ANKAL AKIWA NA MDAU NDESANJO MACHA ALIYEMWINGIZA KWENYE LIBENEKE HUKU HELSINKI, FINLAND, SEPTEMBER 5 2005 AMBAPO ANKAL ANAMSHUKURU SANA NDESANJO KWA KUMLETA KATIKA ULIMWENGU HUU WA MAWASILIANO KWA MTANDAO. BAHATI MBAYA AMA NZURI SHEREHE RASMI ZA MIAKA MITANO YA GLOBU YA JAMII IMEAHIRISHWA KWA SABABU ZILIZO NJE YA UWEZO WETU, ILA ZIMEPANGWA KUFANYIKA MARA BAADA YA UCHAGUZI AMBAPO KUTAKUWA PIA NA UZINDUZI RASMI WA www.michuzipost.com
NA MAMBO YATAKUWA MSWANO ZAIDI
UKITAKA KUONA POST HII AMBAYO NI YA KWANZA SIKU HIYO YA SIKU

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Hongera mno Kaka Michuzi, Mungu na azidi kuwa nawe unatuhabarisha mengi kwa kweli. Asante sana.

    ReplyDelete
  2. Hongereni sana wakurugenzi wa Globu ya Jamii kwa kutimiza miaka 5 ya maendeleo,tunazidi kuiombea globu ya jamii mafanikio mema na maisha marefu,Pia tunakupongeza Ankal kwa uvumilivu uliokuwa nao mda wote huu,kwa kuyavumilia mawimbi na ngurumo kali za wadau wa globu,tupo pamoja nawe ...kwani ukubwa jalala,utupiwa mema na mabaya ...
    Hongera sana,tuhongere sote..
    wadau
    FFU wa ughaibuni

    ReplyDelete
  3. Asalaam alaykhum ankal, Pole na swaumu! Hongera sana kwa kazi nzuri nasi tunafata nyayo za juhudi zako katika kupasha habari jamii duniani kote. Insahaalah mola akujaalie maisha marefu na yenye furaha kila mmoja nafurahia na kufaidika san na huduma yako. "Blog ya jamii idumu daima" Amiin!

    Wasalaam

    Chef Issa

    ReplyDelete
  4. E bwana ee, siku hazigandi. Hongera sana Bro Michuzi kwa kazi njema kwa jamii. Ni miaka mitano ya mafanikio. Tunataraji miaka ishirini na tano ijayo ya MAPINDUZI makubwa.
    Maggid
    Iringa

    ReplyDelete
  5. Sababu zilizo nje ya uwezo wako? Ankal....tafadhali chukua chako mapema!!!

    ReplyDelete
  6. Hongera sana kwa kutimiza miaka mitano ya kublogu, nakutakia heri na mafanikio katika miaka mingi ijayo.

    ReplyDelete
  7. michuki nakupongeza sana na glob for five year anniversary. Ila uwe makini sana ukuaji wa glob ya jamii naona umetwkwa na siasa na ndiyo hapo "professionalism" inakufa. Mimi naikubali sana hii glob kwa kufanikisha upashaji habari, kuelimisha na kuburudisha..ila imeshindwa kumaintain neutrality na profssionalism hasa kwenye siasa. Ninajua kuwa kuna habari kibao ukipewa badala ya kuzirusha hewani unawauliza wahusika eti"jamani kuna hii mpya nimeletewa niirushe au vupi" tena nyuzi ya kawaida tu ila kwa kuwa inahusu mrengo fulani inakuwa soo. Blog hii inakazi zaidi ya unayofikiria.Hii blog inatumika pia kama "watch dog" kwa wenye madaraka na waliopewa dhamana. kwa hiyo ni zaidi ya unavyofikiria. Ni vyema ukadumisha "professionalism" na haki kwa wote ili blog hii ya jamii iendelee kutoa mchango zaidi katika maendeleo ya nchi badala ya kuonekana ni chombo cha propaganda cha watu fulani...
    Ni maoni yangu najua unaweza yarusha au kuyaweka kapuni as usual..ila Naikubali

    ReplyDelete
  8. Sidhani kama huyu jamaa wakati mnaanzisha blogu hii alikushauri uweke habari za kukandia vyama vyovyote isipokua CCM... na kwamba unapopewa habari nzuri za hivyo vyama vingine usiziweke (kama ile ya majibu ya mchumba wa Dr Slaa kupitia kwa mwanasheria wa Chadema niliokutumia na hukuiweka). Unachuja na kuweka habari za CCM na kuweka kashfa za uongo za vyama vingine. Ukiletewa majibu ya hizo kasfha wewe unakua huziweki. Acha kuwadandia waliomo madarakani kwani siku zao zahesabika. Sijui utajificha wapi wakishindwa.

    ReplyDelete
  9. Tukiacha hisia za kibinadamu ambazo kila mmoja wetu anazo, pamoja na mitizamo yake, blogu hii pamoja na mmiliki wake wamekuwa mfano mzuri wa kuigwa kwa vijana wengine. Jina la MICHUZI lina historia kubwa katika tasnia ya habari na itabaki kuwa hivyo. HONGERA SANA MKUU

    ReplyDelete
  10. Mgombea Mwenza wa CUF Juma Duni Haji alilieleza gazeti hili kwamba Watanzania waelewe kuwa hata wakiipa CCM miaka mingine 100 ya kutawala hawataweza kuwa na maisha bora.
    “Kuna silaha mbili zinazotumiwa na CCM kushinda. Kwanza, masikini na mtu mjinga ndiye anayetawalika. Pili, tajiri hawezi kutawalika. Kwa hiyo wanatambua hizi silaa na wanahakikisha watu wanabaki kuwa masikini na wajinga ili waendelee kutawala.
    “Tumefika kwenye shule moja tumekuta ina wanafunzi 900 lakini walimu wanne, kwenye shule nyingine mwalimu mmoja huyo huyo amejiita Mwalimu Mkuu, ukimuuliza kwa nini ajipe cheo hicho anacheka tu,” alisema Duni.
    Athari kubwa ambayo inatukabili ni matumizi makubwa ya fedha kwa upande wa CCM, tupo njiani kuelekea Bukoba Vijijini ni dhahiri fedha nyingi zimetumika na hii ni njia mojawapo ya kukandamiza demokrasia,”
    Alipoulizwa kwamba matumizi ya fedha hizo inawezekana ikawa kwa mujibu wa Sheria ya Gharama za Uchaguzi inayotaja kiwango hadi Sh bilioni 50, Maharagande alisema kwa vyovyote vile na hasa kwa kuzingatia mazingira ya Tanzania, demokrasia inaathirika.
    “Wamesambaza mabango kila kona, fulana zitagawiwa karibu kwa kila Mtanzania…najiuliza inakuwaje mabilioni yamwagwe kiasi hicho wakati huduma za jamii kule wanakoenda kuomba kura zikiwa zimezorota. Dawa hospitalini hakuna hata karatasi za kuandika taarifa za wagonjwa lakini karatasi za kampeni zimesambazwa hadi vyooni,” alisema Maharagande na kuongeza kuwa wana matarajio makubwa kwamba Profesa Ibrahim Lipumba mgombea urais kwa tiketi ya CUF atashinda na kuunda serikali licha ya matumizi hayo makubwa ya fedha kwa upande wa CCM

    ReplyDelete
  11. Hongera Ankala kwa kutimiza miaka 5 ya globu hii ya jamii imekuwa ikitufikishia habari mapema mno. Hatuna budi kuipongeza

    GLOBU HOYEEEEEEEEEEEEE!!!!!!!!!!!!!!.

    ReplyDelete
  12. Hongera mkubwa! najua umeanzia mbali
    Ahsante kwa kutuhabarisha.
    Lakini Ankal usiegemee sana upande mmoja...........
    Na wala usiwe unatubania tunapoweka comments zetu zinazopingana na mtazamo wenu.....

    Billy

    ReplyDelete
  13. uwege pia unasikiliza ushauri wa wanaglobu basi. hasa mambo ya kukurupuka kuandika habari na kuipublish kabla ya kuhakiki ubora na kubana comment zenye kujenga

    ReplyDelete
  14. EBANAEE! KAMA VIPI KWENDA ZAKO, SIKU ZA HIVI KARIBUNI KUFUATIA MASWALA YA KAMPENI UMEKUWA UNANICHEFUA FULANI, KUTOKANA NA BAYAZNES YAKO KATIKA HABARI ZA VYAMA VYA SIASA UMEKUWA UNAKIPENDELEA SANA CHAMA CHA MAPITUNDUZI KWA SABABU YA UKEREKETWA WAKO. SIPONGEZI WALA NINI

    ReplyDelete
  15. Muhidin mbona unabania maoni yangu? Nakuuliza, kama Dr. Slaa anatakiwa kufikishwa kizimbani kwa kuiba mke, lini Msekwa atafikishwa pia kwa kumuiba Ana Abdala toka kwa mumewe halali? Tena ni lini Makamba atafikishwa mahakamani kwa kubaka mwanafunzi akiwa mwalimu kule Kasulu? Na ni lini JK atafikishwa kizimbani kwa kuingilia wanawajke wa UWT kila wilaya Tanzania? Umeweka ugali mimi natupa mboga.

    ReplyDelete
  16. Hongera sana Ankal Michuzi, katika kipindi hicho ambacho kinaonekana kama ni kifupi, lakini ni zaidi ya jumla ya siku 1,825 umekuwa active na blog yako iko current kila wakati! Si mchezo!!!! Ama hakika unastahili pongezi nyingi, na ankal tambua kwamba wewe umekuwa faraja kubwa sana hasa kwa watanzania wanaoishi nje ya nchi. Mimi nime experience hilo na nakuhakikishia ukiwa far from home at least twice a day utaingia kwenye blog ya michuzi kuangalia "Nini khabari huko home" (I used to. na hapa home, ukiingia maofisini asubuhi, kila mtu yuko kwenye Michuzi blog, yani uko juu kuliko formal doe coms za newsrooms za hapa bongo. Keep it up ANKAL na happy 5th Anniversary!!!RAM

    ReplyDelete
  17. Hongereni!Ila ushauri wa bure mnakoelekea si kuzuri kuwa washabiki wa kisiasa, mtatupoteza wengi. Hata ukiibania comment yangu ila msg delivered!

    ReplyDelete
  18. Michuzi, hii ni blog tu, huku Marekani hata watoto wa darasa la tano sasa wana blog zao, kwa nini ni issue kubwa kwako kuwa na blog sasa? Ningekuelewa kama tupo 1990, lakini sasa ni 2010.

    Hongera kwa vyovyote na wasalimie wanasiasa wako wa CCM.

    Maraha ni pesa
    USA

    ReplyDelete
  19. Hongera Michuzi.Ndesanjo huko wapi?
    Mdau Toledo.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...