Nina msaada ninaotaka kusaidiwa na watanzania wenzangu hasa walio Tanzania japokuwa hata wanje ya Tanzania nao waweza changia. Mim nipo huku ughaibuni kwa mda mrefu kidogo ila kwa sasa nataka nirudi nyumbani na kuanzisha biashara zangu binafsi ambazo zitakuwa zinahusika na uingizaji wa bidhaa ndani ya Tanzania kutoka USA.
Je ni aina gani ya bishara ninayoweza kufanya yenye manufaa kwangu na watanzania?, ambayo itahusu mambo makuu matatu
MAVAZI, CHAKULA NA MALAZI
Nitashukuru kwa mawazo na michango yenu.
Nitashukuru kwa mawazo na michango yenu.
Mdau Marekani
Kuhusu MAvazi,pamba inalimwa Tanzania njoo ufungue kiwanda hiyo itasaidia kutoa ajira kwa vijana wa Tanzania na si kuagiza mavazi toka huko USA.
ReplyDeleteKuhusu chakula.Kilimo kwanza ndo sera ya nchi njoo ufungue shamba kubwa tu,maeneo ni mengi sana hapa Tanzania.
Kuhusu malazi njoo ujenge nyumba na ukopeshe kwa mkopo nafuu hiyo itasaidia watanzania wengi wasio na nyumba hapa nyumbani Tanzania.
karibu sana mwekezaji toka USA.
CCM 2010 ushindi lazima!!!!!
Kondom kwa malazi salama
ReplyDeleteeebwana kwanza kabla hujaanza biashara ni lazima ufanye utafiti wa kitu gani, target yako ni akina nani na competitors wako ni lazima uwajue so kabla hujaanza biashara embu rudi bongo usome mazingira hata kama utakaa wiki mbili tatu ujionee siku hizi mambo yamebadilika biashara ya mavazi, chakula au malazi nadhani siyo dili kama utaweza kuja na laptops za ukwei utafanya biashara
ReplyDeleteNaona umeshachelewa Ndugu yangu Tanzania kuna kila kitu... Njoo na pesa zako uaanzishe Kilimo kwanza, home ya wazee, lakini hivyo utakavyo vimeshajaa teleee
ReplyDeletehiyo inategemea na mtaji wako na uwezo wako wa kumanage bussiness!! ushasema biashara ya kuingiza bidha tz toka marekani inayosuhusu mavazi, chakula na malazi asa unataka ushauri gani tena?
ReplyDeleteBiashara zinalipa hasa ya Mbao yaani ni noma naposema mbao namaanisha vitanda sofa na nk
ReplyDeleteMdau bongo land
Manazi condom, Chakula dawa za maleria na malazi vyandarua na vitanda.
ReplyDeletemimi nakushauri kwa upande wa mvazi yanalipa
ReplyDeletehongera kwa mawazoyako yakurudi home.
ReplyDeletehiyo nikitu rahisi mbona nduguyangu.
chukua pesa zako nenda kanunue kiwanja.
pahala pazuri then tengeneza kijimotel chako utauza chakula na
watu watalala utakuwa na duka lako humohumo ndani ushamaliza utakacho.
naona itakuwa lengo lako limekamilika. ahsante nenda haraka
usisite kilakitu kujaribu mungu atakusaidi.
Mdau wa Marekani,
ReplyDeleteNaitwa Yussufu Laiza nimeajiriwa na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia.(COSTECH) Naishi Dar es salaam.
Ningependa kukupa ushauri pamoja na kukutaka unibebe katika unachokusudia kuwekeza hapa nyumbani. Biashara inayolipa na kuvutia kwa sasa ni showroom za magari ambazo zinachipuka kama uyoga. Naamini biashara hii ina high risk lakini ina high returns.
Biashara ya pili ni ya chakula. Yaani kufungua hoteli katika business city yoyote ndani ya Dar es salaam mathalan pale Ubungo, au Kariakoo au City Centre au Mwenge na hata Tegeta. Kuhusu mavazi, swahiba sikushauri kwani naona jinsi maduka ya mavazi yanavyododa ingawa wengi hukimbilia Hong Kong na China kutafuta bidhaa. Ila kuna biashara ya vipodozi kama utapata fremu maeneo ya Kariakoo nayo inalipa kwa sana.
Tuwasiliane +255 71 321 1726
WEWE MPUMBAVU NINI? UKITAKA KUFANYA BIASHARA LAZIMA UWE NA WAZO LAKO SIO KUOMBA MAWAZO YA WATU.
ReplyDeleteFANYA BIASHARA YA SIASA. NA UANZE MAPEMA KUTENGENEZA MTANDAO KAMA UNA HELA MARA TU BAADA YA UCHAGUZI 31OCTOBA KWA AJILI YA 2015.
ReplyDeleteStreaptease Clubs!!!!!!!!!!
ReplyDeleteHabari mkubwa. Karibu nyumbani and if you are serious then there are a lot of things you can do.
ReplyDeleteMimi binafsi ni mdau katika Hotel Accomodation (Up market) pamoja na food service. I own small restaurants in Arusha, One Shop dealing with food & beverage supplies and I am a partner katika Lodge iko Tarangire.
You can contact me at peter@osupukolodges.com for more details
Kilimo Kwanza ni biashara nzuri na inayolipa sana kwa sasa, hivyo lete matrekta, mbolea na kila aina ya pembejeo za kilimo ili tuzalishe CHAKULA kwa wingi.
ReplyDeleteHongera Mdau kwa kutaka kuwekeza Tanzania. Kuingiza Bidhaa za chakula, mavazi na malazi kutoka USA utakuwa na wateja wachache sana. Itafaa ikiwa una target Market Segment very specific, maana kitu mfano Nguo kutengenezwa USA na kuuzwa Bongo, wakati hata huko USA wanavaa nguo made in China kwa kukwepa gharama ni kaazi kweli kweli. Labda Malazi kama una maana utaanzisha hotel na kuimport watalii watakaofikia hotelini kwako, hiyo italipa!
ReplyDeletetoa mail yako tuwasiliane, sio kila kitu kinatakiwa kuwa disscussed on public.
ReplyDeleteHii ya chakula mzee sijakuelewa yaani unataka kufanya biashara ya restaurant hapa au uingizaji/utoaji wa chakula/mazao? sijakupata vema!!
ReplyDeleteKwa upande wa mavazi ndugu yangu kazi kwa kweli utakua nayo manake huyo Mao ameharibu vibaya mno iyo yaweza kukupa taabu kidogo kwenye kupata chochote maana wengi wetu wavuja jasho siku izi twakopa zen twaingia biashara ya viwalo sasa upande mmoja Mao amekaba upande mwingine yuko mpemba uku chaga pale kinga na mndengereko weeeeeeeeeeeeeeee.
Uzuri waonesha una jembe la uhakika fanya ya malazi iyo mko wachache wenye kuweza na mahitaji yapo
Laa hasha piga zote mbili wasaidiane
-machache-
utaumia tu ukianza kuleta bidhaa zako za USA mchina kamaliza kila kitu huku vitu bei poa sasa hivyo vya huko aghali hutaweza kupata wateja wa fasta ila jaribu tu maana soko bado lipo
ReplyDeleteNdugu yangu, hapo biashara nzuri ni chupi (underwear)za wanawake. lakini sio zile za vinyuzi zinazoonekana mbele tu na nyuma ni ka uzi tu. Yaani ziwe kama bukta.
ReplyDeleteNi ushauri wangu.
px
Jaribu kwa kuanza kuuza dagaa wakavu na batik you never know. All the best
ReplyDeleteAngalia Hii,
ReplyDeleteKwa ujumla suala la kufanya Biashara Bongo kwa kipindi hiki ni gumu, na hiyo siyo Bongo tu bali ni kila sehemu duniani. Mimi nipo china na huku nakutana wa wamarekani wengi tu wanaokuja kuchukua bidhaa kuja kuuza USA, hivyo ni wazi kwamba itakuwa ngumu sana kwako kuchukua bidhaa USA na kwenda kuuza Bongo na utarajie kupata faida. Ushauri wangu;
1. Usithubutu kuamini kumpa mtu huo mtaji wako ili akusimamie biashara utakayoamua kufanya. Kama utapata biashara basi hakikisha wewe ndiyo main player.
2. Most efficient source ya kupata products za kuuza bongo ni asian countries, kwanza China kisha Japan.
3. Biashara nzuri ni ile ambayo itakushirikisha wewe mwenyewe moja kwamoja bila kutumia mtu wa kati.
4. Kwa kipindi tulichopo biashara ya vifaa vya electronics ni nzuri zaidi muhimu ni kuwa unatakiwa kuwa Very Dynamic, most importantly computers and other digital devices.
5. More details check na mimi sajom06@hotmail.com
Best of Luck
Umefanya vizuri kuomba ushauri maana biashara Bongo ina ugumu wake hasa kama mtaji ni mdogo ambao unakuwa na athari katika kupata eneo kidhi la biashara na ukubwa wa mzigo.
ReplyDeletePili, na muhimu, please!! Bongo imeharibika kwa sasa, si kama zamani, mtu anaweza kukupa contact zake ukamtafuta kumbe yeye nia yake ni kukutapeli vitu kaka simu, gari na kujua mahala unapoishi iliaweze kuleta 'kikosi kazi', sitaki kusema kwamba hawa wote waliotoa contact ni watu wabaya, la hasha, ila tumeona mengi, uwe makini sana.
Nkyabo - Bongo