Tanzania imepewa Tuzo ya Umoja wa Mataifa ya Millenium Development Goals (MDGs) 2010 : The Global Heabeat kutokana na mafanikio makubwa iliyoyapata katika maendeleo ya Elimu katika sherehe zilizofanyiaka kwenye ukumbi wa Waldorf Astoria Grand Ballroom jijini New York Septemba 19, 2010. Pichani Waziri Mkuu Mizengo Pinda akipokea tuzo hiyo na kutoka kwa Mmoja wa wasimamizo wa shughuli hiyo na Msanii maarufu , John Schneder.
Pichani Waziri Mkuu Mizengo Pinda na Balozi wa Tanzania kwenye umoja wa mataifa, Ombeni Sefue wakiwa wameshika tuzo hiyo baada ya kukabidhiwa
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akiwa na Naibu Katibu Mkua Umoja wa Mataifa, Dk. Asha Rose Migiro kabla ya mazungumzo yao kwenye hoteli ya Intercontinental jijini New York Septemba 19, 2010. Mheshimiwa Pinda yuko New York kumwakilisha Rais Jakaya Kikwete katika Mkutano wa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa linalojali Maendeleo ya Millenia.

Labda sijaelewa, kidedea kivipi wakati report inasema tuko nyuma, au ndio propaganda hata kama watu wanalala njaa jamani? Usibania naomba kuelimishwa tafadhali
ReplyDeleteAsante Dakta Rose kwa mitindo kutoka Afrika. Unajua kuyapangilia mapigo ya kibantu.Tanzania inawakawaka ndani ya Waldorf Astoria, sio mchezo. Sifa za kweli au mnatupaka mafuta ili mtuchune vizuri?
ReplyDeleteMichuzi nani anakutumia hizi picha za NY haraka namna hiyo?
ReplyDeleteMi nadhani uko kwenye kampeni mikoani kule kwenye kuku kapanda baiskeli bata kavaa raizoni,ahahaha! Au PInda mwenyewe anakutumia? LOL!
Kaka hii si zarau hii jamani? enhe? Si zarau.
ReplyDeleteYaani Waziri Mkuu mzima anakabiziwa zawadi na MSANII? kiprotokali iko sawa hii?
Angekuwa Waziri Mkuu wa nchi zilizoendelea angekabiziwa zawadi na Msanii?
Aaa jamani!?
NI KWELI DR ROSE HUWA ANAPENDEZA SANA NA NGOU ZAKE I HOPE MAMA PINDA ANGETAFUTA FUNDI MZURI WA NGUO ZAKE NAYE HUWA ANAPENDA KUVAA NGUA ZA KIAFRIKA LAKINI NAONA FUNDI WAKE ANAMWANGUSHA
ReplyDeleteHii inaitwa INFIRIORITY COMPLEX kwa waafrika wengi Wasanii ndiyo watu muhimu kwenye campaign kama hizi na zingine kama malaria na HIV PM umependeza sana kula kuku baba
ReplyDelete