Mkufunzi wa Waalimu wa kufundisha watoto wa shule za awali kutoka Afrika Kusini, Mariam Ellokene akiwafundisha baadhi ya Waalimu wa Mkoa wa Dar es Salaam mbinu mbalimbali za ufundishaji kwa Watoto hao wakati mafunzo ya siku tatu yaliyomalizika jana Jijini Dar es Salaam, yalifanyika kwa ushirikiano wa Pearson Longman Tanzania, Longman Foundation na Mradi wa Vitabu wa Tingatinga.
Mwezeshaji wa mafunzo ya Waalimu wa Dar es Salaam wa watoto wa awali akiwaelekeza jambo Waalimu wakati wa mafunzo yao ya siku tatu yanayoendelea kuhusu mbinu mbalimbali za ufundishaji kwa watoto wa Shule za awali, mafunzo hayo yanayoendelea Jijini Dar es Salaaam, yalifanyika kwa ushirikiano wa Pearson Longman Tanzania, Longman Foundation na Mradi wa Vitabu wa Tingatinga

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Sijui kama walielewa lugha maana kiingereza chake kigumu.

    ReplyDelete
  2. Msaada tutani.......nimewahi kuona cartoon za Tinga tinga kwenye channel ya South Africa na niliposoma majina ya washiriki na maProducer wengi wao ni watani wa Jadi (kenyans) akiwamo Eric Wainaina. Hili likoje? copy rights za hili jambo likoje? Nachukulia Tinga tinga kama alama ya taifa au urithi wetu wa Taifa. Naomba ufafanuzi/kujuzwa.

    ReplyDelete
  3. Ankal ukoje? .....nimeuliza humu ya kuwa inakuwaje hii Tinga Tinga inatengenezwa kama Cartoon series South Africa? na maproducer ni wakenya akiwamo Eric Wainaina? hakimiliki ya Tinga Tinga ikoje? ukamuua kubania! unakera!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...