Rais Mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania,Mh. Benjamin W. Mkapa akiwa katika mahojiano na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Umoja wa Mataifa,Bi Flora Nducha katika ofisi za Umoja wa Mataifa,jijini New York,Marekani. Mh. Mkapa aliteuliwa wiki iliyopita na Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa,Bw. Ban Ki-moon kuongoza timu ya watu watatu watakaofualitia na kuangalia kura ya maoni ya Sudan Kusini. Mh. Mkapa amesema kura hiyo ni ya muhimu sana kwa hatma ya mamilioni ya Wasudan ambao Januari tisa watapiga kura kuamua endapo eneo la Sudan Kusini lijitenge na kuwa taifa huru ama la na amesema la msingi ni kwa watu kukubali matokeo mara kura hiyo itakapokamilika.. Mh. Mkapa aliyazungumza hayo wakati wa mahojiano na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio ya Umoja wa Mataifa,B. Flora Nducha
Rais Mstaafu wa awamu ya tatu wa Tanzania,Mh. Benjamin W. Mkapa akiwa katika picha ya pamoja na mkuu wa Idhaa ya Kiswahili ya Redio Umoja wa Mataifa,Bi Flora Nducha

Kwa kusikiliza mahojiano hayo ingia katika mtandao wa Redio ya Umoja wa Mtaifa http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili pia kwenye facebook http://www.facebook.com/UNRadioKis au waweza kubonyeza moja kwa moja kwenye mahojiano yenyewe http://www.unmultimedia.org/radio/kiswahili/detail/113198.html

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 8 mpaka sasa

  1. safi sana kaka, mh wetu waukweli sana.
    congrats mkapa.
    pics hiv, very safi.

    ReplyDelete
  2. Mara zote naamini kwa dhati historia huukumu watu. Huyu ni kiongozi bora ameacha legacy...yetu macho kwa legacy itakayofuata. Na cha msingi zaidi katoka madarakani ameacha wengine watawale. Hongera na Mungu akupe afya na maisha marefu Ben!

    ReplyDelete
  3. Thats is Big Ben! Congrats Sir for wat ever u've done!!

    ReplyDelete
  4. mazoezi jamani!

    ReplyDelete
  5. Bro. Ben shavu hillo, doh

    ReplyDelete
  6. Kweli madaraka ya Urais is full of stress! I can now get back the real picture of Benjamin Mkapa, aliyekuwaga Balozi na mwanahabari! (pichani katokea anacheka na looks more relaxed on that interview! sio kama alivyokuwa akitokea TVT ktk Hotuba zake za wananchi za kila mwezi-seriously and tense)
    Hongera Rais Mstaafu for looking after your self well though watch your weight.
    nouvague, Birmingham Uk.

    ReplyDelete
  7. Watanzania tunakutakia afya nje kaka wa taifa, tunakukumbuka kweli kweli. Safi sana.

    ReplyDelete
  8. On of the brainy President my country has had...

    You are the leader and i envy you..

    All the best in your assignment

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...