Hi Issa,
Naomba unisaidie kuhusu swala la hapo juu. Nimelipia gharama zote za kuunganisha umeme kwenye nyumba yangu 7/8/10. Mpaka jana 20/9/10 sijaunganishwa na huduma hiyo. Jana nilikwenda kuulizia kwa mara ya pili nikaambiwa kuwa shirika hilo limeishiwa waya. Nikitaka kujua kwa nini na lini tatizo hilo litamalizika, naambiwa kamwone engineer ambaye hapatikani ofisini kwake.
Cha kushangaza ni kuwa yule anaetoa majibu hayo haambiwi tatizo hilo litaisha lini. Lakini anaeleza kuwa maelezo yale anaelekezwa na engineer.
Tafadhali tusaidie.
mdau
Hamza
Naomba unisaidie kuhusu swala la hapo juu. Nimelipia gharama zote za kuunganisha umeme kwenye nyumba yangu 7/8/10. Mpaka jana 20/9/10 sijaunganishwa na huduma hiyo. Jana nilikwenda kuulizia kwa mara ya pili nikaambiwa kuwa shirika hilo limeishiwa waya. Nikitaka kujua kwa nini na lini tatizo hilo litamalizika, naambiwa kamwone engineer ambaye hapatikani ofisini kwake.
Cha kushangaza ni kuwa yule anaetoa majibu hayo haambiwi tatizo hilo litaisha lini. Lakini anaeleza kuwa maelezo yale anaelekezwa na engineer.
Tafadhali tusaidie.
mdau
Hamza
Hivi wewe una utoto gani mpaka usijue kinachoendelea? Nyaya zipo, wape! Wewe unategemea njia za kwenda chooni kwao ziote nyasi kwa ajili yako! Una umri gani? Siku nyingine nitakukana. Mimi Mzee wa Kunyorosha
ReplyDeletewameishiwa waya? hii nchi kweli inaendeshwa kimsaada msaada.
ReplyDeleteHamza acha matani bwana unaongelea tanesco ya tanzania au wapi? yaani umelipia mwezi mmoja unalalamika mimi nilikaaga niezi 4 kwa mbinde ndio wakaniunganisha hili shirika inatakiwa liletewe wapinzani ndio litaamka
ReplyDeleteWe wachekesha kweli, wenzio tumejaza fomu miaka 10 iliyopita na bado tunasubiri. Wewe hata mwezi bado walalamika!!!!!!!!
ReplyDeleteHiyo ndo Tanesco bwana, - Tafuta kishoka, wapo wengi ktk kila ofisi ya Tanesco halafu uone kazi itakavyokimbia
Observer
Vote for a change,otherwise utasota milele
ReplyDeleteMzee matatizo ya ukiritimba (monopoly) hayo.
ReplyDeleteNa wewe sio wa kwanza, wala hayajaanza leo.
Mie mwezi July 2004 kama wewe nililipia kila kitu TANESCO ya Keko. Wakati huo nakaa jirani na hiki chuo hivi sasa kinaitwa DUCE.
Nilikuwa bize kinoma kazini, kuondoka saa 1 asubuhi kurudi saa 1 usiku.
Wacha wanizungushe bwana, maana muda wangu wa kuwafuatilia ulikuwa mdogo sasa kale kasaa kamoja tu ka lanchi time (saa saba mpaka saa nane).
Walinizungusha for one year. ONE YEAR niko gizani mzee kwa usenge wa TANESCO.
Mpaka baadae nikaja kupata demu wa kukaa naye home. Alikuwa kifaa sana huyo demu. Basi nikamtuma TANESCO afatilie umeme. Mijamaa nakwambia walipomuona (kwa mujibu wa demu mwenyewe) miudenda wacha iwatoke.
Ndani ya siku tatu tu toka nimtume nikapata umeme.
Kwa hiyo kaza buti mzee, hao jamaa ni wasumbufu utazani umeme wanatoa bure.
Ndio maana naunga mkono kabisa watu wanaowaibia umeme.
Nakutakia kila la heri.
Kamshitaki huyo engineer kwa sheikh yahya- atakupa ulinzi wa nanii kisha kitaeleweka kwa engineer.
ReplyDeleteHivi wewe braza ni Mtz au wewe ni mgeni yani kamda hako tu umeshaanza kuimba kwa sauti uliza sisi tuna vimiaka!!
ReplyDeleteTanesco, shirika la umma, watu wamejaa vitambi kula pesa za watu na za shirika. Shame on you Tanesco. Nakuambia walipita arusha wanadai mamilioni ya pesa kwenye nyumba za watu, ukiambiwa ni milioni 10 unalipa milioni moja kwa Engineer,meneger tanesco na Mshasibu wake inasambazwa kwa kila mkuu unanaletewa umeme na unadaiwa milioni mbili tu kulipia. Wanakuja kukuchomolea wai kinyemela halafu wanarudi wanadai umeiba umeme. Kama humjui mtu tanesco ni kazi kazi kweli. Nakuambia tutapata umeme mzuri na huduma zenye heshima tu utakaposikia mzungu kaingia tanesco na siyo ailimia 100 shirika la umma. Nadhani wansubiri wale kidogo kwa nyumba na mahoteli hayajaisha baada ya hapo utasikia shirika linadaniwa. Kama kuna shida kwa nini hawabandiki matangazo kwenye ubao kuonyesha ni service gani hawana. Michuzi usibanie hii kwani nimechoka na wizi wa tanesco unless unawaunga mkono na wizi wao wa mchana Kam kuna uozo na ufujaji wa mali za umma tanesco wamekithiri. Naomba Mungu sijui ni mzungu gani atakuja kututawala kwenye hilo ili tupate service za uhakika. Na utaona shirika limegeuka kuwa la faida.
ReplyDeleteNaungana na jamaa wa demu hata mie rafiki yangu walijenga nyumba hapo kawe tu, umeme ikawa mbinde. Mamake kazungushwa wee kaona tabu ya nini bintiye bomba sana ana u shepu wa kufa mtu alienda tanesco na kesho yake walikuja na umeme ukawaka, yaani hawa tanesco wana mapepo!
ReplyDeleteNchi tunaiua kwa mikono yetu wenyewe......Sijui JK sura anaipitisha wapi kuomba urais! Ana bahati sana ujinga wa waTZ unasaidia sana wenye ujanja
ReplyDeleteTANESCO is the most bogus parastatal in the country! Hewa kabisa! Hamna kitu pale. Sijui PCCB wanafanya nini jamani!
ReplyDeleteHAMZA POLESANA KWA USUMBUFU ULIOPATA,SHIRIKA LA UMEME SASA NIMEJIAKITI SANA KATIKA KUBORESHA HUDUMA ZAKE KWA WATEJA,MFANO. TUMEANZISHA CALL CENTER HIVI KARIBUNI ITAANZA KUTUMIKA NA NUMBER ZA SIMU KUJULIKANA KWA UMA WOTE.
ReplyDeleteNAPENDA KUKUHIKIKISHIA KWAMBA FEEDBACK KAMA HIZO TUNATUMIA KUJIFUNZA NA KUBORESHA ZAIDI HUDUMA ZETU.
TATIZO HUJASEMA MAENEO YA NYUMBA YAKO,YAANI-LOCATION E.G TANESCO YA MKOA GANI,WILAYA GANI ETC ILI TUKUSAIDIE KUJUA NI ENGINEER GANI ONAYEONGELEWA HAPO.
KWASASA NAKUSHAURI NENDA KWENYE HIYO OFISI YA TANESCO OMBA KUONANA NA MENEJA MKOA AU REGIONAL CUSTOMER RELATION OFFICER UTASAIDIWA.
PAMOJA TUJENGE TANESCO YENYE UFANISI
POLENI SANA NDUGU ZANGU! SIFA YA KWANZA TANESCO NIKUWA WAZINZI LA PILI WALEVI NA YOTE HAYO NI KUTOKANA NA PESA ZA MISHEMISHE WANAZOPATA,HATA HAO MABOSI WAO WANAJUA MWANZO MWISHO NA WAO PIA WANAWATUMIA VIJANA WAO WA CHINI KUHUSU MISHEMISHE HIZO, WEWE CHEZA NA VISHOKA UMEME UTAPATA BILA MATATIZO. MIMI NILIWEKEWA UMEME KWA MUDA WA MWEZI MMOJA MAJIRANI ZANGU WALIKUWA NA MIAKA KIBAO HAWAJAPATA UMEME NA KULIPIA KILA KITU WALIKUWA WAMESHALIPA, SASA HAPO KAMA HUNA CHOCHOTE HUPATI KITU,MISHEMISHE IPO KWENYE VIFAA NA KUWAPATA MA ENGINEER, KAZI KWELI MKWELI-MUNGU SAIDIA TANZANIA.
ReplyDeleteWANATAKA "CHUMVI" HAO
ReplyDeleteHuyo ndugu wa sep 22, 09: 03 wewe acha bwana watu sasa hivi ninaongea hakuna offisi hata moja wameweka BANGO kusema usitowe rushwa wahasibu wenu wote na hao so called Engineer wa vituo ni wezi wakubwa, haswa Moshi, Arusha Mwanza na Dar kama unabisha piga kura za maoni mitaani utajuwa jinsi gani wananchi wanvyopata shida. Na kama unataka kujuwa counter part wenu Idara ya Maji moshi angalieni wanvyofanya kazi kwa kuwa proffetional at work. Wanfurahisha sana. Sasa Nenda Tanesco ni unahitaji pesa kumpeleka mtu akuangalie unaweka umeme wapi, watu wamejaa vitambi wantia kichefuchefu. Michuzi usinanie hii, hawa jamaa ni wezi tu.
ReplyDelete