Afisa Mtumishi Mkuu wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya,Bi. Aida Tesha (kushoto) akiongea na vyombo vya habari katika ukumbi wa mikutano wa tume hiyo wakati wa kukabidhi msaada wa Kompyuta ikiwa pamoja na Hp Laser jet P2055 Printer, APC Back-ups 650VA na Kasperky Antivirus 2010 Licensed, yenye thamani ya Tsh. 2,643,500/=.kwa Asasi ya Guluka Kwalala inayoshirikiana na Tume kukabiliana na kudhibiti matumizi wa dawa za kulevya nchini.kulia ni Mkemia Mwandamizi wa wa Tume,Bw. Yovin Ivo.
Katibu Mtendaji wa Asasi ya Guluka Kwalala,Bw. Bernard Ndunguru akitoa maelezo kwa vyombo vya habari namna wanavyokabiliana na matumizi ya dawa za kulevya pia alitoa shukrani kwa tume juu ya msaada walioupata na kusema hivyo vifaa walivyopewa vitasaidia sana kuchapisha nyaraka muhimu wakati wa utendaji.kulia ni Afisa Mtumishi Mkuu wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya,Bi. Aida Tesha.
Afisa Mtumishi Mkuu wa Tume ya Kuratibu Udhibiti wa Dawa za Kulevya,Bi. Aida Tesha (kati) akikabidhi printa kwa Katibu Mtendaji wa Asasi ya Guluka Kwalala,Bw. Bernard Ndunguru (kushoto) ukiwa ni msaada uliotolewa na tume kwa Asasi hiyo.kulia ni Mkemia Mwandamizi wa wa Tume,Bw. Yovin Ivo.
Baadhi ya wanahabari waliofika katika mkutano huo.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

0 comments so far,add yours

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...