwaka lazima niwe pale, kwahiyo mdau mwenye malalamiko jitahidi utembelee hili eneo wacha ulalamishi.
    Mdau uk.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...