Mkurungenzi wa kampuni ya Pili Pili Entertainment (katikati) Sameer Srivastava akimpongeza nyota mmojawapo wa filamu mpya iliozinduliwa usiku wa leo iitwayo Black Sunday,ndani ukumbi wa cinema wa Mlimani City,Steven Kanumba kwa kuonyesha umahiri wake mkubwa wa kuigiza ndani ya filamu hiyo iliokuwa na msisimko mkubwa kwa watazamaji. Mbali ya Kanumba pia kulikuwepo na nyota wengine walioinogesha filamu hiyo vyema kama vile Aunt Ezekiel,Monalisa,Yusuph Mlela na wengineo.Uzinduzi wa filamu hiyo uliandaliwa na kampuni ya Pili Pili Entertainment na kuhudhuriwa na wageni waalikwa mbalimbali.
Nyota wa filamu ya Black Sunday iliozinduliwa usiku wa leo,Steven Kanumba akibadilishana mawazo na baadhi ya wageni waalikwa waliofika kwenye uzinduzi wa filamu hiyo iliokuwa na waigizaji wenye vipaji kibao, mara baada ya kutoka kuitazama.
Wageni waalikwa wakiingia kwenye ukumbi kuishuhudia filamu hiyo usiku huu.Kwa picha mbalimbali za tukio hili ingia hapa

Lakini kwenye sifa lazima tutoe... steven kanumba anaigiza vizuri wengine wangeiga mfano kwake manake saa zingine unasikia wazi kabisa kuwa mtu anasoma lakini steven anaweka "uhai" kwenye sinema zetu
ReplyDeletehivi jamani steven kanumba kaoa??? au bado ni mwindaji tu?? mimi ni daktari ningependa kukutana nae kama ni yu singo
ReplyDeletesteven kanumba naomba sana ufanye mchezo na dachi, kalunde na mlacha majina yao siyajui ila ni waliigiza sinema ya fair decision, kwa kweli wamenifurahisha na mwingine mtu mzima mhaya simjui jina anafanya sauti yake inakuwa mbaya sana kama ana chura kooni ila ni mwigizani fresh sana
ReplyDeleteDah,kijana hongera sana kwa kazi nzuri. Mi mpenzi sana wa filamu (hollywood,bollywood,nollywood etc na pia kwa saaaaaana, The Bongo Movies. Namkubali sana mzee mzima Kanumba, si kwa kuigiza tu, ila pia kubadilisha sekta ya filamu bongo na kuwa kibiashara zaidi. Enterpreneurship!Nimeipenda hii
ReplyDeleteA millionaire in making
Perth,Australia
kanumba bwana, sasa hapo sijui ndo atakuwa anasemaje!?
ReplyDeletelion children, lol.
hee hee.. nikikumbuka nacheka kweli!?
= = =
Buffalo,
New York
mdau wa buffalo we kiboko imebidi nicheke tuu, watu hamsahau ha ha haaa, im closing!!
ReplyDelete