Na Irene Mark
MVUTANO wa miaka mingi kati ya uongozi wa Kiwanda cha Sukari cha Mtibwa, mkoani Morogoro na wafanyakazi wake na wakulima wadogo wadogo wanaouza miwa kwenye kiwanda hicho umepatiwa ufumbuzi.

Mvutano huo, umemalizika kufuatia mikutano miwili muhimu iliyofanyika baina ya pande hizo tatu chini ya uenyekiti wa Mkuu wa Wilaya ya Mvomero, Fatma Mwasa, kufuatia agizo la Rais Jakaya Mrisho Kikwete, kuzitaka pande hizo kupata majawabu ya haraka ya mvutano huo.

Kufuatia makubaliano hayo, viongozi wa pande hizo tatu pamoja na Mkuu wa Wilaya walimweleza kwa undani Rais Kikwete nini viongozi wa pande hizo mbili wamekubaliana nayo katika jitihada za kumaliza mvutano huo uliochukua muda mrefu.

Akieleza kuhusu makubaliano hayo mbele ya Rais Kikwete na mbele ya uongozi wa kiwanda, viongozi wa wafanyakazi na viongozi wa vyama vya wakulima wadogo wa miwa katika mkutano uliofanyika usiku wa Septemba 7, 2010, Mwasa alisema pande hizo zimebaini changamoto 10 kuu zinazosababisha mvutano kati ya uongozi wa kiwanda na wafanyakazi.

Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na kutokuwapo kwa mkataba wa hiari kati ya wafanyakazi na kiwanda tokea Septemba mwaka jana, ucheleweshaji wa malipo ya pensheni kwa wastaafu, ucheleweshaji wa mishahara, lugha kali zisizovumilika kutoka kwa Meneja wa kiwanda, Greg Swart, ajira kutolewa kwa wageni bila kuzingatia miongozo ya kisera inayohimiza ajira zaidi kutolewa kwa raia.

Kuhusu lugha chafu ya Meneja Greg Swart, Rais Kikwete amejulishwa kuwa meneja huyo tayari amefukuzwa kazi tangu mwishoni mwa wiki kutokana na tabia ya kutukana wafanyakazi na hata viongozi wa Wilaya ya Mvomero.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...