

Most read Swahili blog on earth
Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.
hizi picha tatu za mwisho (chini) zinashangaza sana. inaonyesha CHADEMA are not serious. hivi hapo si wanashabikia CCM?
ReplyDeleteIna maana huwezi piga picha Angle tofauti hadi utoe matanagazo ya CCM. Ama kweli ukishakunywa maji ya bendera unakuwa KADA milele
ReplyDeleteChadema choka mbayaaa, kweupeee watu washa wastukia na siasa zenu za kutugawa kwa misingi ya dini na kabila
ReplyDeletemichuzi!
ReplyDeleteThat background! as if ni kampeni inayofanyika kwa niaba ya CCM????
Hivi haya magwanda ya chadema wanayatoa wapi? Kila mtu akihamia chama hicho anayo.
ReplyDeleteyaani engo ya izi picha kweli, hii kali ya mwaka.
ReplyDeleteCCM kweli wamefunika bovu. Sasa hapo itakuwa nguvu kumsikiliza huyo bwana na huo ujumbe mkubwa hapo nyuma?
anyway.
nikikumbuka nacheka, nikisahau nalia!?
= = =
Buffalo,
New York
Bwana Michuzi hizi picha za kampaini za CHADEMA aliyetuma alikuwa na makusudi chafu. Hawezi kupiga mgombea uku badala ya kupiga watu waliohdhuria anapiga mabago ya CCM na ujumbe wake. Katika fani ya upigaji picha kama mwandishi wa picha uliyebobea, aliyekutumia amepotosha, na kama umemtuma wewe basi nia yenu haikuwa nzuri
ReplyDeleteAnkal sijakuelewa kidogo hapo, ulikuwa unaonesha campaign za chadema au mabango ya campaign ya CCM? usanii uliotumia ni wa hali ya juu. najua utatuambia angle nyingine ulishindwa kupiga picha sababu ya jua. usanii uliotumia hapo ni wa hali ya juu. poa mkuu wenye akili tumeelewa.
ReplyDeleteKaazi kwelikweli!
ReplyDeleteHee kampeni mbona haina wasikilizaji. Baiskeli ndiyo nyingi kuliko watu. Hawa hiki chama cha demorasia cha moshi na arusha vipi?
ReplyDeleteChadema mmefulia mahudhurio hafifu hayo kweupeeeeeee!!!!!!
ReplyDeleteHapa chadema wamepatikana pembeni chagua CCM, HAIFUTIKI HIYO
ReplyDeleteMpiga picha mbona ame-concentrate na bango la CCM badala ya kile alichokuwa anawakilisha (mkutano wa Chadema)?
ReplyDeleteAnkal.....vp hizi picha tatu za mwisho wameleta au umepiga wewe! tehe....tehe........tihiii!
ReplyDeleteStrategy mbovu kabisa hii... Hii ni sawa na kuuza jezi za Man Utd nje ya Stanford Bridge... Unaleta ushindani lakini bado unakwenda kuhutubia mbele ya bango kubwa la mpinzani kuliko vipeperushi vyako. Kwa mtaji huu CCM itakuwa juu for at least another 20 years from now
ReplyDeleteHii Picha safi sana. Maana kwa muda mrefu sasa Wajasirilia mali waneelewa kuwa CCM imewatosa kwa sana; Hivyo ni vyema kuona mbadala wa bango hili kwa kuchagua CHADEMA: Hii ndiyo logic ya huyu kufanya kampeini mbele ya Ubao huu
ReplyDeleteSASA HAO WANYACHUSA MWALUSAKO NA MWAIPAJA MBEYA KWAO KIMEWAKIMBIZA NINI MPAKA WOTE WAKAJAZANE HUKO MOROGORO KUWABANA WARUGURU WASIPATE NAFASI ZA KUUWAKILISHA MKOA WAO,AU NDIO NAO WAMEMKIMBIA MR 2 SUGU ALIEKACHA KWAO SONGEA NA KUVAMIA MBEYA
ReplyDeleteHii kali, kampeni za chadema bango kubwa la CCM likinadi CCM, kama ni mtiani na mpiga picha umetumwa kuinadi CHADEMA unafukuzwa kazi maana hata kama kampeni zilifanyika jirani na bango la CCM ulitakiwa utafute location nzuri ambayo bango halitaonekana.
ReplyDeleteInapendeza kweli.. CHADEMA wanafanya kampeni huku katika background kuna bango la CCM!
ReplyDeletetumeliona bango la chama michuzi
ReplyDeleteankal ina maana gani kulipiga picha hilo bango la ccm maana ungetaka ingewezekana kutoa picha ya hao chadema bila kuingiza hilo bango la sisiemu
ReplyDeleteMabango yenye ujumbe, rangi, nk yanaingia ndani ya akili zetu!
ReplyDeleteHilo bango la CCM kaliweka nani?
Kama ni Chadema, basi linakejeli CCM.
Kama ni CCM basi hiyo set isingetumiwa na Chadema; inaonekana kuwa Chadema inakisaidia CCM!
Naona michuzi mwaka huu umeamua kwa dhati kabisa kutuzihirishia kuwa wewe Ni CCM damu....
ReplyDeleteNdio nini kuchakachua hadi picha ? kuli kuwa na ulazima wa kupiga hizi picha kwa style hii?
Najua team yako ndio iliyopiga hizi picha na kukutumia hila hazifahi kuwekwa hapa maana zinaleta picha mbaya ambayo ukenguwa mtu makini usinge ziweka hizi picha tatu za mwisho...
Huu ni uhuni kabisa......
Nadhani utachakachua na hii comment.
Michuzi. Hakuna ulazima wakuweka picha za Chadema humu kwenye hii blog ya CCM, hizi picha siyo za kampeni za chadema bali ni za CCM maana ujumbe unaosomeka hapo ni "changua CCM'
ReplyDeleteAnkal imefika wakati sasa ukae chini na kufikiria vitu unavyo bandika humu ndani, usijepata lawama au ukajikuta kwenye wakati mbaya, maana chichiem haita tawala milele...
Uchauri wangu: ili kuepuka hizi lawama naona uweke kando maswala ya siasa, au usipo weka mabango ya Chichiem utafukuzwa kazi? Maana njaa inawafanya mfanye vitu ambavyo havikubaliki kwa jamii..
Haya ankal sijui kama msg italiona jua!
Hivi hamjui kirefu cha CCM ni Chama cha Michuzi(mambo ya fweza).Huyu michuzi anafakiri bado tunampenda Kikwete.Yaani bora niharibu kura yangu kuliko kumpigia Kikwete.CHADEMA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE
ReplyDeleteNchi imeisha. Mpaka wapiga picha wamekuwa wahuni. Bania tuu hii comment lakini this is a not professional at all. Hakuna marefu yasiokuwa na nja.
ReplyDelete“…Nawasihi waandishi ambao mna ushabiki na vyama acheni kuvaa tisheti za CCM ama vyama vingine katika kipindi hiki, kwani mnakiuka maadili ya kazi yenu; mnapaswa kutoonyesha ushabiki wa vyama kwa kuwa wananchi wanawategemea kuwaelimisha,” alisema Tendwa.
ReplyDeleteHawa jamaa na magwanda yao ya mgambo naogopa wakichukua nchi, nchi itakuwa ya kidikteta tu
ReplyDeleteMichuzi wewe ni mtaalamu wa sanaa ya taswira. Mwanzoni ulikuwa unatoa habari za chama kimoja tu, wadau wakakupa maoni ukaanza kutoa na wengine. Umerudi kule kule.
ReplyDeleteKwenye suala la kuchakachua comments na kuzitosa zisizounga mkono chama kimojawapo au zenye kuuliza maswali magumu chama kimojawapo inavumilika lakini unapofanya kitu kama hiki kwa kweli ni dhambi kwa wadau wa globu. Ina maana globu imekuwa tawi la dailynews na habarileo?
Hapa wa kulaumiwa siyo Michuzi bali hawa walioamua kwenda kufanya kampeni karibu nabango linalomnadi mgombea wa CCM.Wanaonyesha ni kiasi hawako serious.Kazi ya mpigapicha ni kumpa kazi ya ziadi muangaliaji wa picha ile kuangalia DETAILS za picha na kuzichambua hii inaonyesha kiasi gani mtu aliyepiga picha hii anavyoijua kazi yake vizuri.NARUDIA TENA MUWALAUMU WALE WALIOAMUA KWENDA KUFANYA KAMPENI KARIBU YA BANGO LA MGOMBEA WA CCM
ReplyDeleteHivi hao mgambo hawakuona sehemu ingine ya kufanyia mkutano ila sehemu hiyo tu? wamechemka .ningekuwa mimi nagombea huyo kampeni meneja hana kazi kwa sababu ya kushindwa kunishauri vizuri,huwezi panga mkutano sehemu kama hiyo hata kama ilikuwa imepangwa kabla ccm hawajaweka bango basi ningeaharisha kufanya mkutano sehemu hiyo ilio nisionekane nawapigia kura wapinzani..
ReplyDelete