Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya Korosho Tanzania,Hemed Mkali (katikati) akitangaza ufunguzi wa ununuzi wa korosho hapa nchini kwa msimu wa 2010/2011. Wengine ni Mkurugenzi wa Huduma za Masoko wa Bodi hiyo Mohamed Hassan Hanga (kushoto) na Meneja Tawi wa Bodi Tawi la Dar es salaam Martin Malifedha.Picha na Tiganya Vincent.


NA ZAHRA MAJID- MAELEZO.

MSIMU wa ununuzi wa korosho kwa mwaka 2010/2011 nchini unatarajiwa kuanza Jumatano ya wiki ijayo.

Ununuzi huo unatarajia kutumia Mfumo wa Stakabadhi ghalani ambapo Vyama vya Ushirika vitapeleka korosho kwenye maghala ya Serikali ambapo ndipo mnada utafanyika.

Hayo yamesemwa leo jijini Dar es salaam na Makamu Mwenyekiti wa Bodi hiyo Hemedi Mkali wakati wa mkutano na waandishi wa habari katika ukumbi wa Idara ya Habari ( MAELEZO).

Amesema kuwa korosho zitauzwa kwa mnada utakaofanyika katika Bodi ya Korosho na katika Ofisi za Bodi katika mikoani ya Tanga, Mtwara, Pwani, Dar es salaam, Morogoro, Ruvuma na Wilaya za Kyela na Ludewa Tunduru.

Mkali alisema kuwa korosho zitakazouzwa ni zile tu zitakazokuwa kwenye magulio yaliyosajiliwa na Serikali na kuongeza uuzaji wa korosho kinyume cha utaratibu huo , wahusika watachukuliwa hatua kwa mujibu wa Sheria namba 12 ya mwaka 2009.

“ Wanunuzi wa korosho wanaombwa wafuate taratibu hizi za ununuzi kwani watakaojaribu kukiuka taratibu hizi za ununuzi basi wajue Sheria hii inayohusu sekta ya korosho itachukua mkondo wake” Mkali alisema.

Mkali alizitaja kuwa timu zitakazoendesha mnada huo kuwa na wawakilishi toka Bodi ya Korosho,Vyama vya Ushirika Benki ya CRDB na NMB, Bodi ya Leseni za maghala Tanzania, Maafisa Ushirika watakaoteuliwa kama waalikwa na wengine wanaohitaji kushuhudia watafuata utaratibu maalum wa minada hiyo.

Halikadhalika, alisema kuwa,katika mfumo wa stakabadhi za mazao maghalani, kwa niaba ya wakulima korosho zitakusanywa na chama cha ushirika cha msingi katika magulio yaliyosajiliwa kwa kuwalipa wakulima asilimia 70 ya bei dira kwa korosho daraja la kwanza.

Mkali alisema kuwa watalipwa malipo ya pili asilimia 30 baada ya korosho kuuzwa mnadani.

“Aidha watalipwa malipo ya tatu (ya majaliwa) kutokana na bei itakayopatikana kwenye mauzo mnadani” Aliongeza Mkali.

Mkali alitaja viwango vya bei za korosho kuwa ni Tshs. 800 kwa kilo moja kwa daraja la kwanza(STD) na Tshs. 640 kwa kilo moja kwa daraja la pili(UG).

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. matunda ya kilimo kwanza hayo, mimi huku nanunua korosho gm 100 kwa $1. wkt wakulima huko tz wanauza 0.5$ (nusu dola)per kg..

    simwonei mtu huruma kwa kuwa kila mtu anatumia demokrasia yake kupiga kura

    ReplyDelete
  2. Mimi nadhani irudishwe ule utaratibu wa mwanzo wa Biashara huria kati ya mkulima na mfanya biashara!! Hii itawasaidia sana wakulima wetu kwani bei zitakuwa zinapanda nakushuka kuliko hao crdb na hayo mashirika mengine yaliotajwa.
    Itamsaidia sana mkulima wa korosho katika kujikwamua Kiuchumi, ukizingatia kwa pale kusini ndio zao kubwa wanalolitegemea,and also itaweza kusaidi kukua kwa soko la zao hili!!!!!!

    Mdau usa

    ReplyDelete
  3. Acheni kuponda kila kitu, vitu vingine kama hamjui fungeni midomo yenu na zuieni mikono yenu kutype?

    Hivi mnajua adha iliyokuwa ikiwapata wakulima wa korosho kutoka kwa wanunuzi binafsi? Na bei waliyokuwa wakinunua hizo korosho mnazijua?

    Acheni kabisa kuleta UJUVI wenu kwenye masuala yanayohusu livelihoods za watu, mnataka turudi kule ambako walanguzi walikuwa wanapanga bei ndogo kisa eti soko huria?

    Na wewe huko juu korosho unayonunua gram 100 inakuwa imebanguliwa au hajabanguliwa? Mimi nahisi wewe unafikiri hizo koroshounazokula zatoka hivyo hivyo kwenye miti.

    ReplyDelete
  4. Uingereza, pakiti ya korosho zilizo tayari kuliwa na mlaji madukani 500gms(nusu kilo) ni Paundi Sterling 5 sawa na Tshs 10,000 kwa nusu kilo(500gms).

    Ipo haja ya kufufua viwanda vya ndani ya Tanzania vya kubangulia na kusindika Korosho ilia angalau Tshs 15,000 ya kilo moja ibaki Tanzania huku mkulima akiondoka angalau na Tshs. 8,000/= kwa kilo moja ya korosho.

    Mdau
    KilimoKwanza.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...