LEO TAREHE 29. 09.2010
MWL. LAUREAN MUGOA MUTALEMWA
ANATIMIZA:
MIAKA 85 YA KUZALIWA;
MIAKA 75 YA KUBATIZWA NA
MIAKA 28 YA KUSTAAFU UALIMU.

TUNAMSHUKURU MUNGU KWA KUTUJALIA WAZAZI MAKINI:
BABA MWL LAUREAN MUGOA NA MAREHEMU
-MAMA JULIANA MEMBA MUGOA.










Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 5 mpaka sasa

  1. Waihuka muno Ta Mugoa....Nitukwendera emilembe ya Nyakusinga.....Nimefurahi sana kuona picha yako, maana nakumbuka wakati nikiwa Kagera Miaka ya 60, nami wakati huo nilikuwa na miaka 7.Nawashukuru sana watoto wako wamekulea vema, Kuna mtoto wako anaitwa Mechtilda tulikuwa tukisali naye kanisani Katoma..
    Ningependa kuwasiliana naye.....rosalindajenes@yahoo.com

    ReplyDelete
  2. hongera sana Mwl Mugoa, pamoja na familia yako wote, Mungu amekulinda umefika hapo, ni jambo jema, na zuri na lakupendeza ndugu, wakikaa pamoja kwa upendo na kufanya jambo zuri namna hiyo, nampongeza Mechtilda Mugo pamoja na ndugu zake wote kwa kuandaa kitu kizuri kama hicho. ni jambo zuri. Mungu awabariki sana!!!!!!

    ReplyDelete
  3. Hongera sana Mwl. Mugoa, Mungu akuzidishie nguvu ufika miaka 100 na kuendelea. Nakumbuka nilikuwa nakuona ukifundisha Kashozi boys nami nasoma Kashozi girls. Mimi ni mzee kwa sasa nina miaka 50. Nimefurahi sana kuona bado upo hai ni jambo la kumshukuru Mwenyezi Mungu. Mungu awabariki sana watoto wako. Nakumbuka miaka ya 1967/8 ulikuwa unaendesha gari aina ya V/wagen ya blue, kwa walimu wote wa boys Kashozi, wewe ndiye aliyekuwa na gari enzi hizo ukipita tunashangilia Mwl. Mugoa huyo ! hiyo ilisaidia wanafunzi wote wa girls na boys kukujua kwa sababu ya gari lako.

    ReplyDelete
  4. wao! inafurahisha sana...ni bahati iliyoje kuwa na watoto wanopatana?

    Kama watoto hawapatani, na wazazi wanapata shida uzeeni. Lakini ona, mzee huyu alibarikiwa. Nami nilienda kutembea Kagera na rafiki yangu tukaenda kusali kwenye kigango kimoja karibu na nyumbani kwa huyu mzee, ebwanaeee watoto walimnunulia vx ndio inayotumika kumpeleka kanisani , wakampa na dereve wake. Inafurahisha. Nilimuuliza rafiki yangu kama ndiye chifu wa zamani wa wakagera! akasema hapana, ni kazi ya watoto aliwalea vema. Ohooo anapata ulimwengu maridhawa. Naomba Mungu amuongezee miaka aendelee kufaidi matunda.

    Natoa wito kwa watoto wote waige mfano huu ili dunia ipate baraka.

    ReplyDelete
  5. Babu Hongera Sana.Iam very much proud of you and am happy to be your grandson

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...