Mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM,Dk. Mohamed Gharib Bilal, akimnadi mgombea ubunge wa Jimbo la Singida Mashariki, Jonathan Njau baada ya kusimama katika Kijiji cha Dung’unyi na kusalimia wananchi wakati akiwa njiani kuelekea katika uwanja wa mkutano wa kampeni Makiungu Mjini Mkoani Singida leo.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM, Nape Nnauya, akipiga gitaa la besi katika Jukwaa la bendi ya Vijana Jazz, wakati bendi hiyo ilipokuwa ikitoa burudani katika mkutano wa kampeni wa mgombea Mwenza wa urais wa CCM,Dk. Mohamed Gharib Bilal, uliofanyika kwenye Uwanja wa Makiungu mjini leo.
Mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM,Dk. Mohamed Gharib Bilal, akizungumza na Bi Mariam Lazaro (90) mkazi wa Kijiji cha Dung’unyi, kumuombea Kura mgombea Udiwani wa Kata mpya ya Dung’unyi, Bwana Bruno, (kushoto) wakati msafara huo ukipita katika kijiji hicho kuelekea Makiungu Wilaya ya Ikungi Mkoani Singida leo katika mkutano wa kampeni.Picha na Muhidin Sufiani.

Brother mbona hatuoni na kampeni ya vyama vingine?
ReplyDeletehabari kaka michuzi.Tumeshatuma maoni watu kibao ili wasome mawazo yetu cha ajabu umetubania kabisa sijui kwanini na sisi ndio wadau wa tuvuti hii au mwezetu umeelemea upande mmoja kuwa fear.ni mimi mdau wa michuzi Blog
ReplyDeleteTehe teh tee!
ReplyDeleteNaona upele sasa umepata MKUNAJI.
M-bangubangu/tindiga kazana mwanangu.