Hi Bro Michuzi.
Hii ni siku nilipotembelea kwa Baba wa Taifa Mwl.Nyerere. Napenda sana kutoa shukrani zangu nyingi sana kwa mtoto wa Baba wa Taifa letu, Madaraka Nyerere kwa ukarimu mwingi sana kwa kutukaribisha vuzuri sana na kutupatia huduma nzuri sana, pia kutupatia historia mbalimbali ya Mwalimu.
Kwa kweli tulipokelewa vizuri sana tena sana, tulifurahi sana sanaaa... namshukuru sana Madaraka. Hata wenzangu niliokuwa nao wamesifia sana ukarimu tulio upata. Wadau nawasihi mpatapo nafasi tembeleeni kumwenzi Baba yetu wa Taifa letu.
Asante sana Mr.Madaraka kwa ukarimu wako.
Salamu sana kwa wadau wote!
Chibiriti,
Cesena, Italy
Chibiriti akiweka shada la maua kwenye kaburi la Mwalimu
Chibiriti na wadau wakiwa na Madaraka kwenye kaburi la mwalimu
Chibiriti akiweka sahihi kitabu cha wageni




Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. KWANI HUYU JAMAA CHIBIRITI NI NANI HAPA TANZANIA AU ANA ISSUE MAANA HUWA HAISHI HUMU KILA SIKU KIBERTI NANI

    ReplyDelete
  2. ..kaka misupu, salaam aleykum,
    hivi huyu chibiriti ni nani? maana huwa nasoma tu habari zake hapa ktk blog yako, na sijamsikia muda kidogo..i wish to see him and ask him questions..
    cheers

    ReplyDelete
  3. Chibiriti, Ingekuwa vizuri sana ung'evisit na bibi ajuza wa huko mnapo beba maboxiiiii
    Rafiki yako wa Naching'wea

    ReplyDelete
  4. chibiriti ndani ya fulanaz tunaomba ufanye mpango umtumie ankal hiyo fulanaz, manake yakwake imepaka sana

    ReplyDelete
  5. chibiriti kama hujaoa tafadhli sana nakuhitaji uwe wangu, nikuite my husband wangu na we uniite my waifu wangu, ukinijibu natukutumia contact zangu fasta, yaelekea utakuwa ni mume mwema sana, michuzi hakuna kubana wala nini hapana jelaz hii ni spesheli kwa chibirirti tu!

    ReplyDelete
  6. J.K. Nyerere hakuwa perfect kama sisi. Alikuwa na mapungufu yake, lakini hatatokea kiongozi mwingine kama huyu. J.K Nyerere alikuwa genius. Ni wapi unaweza kwenda na kujichanganya na watu wote bila kujali rangi, dini au kabila zaidi ya Tanzania? Hata majirani wetu wana admit kwa hilo. Alitufanya wote tujione wa Tanzania bila kujali rangi, kabila, au dini.

    ReplyDelete
  7. Hapa kaka Chibi umetuwakilisha tusioweza kufika huko. Asante sana Genius Chibiliti kwa uwezo wako wa kuona mbali

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...