mkutano wake na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, jana. Kulia
ni Mwenyekiti wa Baraza la Ushauri la Vyama vya Siasa, Juma Ali
Khatibu.
Msajili wa vyama vya siasa nchini,John Tendwa amesema leo hana taarifa yoyote ya kutoa kuhusiana na pingamizi la CHADEMA dhidi ya mgombea urais kupitia Chama Cha Mapinduzi CCM Dr. Jakaya Mrisho Kikwete kuwa aliahidi kuongeza mishahara ya wafanyakazi bila kuhusisha Bunge kitu ambacho kinaenda kinyume na sheria ya Fedha za Uchaguzi.
Bw. John Tendwa alikuwa ameahidi kutoa taarifa baada ya siku tano, hata hivyo leo waandishi wa habari walipokwenda ofisini kwake kwa ajili kutaka kujua hatma ya suala hilo, alisema kuwa leo ana mkutano mwingine, na kuhusu pingamizi la CHADEMA tayari ameshavijibu vyama na pia taarifa ipo Tume ya Uchaguzi ya Taifa .
Hivyo akashauri Waandishi hao waende kwa vyama husika na kuwauliza, aidha akaongeza kuwa vyama hivyo pia bado vitalazimika kuwa na muda wa kutosha kupitia kwa kina majibu hayo.
Hata hivyo habari ambazo zimeifikia Globu ya Jamii zinasema Msajili huyo wa vyama vya siasa ametupilia mbali malalamiko hayo.
HIS MASTERS VOICE, HUYU TENDWA VIPI MBONA SIMUELEWI KWANI PINGAMIZI NYINGINE ZILIKUWA ZINATOLEWA MBELE YA WAANDISHI WA HABARI SASA IWEJE HII ASEME INAWEZA KUHATARISHA USALAMA? SIJUI NA MATOKEO YA UCHAGUZI PIA YATATUMWA KWA VYAMA HUSIKA VITANGAZE? AAH TENDWA UMEPEWA MZIGO MZITO NA RAISI ULIYEKULA KIAPO CHA UTIIFU KWAKE.
ReplyDeleteMUNGU IBARIKI TANZANIA IENDELEE KUWA NA WANANCHI WENYE ROHO ZA KUPUUZIA MASWALA TETE KAMA HAYA MAANA INGEKUWA NI KWA NCHI NYINGINE MTU KAMA TENDWA AU/NA CCM WASINGETHUBUTU KUWACHEZEA WATANZANIA NAMNA HII KUFANYA UONEZI WA WAZI NAMNA HII. TUOMBE MUNGU WASIJE WAKATOKEA WATU WENYE MISIMAMO YA KWELI DAMU IKAMWAGIKA NCHINI KWETU KUWATOA WATU AMBAO WANADHANIA TANZANIA NI NCHI YAO NA WANAWEZA KUIFANYIA WATAKALO.
ReplyDeletemichuzi plz uspuuze hii coment ni yangu siyo yako wewe
Tuliyategemea haya majibu... Hata aibu hawana!!!!!!
ReplyDelete