Mkurugezi wa Uhusiano Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akimkabidhi funguo za gari Mshindi wa moja ya magari 100 katika promosheni ya Shinda Mkoko inayoendeshwa na Vodacom Tanzania,Aprina George Chuma. Tayari washindi 30 wameshajishindia magari na kuna magari mengine 70 yanaendelea kushindaniwa katika promosheni hiyo, kulia ni Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania Ephraim Mafuru na anayefuatia ni Mkuu wa Idara ya mahusiano ya wateja Aika Makindara na kushoto ni Mkuu wa kitengo cha usafirishaji wa Vodacom Tanzania Ezekiel Majere.
Mshindi wa shindano la shinda Mkoko linaloendeshwa na Vodacom Tanzania,Aprina George Chuma katikati akionyesha funguo ya gari lake mara baada ya kukabidhiwa rasmi akiwa kwenye picha ya pamoja na Idara husika ya usimamizi wa mahusiano ya wateja,kutoka kushoto Mary Natema,Aika Makindara, Yvonne Maruma, Deus Ntukamazina.
Mshindi wa shindano la shinda Mkoko linaloendeshwa na Vodacom Tanzania,Aprina George Chuma Mkazi wa Tegeta Dares Salaam akijaribu kuendesha gari lake baada ya kukabidhiwa rasmi na Mkurugenzi wa Uhusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba anayemuelekeza dirishani.

Kundi la kwanza la washindi wa promosheni ya Shinda Mkoko kutoka Vodacom Tanzania limekabidhiwa magari yao katika hafla fupi iliyofanyika katika duka la Voda (Vodashop) lililopo Mtaa wa Ohio jijini Dar-es-Salaam.

Mkurugenzi wa Masoko wa Vodacom Tanzania, Ephraim Mafuru, alisema kuwa washindi wataendelea kukabidhiwa magari yao kadri promosheni hiyo itakavyokuwa ikiendelea.

Vodacom Tanzania inawapa wateja wake fursa ya kushinda gari aina ya Hyundai i10, kila siku kwa siku 100 (zaidi ya miezi mitatu). Promosheni hii ya kihistoria ilizinduliwa Jumatatu tarehe 2 mwezi Agosti mwaka huu.

Promosheni ya Shinda Mkoko ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 10 ya kuwepo kwa Vodacom nchini Tanzania. Promosheni hii itakapofika ukingoni, magari 100 yatakuwa yametolewa , kila moja likigharimu shillingi million 12 za kitanzania.

Watumiaji wote wa mtandao wa Vodacom wanaweza kushiriki katika promosheni hii.

“Tunasherehekea miaka kumi ya kutoa huduma zetu hapa nchini, kwa ubora na mafanikio, hivyo tunawiwa kurudisha fadhila kwa wale walioyawezesha mafanikio haya” alisema Mafuru.

Hyundai i10 ni gari mahususi kwa mijini, linatengenezwa na kampuni ya Hyundai Motor na kuzinduliwa tarehe 31, oktoba 2007.

Gari hili hukupa faraja zote za gari la kifahari, na wakati huohuo ni gari lenye gharama nafuu za utunzaji na pia matumizi madogo ya mafuta.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Namuona pale Mary natema akiuza sura, vipi baby wako hajambo.

    ReplyDelete
  2. MMh huyo mshindi bonge la kabati!

    ReplyDelete
  3. KAMA BAADHI YA MAONI KUHUSU SHINDANO HILI YANACHAKACHULIWA, BASI UKWELI WAKE WA USHINDI UNANITIA MASHAKA.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...