KATIKA KUSHEHEREKEA SIKUKUU YA EID, TANZANIA READING ASSOCIATION ( T . A ) IKISHIRIKIANA NA TANZANIA READING FC INAWALETEA MPAMBANO WA SOKA KATI YA TANZANIA READING FC Vs TANZANIA MILTON KEYNES FC.

BAADA YA KUSUBIRIWA KWA MUDA MREFU NA WAPENZI WA SOKA WA NCHINI UK, MABINGWA WA SOKA NCHINI UINGEREZA TANZANIA READING FC ( REMCO ) HATIMAE WATAINGIA UWANJANI KULITETEA TAJI LAO DHIDI YA TEAM YA MILTON KEYNES KUTOKA MILTON HAPO JUMAMOSI YA TAREHE 11 SEPTEMBER 2010, KUANZIA SAA NANE MCHANA KATIKA KIWANJA CHA KENSINGTON PARK OFF OXFORD ROAD OPPOSITE TESCO READING.

BAADA YA KUKOSA UPINZANI KWA MUDA MREFU, "VIJANA WA TEAM HIYO YA READING WAKO TAYARI KUONYESHA NI KWANINI TEAM ZINGINE ZIMEKUA ZIKIWAOGOPA" ALISEMA KOCHA MCHEZAJI WA TEAM HIO HANIU.

NAE MENEJA WA TEAM YA MILTON ALISEMA VIJANA WAKE WANATAKA KUTHIBITISHA KUWA WAO NI MOTO WA KUOTEA MBALI ,WAKO TAYARI KUCHUKUA NAFASI HIYO YA UBINGWA UNAOSHIKILIWA NA TIMU YA READING TANZANIA FC .
WASHABIKI WA TEAM HIZO MBILI WANAUSUBIRI KWA HAMU KUBWA MPAMBANO HUO KWANI WANATAMBIANA .

WADHAMINI WA PAMBANO HILO, TANZANIA READING ASSOCIATION ( T . A ) KUPITIA KWA MJUMBE FRANCIA CHENGULA WATATOA ZAWADI KWA MSHINDI WA PAMBANO HILO ATAPEWA ZAWADI YA POUND £100, MCHEZAJI BORA ATAPEWA ZAWADI YA MPIRA WA MIGUU , NA MSHINDI WA PILI ATAPEWA ZAWADI YA MPIRA MMOJA.

MJUMBE WA T.A . FRANCIA CHENGULA ALISEMA MORE TO COME FROM TANZANIA READING ASSOCIATION NA TANZANIA READING FC KWANI TUNAANDAA MPAMBANO MWINGINE KATI YA TA READING FC NA TEAM YA READING POLICE; USIKOSE.

TA READING INAKARIBISHA MICHANGO ILI KUSAIDIA TEAM HII AU WAFANYA BIASHARA WANAOTAKA KUTANGAZA BIASHARA ZAO KUPITIA HII TEAM.

TAFADHALI WASILIANA NA MJUMBE FRANCIA 07970113058.
ASANTENT NA KARIBUNI WOTE.

BAADA YA MPIRA HUO BONGO DEEJAYS WAMEKUANDALIA BURUDANI YA KUSHEHEREKEA EID KATIKA UKUMBI WA THE FACE CLUB KUANZIA SAA NNE USIKU MPAKA SAA KUMI NA NUSU ASUBUHI WOTE MNAKARIBISHWA!!

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. Hizi ndio za watz badala ya kuja na strategy za maana za kusaidia watu waache kubeba box mnakuja na mambo ya shangwe tu. Mnasikitisha...Rudini nyumbani

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...