
Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji nchini (TIC) na Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw.Emmanuel Ole Naiko akimkabidhi kinyago Miss Tanzania 2010 Geneviev Emmanuel kama sehemu ya kwenda kuitangaza nchi yetu,Mlimbwende huyo anatarajia kuondoka nchini kesho kuelekea Beijing,China ambako mashindano hayo yatafanyika.

Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji nchini (TIC) na Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw.Emmanuel Ole Naiko akimvisha skafu yenye bendera ya Taifa Miss Tanzania 2010,Geneviev Emmanuel katika hafla fupi iliyofanyika leo katika viwanja vya kituo cha uwekezaji nchini (TIC).mrembo huyu anataraji kuondoka nchini kesho kuelekea Beijing,China kwenye mashindano ya Dunia.

Miss Tanzania 2010,Genevieve Emmanuel akiwa na mgeni rasmi katika hafla hiyo,Mkuu wa Sekta Binafsi nchini,Ester Mkwizu (pili kushoto) na baba yake mzazi, Emmanuel Mpangala pamoja na Mama wakiwa katika picha ya pamoja katika halfa hiyo ya kumuaga mrembo huyo iliyofanyika leo jijini Dar.

Mkurugenzi wa kituo cha uwekezaji nchini (TIC) na Mlezi wa Kamati ya Miss Tanzania Bw.Emmanuel Ole Naiko akizungumza kwenye hafla fupi ya kumkabidhi bendera Miss Tanzania 2010 kwenye viwanja vya TIC mapema leo asubuhi jijini Dar

Mwenyekiti wa kamati ya Miss Tanzania,Hashim Lundenga akizungumza kwenye hafla fupi ya kumkabidhi bendera Miss Tanzania 2010 kwenye viwanja vya TIC leo jijini Dar

mtaalamu wa mambo ya habari wa Vodacom Tanzania,Matina Nkurlu (katikati) akiwa na wadau wengine katika hafla hiyo fupi ya kukabidhiwa bendera ya Taifa,Vodacom Miss Tanzania 2010 Genevieve Emmanuel.

Baadhi ya wanahabari na wadau wengine wakifuatilia kwa makini shughuli hiyo ya kukabidhiwa Bendera ya Taifa Miss Tanzania 2010, Genevieve Emmanuel iliyofanyika leo katika viwanja vya kituo cha uwekezaji nchini (TIC).
Namtakia safari njema mrembo wetu.
ReplyDeleteMungu amjalie aweze kuitangaza vyema nchi yetu ya Tz
haya dada kazi kwako "go and make us proud" all the best.
ReplyDeletesiku ya kurudi nadhani mtakua hapo watu wote hao kumpekea pia.
ReplyDeleteNaomba nitoe ushauri wa bure. Nchi za wenzetu wanachagua Ma Miss wa nchi zao kuanzia kipindi hiki hadi mwisho wa mwaka. Eg Miss India anachaguliwa around Nov au Dec. Mshindi anakuwa anaandaliwa kuanzia mwanzo wa mwaka mpaka muda wa Miss World Competition. Kwa hiyo anakuwa na muda wakutosha wa maandalizi. Sasa hapa TZ tunachagua a few weeks before Miss World. Wengine hata sura yake bado hawajaizoea. Pia it means hamna maandalizi, then what do we expect? Ma Miss wa nchi zingine wakitoka kwenye mashindano ya Miss World ndio wanakuwa wanamalizia reign yao ya ku represent nchi zao. Sasa wakwetu akirirudi (bila mafanikio) ndio anaanza reign yake. Nadhani hata yeye atakuwa ana lack motivation maana she has nothing more to expect. Could be ndio maana wengi wanaishia kwenye magazeti ya udaku. Kama nikuwakilisha nchi tayari alishawakilisha. Ni ushauri wa bure. Comments are welcome.
ReplyDeleteNdo maana mnashindwa kila mwaka. Mtu kachaguliwa juzi tu no maandalizi, haya leo mnamuaga kwenda China. Anaenda kufanya nini? Kheee nyie vipi??????????
ReplyDelete