Hi Anko Michuzi,
Mimi ni mdau niliekua nakula nondo,Boxi na kuishi kwa miaka 15 Nchini USA, Baada ya kuchoka kubeba boxi nikaamua nirudishe timu home na mazaga zaga yangu hadi vijiko. Sasa basi baada ya Container langu kufika Bandarini pamoja na usumbufu wote siku naenda kulipia ushuru Tanzania Custums naambiwa pamoja na kwamba nilipata Tax exemption ya Gari langu na vitu vingine vya ndani maarufu kama Personal effects lakini kutokana na Gari langu kua na umri zaidi ya miaka kumi nikaambiwa siwezi kupata Tax Exemption ya hilo gari japo mimi nimelipakiza mwezi may 2010 na nimelitumia kwa miaka 11 nikijua kitakacho ni cost ni ushuru wa uchakavu tu.
Nilipoulizia nikaambiwa kuna sheria mpya imeanza kutumika majuzi ambayo imesainiwa na kamishina wa TRA bila kujari hiyo gari niipakiza lini hata kabla ya hiyo sheria haijaanza kutumika.
Naomba wadau mnisaidie kujibu maswali yafuatayo:-
1. Je sheria za nchi zinatungwa na kamishina ama Bunge?
2. Kama Kamishina anatunga sheria kwa nini asiangalie ni lini ulipakiza mzigo wako
3. Kwa nini kama sheria zina badilika tuzitangaziwe atleast miezi sita kabla sheria hiyo kuanza?
4. Je nifanye nini maana mpaka sasa hivi nimedata
Asanteni wadau
Mdau aliyechanganyikiwa

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 26 mpaka sasa

  1. pole sana mdau hiyo ndio WELCOME bongo bado huo ni mwanzo tu 15yrs nafikiri ulikuwa umeisahau tz ila sasa itaifahamu vyema,sijui umerudi na $$$$ za kutosha kwani kama unataka kufanya biashara watakuletea VAT za hadhi yako-mdau canada

    ReplyDelete
  2. pole sana kwa matatizo,hiyo ndio TRA,ni idara inayojitungia sheria na serikali inawaangalia tu,is untouchable,hapo watakuzungusha na kila siku wanaongeza charges,usipoangalia utakosa yote,tafuta pesa uitoe haraka kabla hawajaanza kuinyofoa mataa.ndio karibu nyumbani hiyo.

    ReplyDelete
  3. Chukua Vacation, relax your mind. Utapata ufumbuzi na kujifunza namna ya kufanya maamuzi na kudeal na system ili ufanikiwe. Usichangayikiwe, Bongo itabadilika baadae sana.

    ReplyDelete
  4. Pole.

    (US Blogger)

    ReplyDelete
  5. pole sana mdau,mwambie akupe nakala ya hiyo sheria, kisheria wanatakiwa wakuonyesha endapo uta request wakikataa nenda ukatafute kwa ajili ya kuomba ushauri. chuo kikuu cha DSM wanapatikana wa bure.

    ReplyDelete
  6. Pole sana. Kwa taarifa tu hao watu wana kazi mbili kukusanya mapato ya taifa na nyingine ni kukomoa watu wengine hasa wakikuona unataka kuishi maisha mazuri. Wanavyojua wao ni kwamba maisha mazuri wanatakiwa wawe nayo wale wanaofanya kazi TRA tu. Sheria huwa inalazimishwa imuumize mwenanchi zaidi kuliko malengo ya kutungwa kwake.

    ReplyDelete
  7. Kaka hapa bongo kalipe uchangie maendeleo ya nchi yako we si unasikia bajeti ina nakisi? kalipe acha kulalama wewe, tumia hela ikuzoee.

    ReplyDelete
  8. unajinsi nenda kwa mlango wa nyuma watakuachia hao, ukikomaa hivyo vitu utavikosa, hii ndio bongo, well come bongo

    ReplyDelete
  9. lakini mdau ilo gari ulilotumia miaka 11 huku Bongo unalileta la nn? si uneliuza huko huko uje kununua gari ya karibuni huku, magari mabovu hayatakiwi huku Bongo ndio maana wanaweka sheria ngumu kuyadhibiti. Gari lenye miaka 11 ni la kizamani sana (lina umri kama mtu) sidhani kama linastahili kuingia Tz. Tunataka maendeleo kama waliopo Bongo wamekataza gari lenye miaka 10 au zaidi lisiingie kwa kuweka kodi zaidi wadau mlioko nje mfuate sheria hizo

    ReplyDelete
  10. oohhh!!! mzee pole sana, unajua sie hatuna nchi endelevu ila tuna tuna nchi kandamizaji hasa kwa mtu wa kawaida, hakuna sheria za mr. flan ila ni ubabaishaji tu na mazoea ya sehemu flan kana kwamba ni nyumbani humo tra. na hayo ndugu ya ni madogo tu! uliza zaidi utajua tena ya kinyama ile mbaya kuna watu wanaanza upya maisha sasa kwa ajili ya hao watu, sie hatuna nchi ni genge la watu flani limekusanya ili kufanya ya kwao hususan nafsi zao ziwe safi sio kwa wewe mwananchi wa kwaida uliondoka kwa kuchangiwa na ukoo mzima nauli, shamba kuuzwa,nyumba kuwekwa rehan, sasa leo unarudi kujisaidia masha yako na familia yako unakutana na mashetan mlangon, ni bora unakuwa mtumwa kwa watu huku kuliko home, so jitahid kuitoa haraka maana ndugu inaweza kukushinda baada ya charges kuwa zinaongezeka siku baada ya siku, home pagumu sana du!!

    ReplyDelete
  11. Kinachosikitisha zaidi ni matumizi ya hizo pesa wanazokusanya kwa walipa kodi........kimsingi zinapaswa kurudi kwa wananchi kupitia njia mbalimbali lakini zinaishia palepale mjini kwenye wizara mbalimbali.

    Mashangingi, safari nyingi zisizoisha, warsha na semina n.k.

    Bado kazi nzito....nadhani hata uhuru hatujapata...amani ipo huku watoto wanakaa chini mashule, huduma za afya duni........tabu tupu...hata hao WB, global fund, Millenium challlenge ...hamna kitu makaratasi na mikutano mingi..lakini walengwa hawapati hata 10% ya malengo.

    ReplyDelete
  12. Ni kweli kwa mujibu wa mabadiliko yaliyofanyika kwenye budget ya 2010/2011 the goverment has restricted exemption on motor vehicles aged 10 years or more from the year of manufacture to Civil servants, Returning Residents, Non Govermental Organizations and Investors Registered under Tanzania Investment Centre

    ReplyDelete
  13. ACHA URONGO NDUGU, HAKUNA UKWELI WOWOTE KATIKA MAELEZO YAKO, MASWALI YAKO YA MSINGI NI SWALI LA KWANZA HADI LA TATU, INAONEKANA HIYO NI HOMEWORK UMEPEWA DARASANI, SASA UNATAFUTA MAJIBU KIJANJA...ACHA KUSUMBUA WATU AKILI

    ReplyDelete
  14. Sheikh ShangaroroSeptember 30, 2010

    jiunge haraka na kampeni ya ccm ukipata mwanya mnong'oneze brother K.tatizo lako utafanikiwa.

    ReplyDelete
  15. Mdau Pole sana, lakini huna haja ya kuchanganyikiwa sana cha msingi kaa nao hao wahusika wa TRA waone jinsi wanavyoweza kukusaidia naamini utafikia ukomo wa tatizo lako wasipokuelewa waachie tu hilo gari.vile vile TRA ni mamlaka iliyoshoindwa kabisa kwenye ukusanyaji wa kodi zenye tija wameshindwa wanabaki kubanana na vigari chakavu tu vya wanafunzi, migodi na vyanzo vingine vyenye kodi kubwa hawaendi kabisa huko. TRA ni taasisi ya dhuluma na unyang'anyi tu ni wavunaji wasio panda chochote, wezi tu.

    ReplyDelete
  16. mimi nakushauri kwanza clear item nyingine zote ibaki gari, then beba documents zote halafu nenda uombe kukutana na director ama mkuu wa kitengo husika. Kwa kufata protocal, akishindwa kukusaidia basi omba kumwona wa juu yake, ikitokea umeshawaona wote na hawajakusaidia. Basi nenda kafungue kesi mahakamani na tafuta wakili wa serikali ambaye yeye atakupa masaada huo bure kabisa. I am telling you hata kama gari hiyo itaozea huko, but they will compasate kwa sababu katika hali ya kawaida item inaangaliwa ile siku/tarehe ambayo ilitumwa na si kufika. Hata hivyo ni kwa nini hivyo vitu umevituma may halafu vimefika september?!

    ReplyDelete
  17. Pole sana. Hiyo ndiyo bongo, wivu witu tu. Sheria zinatungwa kwa kuangaliwa kwenye sura. Nakushauri tafuta ela utoe mizigo yako kabla haijapotea pia. utafatilia sheria mpaka mambo mengine yatasimama.

    ReplyDelete
  18. pole sana mdau.. hata ukisha kulipa hizo pesa zitakwenda mifukoni mwa watu.. hazitotumika kwenye maendeleo ya taifa.. kwa hivyo inazidi kutia magazabu ukitaka kulipia kodi

    ReplyDelete
  19. Sheria ya kutoza ushuru wa ziada kwa magari chakavu yenye umri wa zaidi ya miaka kumi ilipitishwa na bunge miaka mitatu iliyopita na kusainiwa na rais kuwa sheria kamili miaka miwili iliyopita.Hao jamaa wa TRA wana ugumu wa kuelewa sababu tofauti ya miezi michache haiwezi kuwa kigezo cha kusimamia kuwa ulipie hiyo excise duty.Pole mkuu na karibu bongo

    ReplyDelete
  20. pole kaka,
    hiyo sheria imepitishwa juzi ktk bunge la bajeti lililopita, nilivyoielewa mimi ni kuwa wote wenye misamaha ya kodi, haswa wafanyakazi na returning residence, kuwa utasamehewa kodi yote ikiwa gari lako lipo chini halizidi miaka kumi, so ni sheria ya bunge. tatizo la nchi yetu sheia hutungwea na kufunikwa kwenye makabati wakisubiri wakiukaji. wtu hawakueleweshwa juu ya hilo. pole kaka, k

    ReplyDelete
  21. Pole sana ,Kwa taarifa yako hiyo sheria ipo miaka tangu 2006.Wewe unatakiwa ulipie tu hizo charges otherwise utajikuta unalipa storage kubwa sana kuliko gharama ya gari.Hao TRA ukibishana nao utakesha tu.Its better you acts ASAP

    ReplyDelete
  22. Ndugu,
    Niseme tu ulifanya timing mbaya sana. Unasema ulilipakiza gai mwezi May 2010Yaliyotokea yamesababishwa na haya yafuatayo:

    1) Sheria ya tax exemption kwa wanafunzi wanaorejea ina restrictions zake. (kama pia ilivyo tax exemption ya public servants wanaoagiza gari). Gari likishazidi miaka 10 kwa kawaida halina exemption na hata wale ambao hawaombi exemption hutozwa anti-dumping fee over and above normal tax. Hii huchajiwa kwa kila mwaka lililozidi.Lengo ni kuzuia tz kuwa jalala la bidhaa kuukuu za huko kwa wenzetu.

    2) Sheria hazitungwi na commissioner, lakini commissioner anatumia sheria ya bunge au regulations za waziri-ambazo zinaruhusiwa ktk hiyo sheria ya bunge. kwa hiyo, kwa kuwa mwezi wa saba kila mwaka kuna marekebisho ya kodi-yanayotokana na bajeti kuna sheria inayoitwa Finance Act ambayo lazima kila mwaka inaintroduce marekebisho mapya ktk sheria za kodi. So, huo utaratibu mpya utakuwa umekuwa interoduced na Finance Act, 2010, ambayo ilianza kutumika July. Ingekuwa gari lilishafika before July ndio wangetumia sheria ya zamani. Lkn kama lilifika baada ya july 1 inawezekana sheria hiyo imesema iko applicable, notwithstanding the date of shipment.(only the date of arrival was relevant).

    3) Kama unahisi hamna haki, unaweza kulodge objection na Tax Revenue Tribunal hapo dar na hilo swala litasikilizwa kwa haraka sana. Ni mahakama maalumu ya mambo ya tax na hushughulikia kwa haraka. Wakati unasubiri uamuzi malipo ya kuhifadhi gari bandarini hayatalipiwa (i hope bado sheria inadai hivo). So, utafute lawyer akusaidie. Lkn uassess kwanza feasibility ya hili.
    Pole sana, na hiyo ndio sheria. Itakubidi ulipe kodi yote, na hiyo anti-dumping fee ya mwaka 1. Sasa uombe Mungu na TRA wasifanye arbitrary uplifting ya cost za gari.

    ReplyDelete
  23. Gari yoyote inayoingizwa tz ikiwa na umri zaidi ya miaka 10 ni lzm ilipiwe 25% zaidi ya CIF ya hiyo gari, haijalishi km huko inakotoka ulikuwa ukiitumia au ndo umeiagiza kwa mara ya kwanza.

    kamishina wa kodi kwa niaba ya waziri wa fedha anayo mamlaka ya kutunga bylaws kwa ajili ya kugovern ukusanyaji wa mapato ya serikali.

    usijali kaka, hii ni ktk kutunza mazingira yetu!! pole sn na karibu nyumbani!

    ReplyDelete
  24. Kaka soma hapa chini ndo uwajue vizuri TRA

    Wakongo waandamana Dar
    na Mwandishi wetu

    WAFANYABIASHARA na waagizaji wa magari kutoka nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC), wameandamana wakiilalamikia Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), kuwazuia kutoa magari yao bandarini bila kuwapa sababu za msingi.

    Tukio hilo lilitokea mjini Dar es Salaam jana, ambapo wafanyabiashara na waagizaji hao walilazimika kuandamana kutoka bandarini hadi kwenye ukumbi wa Karimjee kwa ajili ya kumtafuta Kamishna wa TRA, ambaye alikuwepo hapo kwa ajili ya kuhudhuria mkutano.

    Wakizungumza na waandishi wa habari, Wakongo hao walisema magari yao yamezuiliwa kwa kipindi cha muda mrefu na ilidaiwa magari hayo yana mfumo wa usukani wa upande wa kushoto badala ya upande wa kulia, kitu walichosema eti ndio sababu ya kutopewa na kusema si sababu ya msingi kwao.

    “Sababu iliyotolewa si ya msingi kutokana na nchi yetu kutojali mfumo wowote wa usukani wa gari. Sisi tunataka Mamlaka ya Mapato waruhusu tuchukue magari yetu hata kama yana matatizo yatajulikana huko nchini kwetu Kongo, wala si hapa Tanzania,” alisema mmoja wa Wakongo ambaye hakutaka jina lake litajwe.

    ReplyDelete
  25. kwa mawazo yangu kwako rudi usa kapige miaka yako 25 mingine hata ukirudi bongo unarudi na mkongojo wako,labda sirikali itakuwa nyengine na mambo mengine.

    ReplyDelete
  26. Hili ndilo tatizo la these clowns that have never ran a business making the rules. Hawajui kuna magari ya miaka 30 yenye thamani kuliko magari mapya. Pia wao hawalipi hizi kodi kwa hiyo hawajali wala hawaelewi kuwa mtu hanunui gari la zamani kwa mapenzi yake. Pia gari lililotumika mtoni hata la miaka kumi bado ni mali tu. Huku wenzenu tukinunua gari kodi ya mauzo ni asimia 6.25 naliweka barabarani sasa hizi asilimia 50 tena si ndio maana tunaendelea kupiga boxi tu!!! Pole lakini mdau wakishakuboa vya kutosha rudi tuendelee kupiga boxi mpaka kieleweke maana bado linalipa.

    Mdau, Boston, U.S.A.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...