Msimamizi wa Ujenzi wa meadi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Singida, Deodatusi Mushumbuzi, kutoka Chuo Kikuu cha Ardhi, (kulia) akimtembeza Mgombea Mwenza wa urais,Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipofika kukagua maendeleo ya ujenzi wa Hospitali hiyo inayojengwa eneo la Kata ya Mandewa Wilaya ya Singidat. Kushoto ni Mkuu wa Wilaya ya Singida, Pascal Mabiti.
Mbunge wa Viti Maalum wa Mkoa wa Singida, Martha Mlata, akicheza pamoja na wananchi wa kijiji cha Puma ngoma ya asili ya kabila la Wanyaturu, wakati mgombea Mwenza wa urais,Dk. Mohamed Garib Bilal, alipofika kijijini hapo kufanya mkutano wa kampeni na kumnadi mgombea Ubunge wa Jimbo la Singida Magharibi, Hamis Misanga.

Nashindwa kuelewa hawa wanatembelea na kufungua hivi vitu wakati wa kapeni ..Hii ni conflict of interest hao wagombea wengine wao watafungua nini? hivi naamini havijajengwa na CCM ...
ReplyDeleteNa utupe hii lakini ujumbe utakufikia kumbuka dunia ni mapito...