Mkurugenzi wa benki ya NBC, Lawrence Mafuru (kulia) akizungumza na wageni wakati wa tafrija maalum ya Benki hiyo kwa washiriki wa Mkutano wa 20 wa Mwaka wa PPF mjini Arusha.
Mkurugenzi Mkuu wa benki ya NBC Bw. Lawrence Mafuru (kushoto) pamoja na Mkurugenzi wa Masoko wa NBC Bw. William Kallaghe wanaonekana wakiingia katika mkutano wa 20 wa Wadau wa Mfuko wa PPF uliofanyika jijini Arusha hivi karibuni. Kwa nyuma anaonekana Mshauri wa mambo ya Uhusiano na Jamii-NBC Bi. Rachael Kimambo.
Mkutano ulikutanisha wadau mbalimbali na baada ya shughuli za mchana wote, wageni walijumuika pamoja na kubadilishana mawazo wakati wa chakula cha jioni kilichokuwa kimeandaliwa na benki ya NBC. Katikati anaonekana Bw. Lawrence Mafuru ambaye ni Mkurugenzi Mkuu wa benki ya NBC.
Baadhi ya wageni waalikwa wakiwa katika tafrija hiyo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. Picha ya kwanza namuona Ansger Mushi anamkumbushia Lawrence Mafuru kuhusu beef lao la uongozi walipokuwa chuoni ...wakati huo Ansger Mushi alikuwa mgombea wa uraisi na Lawrence naye alikuwepo kwenye uongozi wa chuo hahahaha !!!! Dunia kweli duara jaribu kutengeneza marafiki wengi kuliko maadui kwani hujui kesho itakuwaje
    Hongereni nyote , Mushi na Mafuru kwani nimesikia Mushi naye ni bosi fulani pale ILO

    Ni mimi mwanachuo mwenzenu

    Gauss
    gauuzz@yahoo.com

    ReplyDelete
  2. Mafuru hizo mvi za kweli au za bandia? kumbe chartered institute of bankers exams zinalipa namna hiyo?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...