Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Emmanuel Ole Naiko akizungumza leo katika uzinduzi wa huduma mpya mbili za kibenki zitolewazo na benki ya UBA.Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Emmanuel Ole Naiko (kushoto) akiangalia simu yake ya kiganjani kuona ufanyaji kazi wa huduma mbili mpya za kibenki zilizozinduliwa na benki ya UBA leo jijini Dar.wanaoangalia ni Mweka hazina wa Benki hiyo kwa hapa nchini,Alexander Ngusaru na Meneja mkuu wa benki hiyo,Imo Etukpicha ya pamoja,kutoka kulia ni Mweka hazina wa Benki hiyo kwa hapa nchini,Alexander Ngusaru,Mwenyekiti wa bodi ya Wakurugenzi wa benki hiyo,Jenerali mstaafu,Robert Mboma,Mkurugenzi Mtendaji wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC),Emmanuel Ole Naiko (mgeni rasmi) na kushoto ni Meneja mkuu wa benki hiyo,Imo Etuk.

*** *** *** ***

Benki ya UBA nchini Tanzania imeleta mwamko mkubwa wa kibiashara kutokana na kuanzishwa kwa huduma mpya mbili za kibenki zijulikanazo kama AfriCash na Afritrade. Huduma hizi za kipekee zimeletwa na Benki UBA Mahsusi kuboresha huduma za kibenki barani Afrika.

Huduma hizi mbili zimezinduliwa leo siku ya Jumatano Tarehe 27/10/2010, na zitasaidia kukuza zaidi huduma za benki ya UBA, ambazo sasa zimetapakaa katika nchi 19 barani Africa.

Akizindua huduma hizi, Afisa Mtendaji Mkuu wa benki ya UBA Tanzania Bwana Ayobola Abiola alisema hudama hizi zilianzishwa ili kupunguza matatizo katika ufanyaji wa biashara na malipo kwa urahisi zaidi.

Huduma ya Afritrade imeletwa mahsusi kwa ajili ya kuwawezesha wateja wa UBA kufanya malipo kwa urahisi kwa mlengwa bila tatizo lolote popote pale alipo katika Bara la Afrika.

Bwana Abiola alisema, “Mteja wa Afritrade atatakiwa kupata vibali kutoka ofisi za UBA, ili kuweza kutumia huduma hii,mteja atatakiwa kuonyesha mahali alipo mpokeaji na kielelezo kitatumwa kwa ujumbe mfupi kwa njia ya simu ya kiganjani au barua pepe.

Ujumbe wa maandishi utatumwa kwa mpokeaji mara moja ndani ya masaa 24 ukiambatanishwa na hati husika za malipo.Ili mpokeaji aweze kusafirisha mizigo, Hati zote za malipo vitakaguliwa na kuhakikiwa na wafanyakazi wa UBA na kukabidhiwa mpokeaji.Vielelezo vya uthibitisho vitatumwa kwenye ofisi za UBA alipo mpokeaji na ndani ya masaa 24 madai yate ya malipo yatakamilishwa”


Akiongelea faida ya huduma ya afritrade kwa wateja wa UBA ni pamoja na kupunguza gharama kwa wateja kwa kulipisha gharama naafuu ukilinganisha na gharama za zingine biashara, biashara kwa wakati ukiwa ndani ya Jumuiya ya Afrika mashariki (EAC), Jumuiya ya kiuchumi ya Afrika Magharibi (UEMOA) Umoja wa kiuchumi na fedha, na Jumuiya ya Fedha na Uchumi ya Afrika ya Kati (CEMAC), huduma zitapatikana kwa haraka zaidi ndani ya siku moja kupitia ofisi zetu UBA ambazo zimetapakaa barani kote Afrika na sio kupitia kwenye mgongo wa mabenki ya kimataifa na njia nyingine.

Akiiongelea huduma nyingine iliyotambulishwa ya “Africash” amesema huduma hii ya malipo ya kifedha inalenga watu binafsi na vikundi mbalimbali ndani ya Afrika ambavyo vimeongezeka kwa wingi ndani ya mwongo mmoja uliopita.

Amesisitiza kwamba huduma ya Africash iko katika nchi 19 ambazo UBA inaofisi ikiwa ni pamoja na Kenya, Ghana, Sierra Leone, Ivory Coast, Liberia, Cameroon, Uganda, Chad Burkina Faso, Senegal, Benin, Gabon, Guinea, Nigeria, Zambia, Tanzania, Msumbiji, Congo Brazzaville, Democratic Republic of Congo.

Mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi ya benki ya UBA Mh. Gen Robert Mboma amesema uzinduzi wa huduma hizi mpya unaonyesha jinsi gani UBA inajali kwa kuboresha huduma za kibenki katika bara la Afrika.

“Bara letu lina fursa nyingi za kibiashara baina ya nchi na nchi, kwa hiyo huduma hii itasaidia ukuaji na maendeleo kwa ujumla na ndio kitu tunataka kufanya kukuza biashara zetu”.

UBA ni moja ya taasisi za fedha zinazoongoza Afrika zinazotoa huduma mbalimbali za kifedha kwa wateja zaidi milioni 7.5 na ina matawi zaidi ya 850 ndani ya bara la Afrika.

Kuwepo kwa benki ya UBA katika miji ya New York, London, and Paris pamoja na miji mingine ya kifedha, unajumuisha uwelewa wa Afrika pamoja na wa nje kwa ujumla ili kuunganisha watu na biashara Afrika nzima na dunia kwa ujumla kupitia huduma za kibenki za wateja wodogo na wakubwa, kuwezesha malipo ya nje, mikopo ya biashara na uwezeshaji wa kibenki ndio maana unaifanya UBA kuwa chaguo la Waafrika na biashara zote zenye maudhui ya kiafrika ulimwenguni kote.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 1 mpaka sasa

  1. UBA 4 Africa, sio Stanchart wala CITI. Wadau Msiwe na wasi kwa kuwa inaongozwa na Wanigeria kwani si wote wasanii.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...