Vision Investments inayo furaha kuwaletea kwa mara ya tatu mfululizo maonyesho ya magari “ Automotive Festival 2010” . Maonyesho ya siku tatui ambayo yataleta pamoja wadau wanao husika na sekta nzima ya magari na huduma shirkishi zinazohusiana na magari.Tarehe 1 hadi 3 Oktoba 2010.Kiingilio Tsh 2000/- wakubwa na watoto.

Maonyesho haya ya pili ni muendelezo wa maonyesho ambayo yalifanyika Oktoba mwaka 2009. Na hii ni sehemu ya pekee ambayo inawapatia wafanya biashara, wapenzi na watumiaji wa magari na huduma shirikishi fursa yakukutana naku badilishana ujuzi, mawazo na huduma juu ya sekta nzima ya magari. Watoaji wa huduma za mikopo kama Benki ufundi na ushauri wa masuala ya magari watakuwepo.Wataalamu wa michezo ya magari nao watakuwepo kuonyesha ujuzi wao.

Kutokana na mratibu wa maonyesho haya Bw. Ally Nchahaga, “Tanzania Automotive Festival” Maonyesho haya yanategemewa kufanyika kila mwaka mwezi wa kumi.

Wananchi wategemeee kuona na kujifunza masuala mbali mbali kuhusiana na sekta hii nyeti kwa uchumi na maendeleo ya taifa kwa ujumla.

Kauli mbiu ya maonyesho haya ni “Defensive driving key to road safety”

Inaletwa kwenu na: STANBIC BANK, CLOUDS FM, CHOICE FM, SIMBA COACHES, ENGEN,

U - TRACK, SYNOVATE, QUALITY MOTORS, EXPOTEAM,SUPERDOLL, NOBLE MOTORS, EXTREMEWEBTECHNOLOGIES, AAR, KOBA BATTERIES,ULTIMATE SECURITY, STAMBULI INVESTMENTS, NAM ENTERPRISES, OZONE PRODUCTIONS, I – NOCH,AUTO TRADER, G5, WHATS HAPPENING IN DAR,THE BEACHCOMBER TOURS & SAFARIS,HEINEKEN,K-NICE POOL TABLE

Kwa taarifa zaidi tembelea tovuti yetu
www.autofest.co.tz
Barua pepe:
info@autofest.co.tz

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mwaka jana hawakuhakikisha kuwa kuna usalama kwa wananchi wanaokaa kandokando ya barabara wanazozitumia. Kutokana na hilo walisababisha vifo vya watoto na watu wazima. Je, mwaka huu usalama umehakikiwa mpaka mashindano haya yanaruhusiwa?

    ReplyDelete
  2. "Defensive Driving Key to Road Safety", tupe na kiswahili chake kwa sisi ambao "English is not recheable"!!

    ReplyDelete
  3. 'Defensive' au 'cautious' driving???

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...