Kwanza nakupongeza kwa kutupasha habari mbali mbali ambazo nyingi ni za kutuburudisha na kuelimisha. Ni ukweli usiopingika kuwa blog yako inasomwa na watu wengi sana, hasa sisi watanzania tuishio nje ya nchi. Lakini pia tukumbuke kuwa blog yako ni kioo cha jamii, na baadhi ya vijana wetu wanaamini kila kinachoandikwa kwenye blog hii ni sahihi.
Hivyo basi ni changamoto kwako kuhakikisha lugha na taarifa zinazotumika katika blog yako ni sahihi kwa kiwango kikubwa. Mimi naomba nigusie matumizi ya lugha inayotumika hasa wakati tunapochanganya maneno ya kingereza na kiswahili. mfano:Chuo kikuu cha University of Dar es salaam, hapa maneno yamerudiwa, chuo kikuu maana yake kwa kingereza ni University.
Mfano mwingine ni barabara ya Ali Hassan Mwinyi road, hapa utaona barabara maana yake kwa kiingereza ni road. Lugha kama hizi zimekuwa zikitumika mara kwa mara na hivyo kuleta mkanganyo wa lugha ambao si sahihi.
Mdau Ruger wa Ughaibuni

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 37 mpaka sasa

  1. we ruger kama umekosa la kufanya plse bora upotee kabisa katika blog ya jamii, cos unaonyesha uwezo wako ulivyo limited, lugha ya kisanii haifuati mpangilio maalumu ni hio inatumika ili kuwapa watu flevour, na kufanya habari isiboe, so kama unataka sehem iliyo andikwa kwa rugha fasaha nenda kanunue vitabu vya baba wa taifa(mwl nyerere) kule nadhani ndio utakupenda but huku kwenye blog yetu tuachie wenye nayo na kama ndio mgeni ur wellcome but usitubadilishe

    ReplyDelete
  2. Na wewe nenda kamalizie English course yako ufanye mitihani ufaulu ili uanze shule yako ya Masters huko uliko. Usitake kujifanya Mwalimu wa lugha hapa wakati wewe mwenyewe mwanafunzi. Hicho usichokielewa ni nini sasa?

    Tatizo umetoka huko sijui Karatu sijui Hannang hakuna mtandao wala nini, umefika shule ughaibuni unakutana na blogu ya jamii. Hivi unataka kusema miaka yoote hiyo watu walokuwa wakisoma hii blogu hawakuona hayo au hawajui lugha?

    Wahi wahi mitihani ya lugha kabla ya shule kuanza i njiani na bado uko na assignments kibao.

    Lakini karibu globu ya jamii, ukienda kwa wenye chongo nawe.........! Mana hata huko uliko utakutana na ambayo hujayazoea kama vile hairuhusiwi kutema mate hovyo hata kama unayo unayameza tuu! Usisalimie watu hovyo, usichukue vitu sio vyako kwenye friji mnayoshea, usichukue chumvi ya mtu, hakuna kuomba chumvi, ukialikwa lunch wende na pesa yako! Na mengi mengineyo tofauti na ulivyozoea.

    ReplyDelete
  3. Wakuja mwingine huyoooo! karibu sana kijijini.

    ReplyDelete
  4. achana na blog hii, own by jocker! nothing serious inside!

    ReplyDelete
  5. Naomba nimsaidie Ankal kwa hili,, mdau umefurahi na mada yako ambayo hio ni kielelezo tosha kwaAnkal kuwa hii ni Globu ya jamii kwa maana kuwa ujumbe mmoja kila mtu anauchukuia tofauti. kwa ufupi ni kuwa mchanganyiko wa lugha ndio lugha pekee amabyo wadau wa blogu ya jamii tu wanauelewa kama umegundua mchanganyiko huo hutumika katika globu hii tu na ndio lugha wadau wanapenda kuisoma na sio kimakosa ni makusudi kabisa,,, hii ndio art ya ankal (unique) ukweli ni kwamba hapa unapata news za habari muhimu katika hali rahisi au tulivu au kama burudani.. sio hayo tu kana maneno kama Globu badala ya blog ,, lebo, yalee yalee, libeneke,, mwanaharakati, mpiganaji hizo ndizo codes za ankal.. lazima uwe naye pamoja ili uweze kupata taswira,,, kama sivyo ataelezea mdau namba 1 mwenyewe
    au sio Ankal?
    Nashe

    ReplyDelete
  6. kwakweli watu wengine wamekosa la kufanya. kama unaona watu hawatumii lugha vizuri mbona usianzishe blog yako. michuzi akikubaliana na hilo wadau wengi maoni yao hayatakua kwenye hii blog.

    ReplyDelete
  7. Mdau karibu sana ktk libeneke la jamii.maana yaonekana kabisa kama ni mgeni.haha
    let it flow kwani hapa hilo suala la lugha gongana limeshika hatamu since few years back.mbona umesahau ile "my wife wake ama my husband wake"?and many more!!

    ReplyDelete
  8. Ruger pole, inaelekea wewe umetoka bongo siku nyiiingi. Hiyo ndio lugha yetu humu ndani sio kama Ankal anakosea, ni humor ya michuzi blog kama kusema my wife wangu. Lazima uliondoka bongo mwaka 1979 wewe labda useme kwa kuchapia majina ya watu na spelling kwa ajili ya haraka lakini daraja la salender bridge? humu ndio mwake

    ReplyDelete
  9. WEWE KAA NA KINGEREZA CHAKO CHA UGHAIBUNI HUKUHUKO, HII NI STYLE YA HII GLOBU FYI. POLE KWA KUGUNDUA KITU AMBACHO SI MAKOSA WALA ILA NI STLE YA BLOG. TEHTEHTEH. GO N GET UR LIFE MDAU!

    ReplyDelete
  10. Nakubaliana na wewe kabisa. Hiki kitu kimekuwa kikinikera kwa muda mrefu. Kwa nini kurudia neno moja mara mbili kwenye sentensi moja?. Kufanya hivyo kunaonyesha au kunatoa picha kuwa mwandishi ana matatizo ya lugha, au haelewi maana ya hayo maneno ya kiingereza. Maneno kama road na university na hall yana maana yake, sio UREMBO.

    ReplyDelete
  11. Take it easy mdau, hii ni moja ya vionjo vya hii blog.Lugha ya blog isikutatize!

    ReplyDelete
  12. Watu wasiokuwa na sense ya humor ndo kama Ruger.Ina maana muda wote unaokuja hapa hujaelewa kuwa ni "utani" michuzi anavyoandika barabara ya Ali hassan Mwinyi rd?
    Hujawahi kusikia ktk maongezi ya kawaida watu wanachapia na kusema jengo fulani lipo ktk barabara ya Morogoro road?
    Acheni kuwa uptight,It's just sense of humor.

    ReplyDelete
  13. Blogu ni ya jamii, na tunaelewa kabisa misemo kama hiyo. Sioni haja ya kubadilisha lugha.... ni blogu ambayo sio ya kitaaluma, kama mtu analengo la kufahamu kiswahili fanisi...for sure this is not the place to be.

    But we love it the way it is...not too serious, it's fun and free. I love it when we call it globu, siku ya hepibesidei, barabara ya Ali hassan mwinyi road etc. A little sense of humor goes a long way.

    Michuzi eee, don't change a thing, labda comments za watu tu ndio itasaidia kama zikiwa zinasomwa na kuwa edited kabla kupostiwa. Na all stupid comments zisiwekwe.

    ReplyDelete
  14. Mdau Ruger, hiyo comment yako kwa kawaida huwa inasemwa sana either na wageni wa blog yetu ya jamii au watu wanojifanya wasomi. Kwa taarifa yako for the past 4 yrs, glob hii imeshakuwa visited by more than 9,306,343 people. Nadhani hao ni watu wengi kuliko idadi ya wapiga kura wa TZ mwaka huu. Moja ya sababu kubwa ya watu kuipenda blog ya jamii, mbali ya kushare important current information, ni lugha hiyo ambayo unayoizungumzia wewe. Ndugu yangu hiyo ndiyo lugha yetu, na wanajamii huwa tunaipenda sana kwani mara nyingu huwa inashusha pressure, na pia huwa inatuburudisha saaana wakati tunajipumzisha baada ya kazi ngumu ya kubeba box. Ankal, usiwasikilize hao kina Ruger, achana nao bro, tafadhali endeleza libeneke la jamii. Ninakuja vacation huko mwezi huu, nitakucheki offisini kwako Barabara ya Samora Road.

    ReplyDelete
  15. Mchangiaji hapo nasimama na ndugu Issa Michuzi. Ninavyochukulia mimi ni kwamba ili kunogesha uzuri wa blog, ni kutumbukiza ka utani ka namna hiyo mfano Barabara ya Morogoro Road. Siyo kwamba haelewi kwamba kuna kurudia neno la hasha.. ila ni kunogesha mambo. Na watu kama sisi tunamuelewa kwani anakuwa anafikisha ujumbe kwa njia ya utani.

    Kwa hiyo Mdau kubali mambo kama hayo na chukulia kama mfano wa katuni katika kufikisha ujumbe. Mungu akutangulie katika tafakali zako..


    Mdau....

    ReplyDelete
  16. Mi nakubaliana kwamba ni vizuri kuwe na humor (mnakumbuka tulichoka na magazeti "formal" ya "Uhuru" na "Mzalendo" yalipokuja ya binafsi tukapumua! Pili ni kuhusu makosa na spelling kwenye habari. Hili vile vile inabidi tukubaliane nalo mradi tumepeta ujumbe sababu huyu Michuzi vile vile ana majukumu mengine si kwamba siku mzima anafuatilia blog (Globu!!)tu. Vile vile naona anajitakihi ku post haabri haraka mara zinapotokea kea hiyo makosa kama hayo yanaweza kutokea...Mtu kama unataka mambo ya ki "formal", basi anzisha blog yako uelilishe jamii KIVYAKO..teh teh teh...!!!

    ReplyDelete
  17. Angalizo kwa Anon wa Sun Sep 05, 06:13:00 AM. Hiyo idadi uliyosema ya 9,306,343 si idadi ya WATU ni idadi ya CLICKS.Kwa maana kwamba kama wewe kwa siku moja ukitembelea globu mara 20 basi na idadi itaongezeka hivyo hivyo. GLOBU YA JAMII HAIKUONI SURA YAKO WEWE kwamba ni nani wakati unatembelea na kukuingiza kwenye mahesabu (counting), labda teknolojia hiyo itakuja baadae lakini kwa sasa haiko. Tuelimishane kidogo vile vile....

    ReplyDelete
  18. Kaka Ruger ..welcome to the club acha ushamba,hichi ni kijiwe tu kama vijiwe vya mitaani lakini kutokana na maendeleo ya technoljia..watu mnaweza kuchangiana mawazo kupitia mitandao..kwa hiyo lugha yoyote humu ni ryhsa hata matusi ..wee tukana ..

    ReplyDelete
  19. Nadhani huu mjadala ungekuwa mfupi kama tungemwambia mhusika kuwa Ankal alikuwa anafanya kazi na kuandika kwenye yale magazeti ya Serikali kwa ung'eng'e!... Ilikuwa Daily News? Au?

    ReplyDelete
  20. wabagambaakago bwana...! utawajua tuu.

    ReplyDelete
  21. wapiii peter nalitolea wa chuo kikuu cha mzumbe university ya kule mologolo??? ha ha haaa, kaka utaumwa sana hizi lugha ndo zinanogesha libeneke, hii blogu sio ya kina ras makunja mambo kimgambo mgambo noooo, wrong namba jaribu nyingine tena eehh!

    ReplyDelete
  22. Wadau.
    Tatizo ni kwamba sio upotofu wa kuchanganya maneno ovyo ovyo tu, ila itafika wakati watumiaji wa lugha hasa ya Kiswahili wanaamini maneno potofu kuwa ndio sahihi.
    Kwa mfano kuchnganya "L" na "R" . Siku hizi kidogo kidogo herufi "R" inatokomezwa kutoka kiswahili.
    Jipya nililoliona humu pia ni wakati herufi "H" inaachwa kabisa! k.m alikuwa "astaili" kuwa kiongozi!
    Hadi sasa Kenya wanazungumza na kuandika Kiswahili fasaha zaidi kuliko your average Tanzanian youth, kitu ambacho hakikuwepo miaka ya nyuma.
    Believe me... I fear and cry for my beloved Swahili.

    ReplyDelete
  23. ndugu ruger umetokea wapi??inaelekea huelewi maudhui ya blog ya jamii..
    japo inatupasha mambo ya jamii mbalimbali bt michuzi hatumii lugha serious..hii lugha atumiayo ndio kionjo ya blog hii...its a fun and free areas although issue zinazokuwa discussed nyingine ni serious ila in a fun and free manner..

    ReplyDelete
  24. Uliyetoa malalamiko ya lugha, uko sahihi bwana. Nasema hivo sababu kuna watoto wetu wengine ambao Kiswahili ni lugha wanayojifunza, na hapa ndipo mahali wanapoona inatumika kwa mtindo huo. Hivyo ina madhara fulani kwa wageni wanaojifunza, na watoto pia wanaojifunza, hasa nje ya TZ.

    Hata hivyo, hapa ni mahali pa burudani, kama walivosema waliotangulia hapo juu. Hivyo, ni juu ya msomaji kutambua kuwa huu ni uwanja tofauti na darasani, kitabuni nk.

    Mfano wa maneno mengine 'yanayokiukwa' kanuni za uandikaji ni haya na nayapenda sana yakitumika:-

    1) Glob(u) - blog

    2) Ankal - uncle

    3) Chuo kikuu cha university of "........" - chuo kikuu cha "------".

    4) My wife wangu - my wife (mke wangu).

    5) Dinner la mchana - chakula cha mchana (lunch).

    6) Barabara ya Sam Nujoma Road - Sam Nujoma orad.

    7) Afutarisha - atoa futari.

    8) Hepibesdei ya kuzaliwa - birthday (siku ya kuzaliwa).

    9) Mji wa Kusoma - Reading city (mji wa Reading)

    10) Bwawa la maini - Liverpool.

    etc..... etc..... etc

    MDAU....... Marekani

    ReplyDelete
  25. Karibu jamvini, tatizo ni kwamba umeingia tu bila kupiga hodi na kisha kukaribishwa, nachukua fursa hii kukukaribisha rasmi na utambue hii ndio lugha ya humu
    Aksante

    ReplyDelete
  26. We Mzee Ruger ngoja nikupe story..kwanza my wife wako mzima? na my daughter wako? Juzi nilienda town toka kijiji cha Makongo village...nikaweka uwese kwenye gari pale shell ya BP Mwenge..halafu nikala kona barabara ya Ali hassan Mwinyi road kupitia daraja la Salender bridge...nikaibukia Hoteli ya Sheraton Hotel...hapo nilifika kuonana na Mshikaji wangu anayesoma chuo kikuu cha Mlimani university.....Anyway nitakumalizia baadae yaliyotokea hapo.

    ReplyDelete
  27. Mr. Bug EyezSeptember 05, 2010

    huyu Ruger atakuwa ni mwana mieleka na kwa bahati mbaya saaana kaangukiwa ktk pua.haha take it easy mdau.tumezoea lugha hiyo longer enough.thanks for your mizandastandingi.

    ReplyDelete
  28. Ni kama anavyosema Happy BIRTHDAY ya kuzaliwa kwa ankal...si unaona inajirudia pia...Michu Hongera kwa kupachika MY HUSBAND mume wake...au MY WIFE mke wake n.k...huwa nafurahia kusoma upuuzi wako SANA

    ReplyDelete
  29. Ndio nyie mnaolalamika mnaposikia wageni wanaenda kusoma Kiswahili Kenya.

    ReplyDelete
  30. hao wanaosema kenya wanaongea kiswahili fasaha waende kwenye blog nyingine kuwadanganya lakini sio hii. wakenya kibao tunafanya nao kazi na kiswahili ni hali jojo..yaani wanapiga kiswanglish kwa kwenda mbele.au wengine wanaongea na kilugha kabisa manake kiswahili hakipandi.sasa sijui hiyo kenya ni kenya ipi..tusipende kuwakweza majirani zetu kwenye kila kitu..

    ReplyDelete
  31. We nawe kwani umesikia hii ni globu ya kujifunzia lugha? Si hao wageni wakajifunze kwenye globu za lugha, nyinyi ndio mshipa wa utani umewakatika kila kitu serious, relax kama 7juu au seven up! Yoo man relax!

    Hao wageni wenu wanaenda kuandika majarida au wanataka kujifunza lugha ya kuwasiliana na watu? Hicho kiswahili cha TUKI na BAKITA wataongea na nani mtaani!

    Mtajibeba mwaka huu! Raaaa!

    ReplyDelete
  32. Heri mimi sijasema.

    ReplyDelete
  33. Michuzi naona siku hizi unakosea majina ya miji bana. Mbona mji kuu wa Japan zamani ulikuwa Tukuyu leo unakua Tokyo tena.

    Hata miji/ nchi mingine naona taratibu unaanza kuyapa majina tusiyazoe. Naomba turudishie utamaduni wa kutumia majina yale ya zamani, mfano;

    UK = Ukerewe
    Dubai = Dumila

    ReplyDelete
  34. pamoja na kuwa hivi ni vionjo, uandishi huwa ni mbovu. hata habari nyingine za kiswahili huwa lugha inakosewa sana, si utundu. wacha watu wakajifunze lugha ya taifa kwa mjomba kamau

    ReplyDelete
  35. kabang` yale yale ya shalobalo .....

    ReplyDelete
  36. mdau hoja yako nimeilewa sana na vizuri michuzi angerekebisha kwani siku hizi tuna watoto wadogo sana wanatumia computer na wao wanakuja kusoma na hii inaweza kuwapotosha.wadau wanao kupinga wao wana fikra ndogo ndio maana wanashindwa kuelewa je watoto wadogo wanaotembelea ambao ndio kwanza wanaanza kujifunza wataweza kutofautisha hizi lugha gongana? au globu ya jamii ni ya wakubwa tu?

    ReplyDelete
  37. ebu msituchoshe...nunua soma kwa hatua fundisha wanao kusoma na kuandika kiswahili fasaha...mnataka mteremko eeh ankali awafundishie watoto wenu kiswahili?? warudishe bongo wakasome saint government ya mferejini watajua kiswahili...raaaaaaaaah

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...