Mkurugenzi wa kituo cha Amani Orphanage Center Margareth Mwegalawa akipokea msaada wa vifaa vya kufundishia vyenye thamani ya milioni 2/- kutoka kwa Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa KCB Tanzania ,Christina Manyenye wakati wa hafla iliyofanyika kwenye kituo hicho kinachohudumia watoto yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu jijini Dasr es Salaam leo.
Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa KCB Tanzania, Christina Manyenye (kushoto) na Mkurugenzi wa kituo cha Amani Orphanage Center , Margareth Mwegalawa wakiwasaidia kufungua maboksi yenye vitabu vilivyotolewa na benki hiyo wakati wafanyakazi wa benki hiyo walipotembelea kituo hicho na kutoa msaada wenye thamani ya shilingi milioni2/- jijini Dar es Salaam jana
Baadhi ya wfanyakazi wa KCB Tanzania wakiwa wamewabeba watoto wa kituo cha yatima na wanaoishi kwenye mazingira magumu cha Amani Orphanage Center cha Boko wakati wa makabidhiano ya vifaa vya kufundishia vyenye thamani ya milioni 2/-kwenyer hafla iliyofanyika shuleni hapo jana jijini Dar es Salaam

Na Mwandishi Wetu

BENKI ya KCB Tanzania imeamua kubeba jukumu la kuwalea watoto 11 wa kituo cha watoto yatima cha Amani Orphanage Centre kwa kukikisaidia na kukihudumia kwa mahitaji ya vifaa muhimu vya shule kwa watoto hao kilichopo Boko jijini Dar es Salaam.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi msaada wa vifaa mbalimbali wenye thamani ya zaidi milioni 2/- kwa ajili ya takribani watoto 45 wa shule hiyo,Mkurugenzi wa Masoko na Mawasiliano wa benki hiyo Christina Manyenye alisema kwa kuanzia wametoa vifaa hivyo ili viwasaidie kwanza yatima.

Akifafanua alisema kutokana na kuguswa na watoto wa kituo hicho kilicho chini ya Shirika la Empowering Children and Community Organization kilichoanzishwa kusaidia watoto yatima na wale wanaoishi katika mazingira magumu wameona wakisaidie kutokana na kuona kwamba ndoto za watoto hao ni sawa na za wanaotoka katika familia zinazojimudu kimaisha.

“Hivyo basi hatuna budi kuwasaidia watoto hawa na tunaahidi kuendelea kuwasaidia ili kukipunguzia mzigo kituo cha Amani jukumu la kuwalea watoto kituo hiki cha Amani ikiwa ni pamoja na kuwawezesha kusoma. Ni wachache sana wanaoweza kufanya ubinadamu huu,” alisema Manyeye.

Hata hivyo aliongeza kwamba msaada huo umefuatia KCB Tanzania kutambua umuhimu wa jamii na kufahamu ukweli kuwa maendeleo ya jamii ni maendeleo ya taifa zima. Aidha alisema bila jamii yenye maendeleo uwepo wao kama benki utakuwa na mashaka.

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa kituo hicho Margareth Mwegalawa alisema kuwa licha kuhudumia watoto yatima 11 wanaoishi bweni, pia wanahudumia watoto wengine wanaoishi katika mazingira magumu kwa kuwapatia vifaa vya shule na mahitaji mengine.

Hata hivyo wanakabiliwa na uhaba wa vyumba vya kulala watoto, vitanda, uchakavu milango na madirisha ya jengo la kituo hicho jambo linalochangia kituo kuchukua watoto wachache wanaoendelea kuishi kwenye mazingira magumu.

Kutokana na hilo waliiomba KCB Tanzania na taasisi zingine kujitokeza kukisaidia kituo hicho kwa kukipa misaada mingine ikiwemo magodoro, vitanda, vifaa vya kusomea watoto, vyakula, madawati ya kukalia na vifaa vya kufundishia.

Nae Afisa Maendeleo ya Jamii kata ya Bunju, Syzgo Alexander aliiopongeza benki hiyo kwa kuwa na moyo huo wa kujitolea na kusema kutokana na mahali kilipo kituo imeonesha imejitoa kuihudumia jamii kwa hali na mali jambo alilotaka liiungwe mkon o na Watanzania.

KCB Tanzania ni benki kubwa Afrika Mashariki ikiwa na rasilimali nyingi ikiwemo matawi zaidi ya 200 na mashine zaidi ya 400 za kutolea fedha (ATM) zilizotawanywa kote Afrika Mashariki na mtandao unaofikia nchi za Rwanda na Sudan Kusini.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Watoto hawa wanahitaji matunda na maziwa ya ng'ombe au ya mbuzi na si soda ambazo zina madhara kwenye meno yao na hazisaidii kuijenga miili yao. Unapotoa misaada jaribuni pia kuangalia faida ya mnavyotoa kwa miili yao.

    ReplyDelete
  2. there is only one party campaign news, or other parties do not do campaigns? and we need to know what promises we are given not family matters of the candidate, in this way there is no any democracy what we need is changes not benefits of the few people who don't see the large number of Tanzanian who live below half dollar per day and not one dollar as we use to know.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...