MECHI ya vigogo wa soka Simba na Yanga kuwania ngao ya hisani itafanyika kesho saa 10 na robo uwanja wa taifa.
Mchezo huo ambao ni lazima bingwa apatikane na kukabidhiwa ngao hiyo kingilio kimepangwa kuwa shilingi 40,000 kwa jukwaa la VIP A VIP B shilingi 30,000 VIP C shilingi 20,000 viti vya rangi ya chungwa shiling 15,000 nyuma ya magoli shilingi 10,000, viti vya blue shilingi 7,000 na kijani shilingi 5,000.
Mchezo huo utachezwa kwa dakika 90 na iwapo hawatafungana wataenda mikwaju ya penati na mshindi atakabidhiwa ngao, ikiwa ni kuashiria kuanza rasmi kwa Ligi Kuu ya Tanzania bara iliyopangwa kuanza kutimua vumbi Jumamosi ijayo Agosti 21.
Timu ya Mtibwa Sugar ya Morogoro ndio ya kwanza kutwaa ngao hiyo mwaka jana baada ya kuinyuka Yanga mabao 2-1 baada ya mashindano hayo kurejesha, mara ya mwisho yalifanyika mwaka 2001 na Yanga ilishinda mabao 2-1 dhidi ya Simba.
Mabao ya Yanga yalifungwa na Edibily Lunyamila na Yusuf Tigana wakati la Simba lilifungwa na Steven Mapunda.
--------------------------------
MICHUZI POST IMECHIMBA HISTORIA ZA YANGA NA SIMBA PAMOJA NA MAMBO KIBAO AMBAYO MASHABIKI WOTE WA TIMU HIZO KONGWE MNGEPENDA KUJUA NA KUHIFADHI KAMA KUMBUKUMBU.
JAMANI EE NAOMBA NISAIDIWE. HIVI HII NI NGAO YA HISANI AU NGAO YA JAMII?.
ReplyDeleteNASHINDWA KUELEWA MAANA MAGAZETI/BLOGU ZOTE ZIMEANDIKA NI NGAO YA HISANI AU NI KWA SABABU IMEZOELEKA HIVYO?.
MIMI NAFIKIRI NENO ZURI NI NGAO YA JAMII.NAOMBA MAWAZO YENU
KATI YA WEB ZOTE NILIZOTEMBELEA JANA NA LEO NI MOJA TU AMBAYO IMEANDIKA KUWA HUU MCHEZO NI WA NGAO YA JAMII NA WALA SI NGAO YA HISANI KAMA ILIVYOZOELEKA KABLA.
ReplyDeleteWAANDISHI INABIDI MTUSAIDIE SISI WASOMAJI.MIMI NAFAHAMU KUWA MCHEZO WA JUMATANO KATI KA SIMBA NA YANGA NI MCHEZO WA NGAO YA JAMII.
Tanzania kwa kuiga bwana!
ReplyDeleteEbwanaee Leo Simba ndo Watajuta kumfahamu Assamoh coz atakayo itoa ni balla
ReplyDeleteMungu wangu weeee.Waingereza ama ligi ya Uingereza imetuharibu. Blame on Television. Ligi yetu ilikuwa inaanza january sasa inaanza August kama vile na sisi tuna summer na winter seasons.Wenzetu wanafanya vile sababu ya Climate waliyonayo sisi ni kufuata mkia tu hatujali jiografia yetu wala nini.Muda si mrefu shule zetu nazo zitaanza September mpaka May.
ReplyDelete