Mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akisalimiana na msanii wa kikundi cha burudani cha New Vission cha Mererani, Sifuni Justine(miaka 18), wakati alipowasili kwenye uwanja wa CCM Kata ya Endiamtu mji mdogo wa Mererani Wilaya ya Simanjiro, kufanya mkutano wa kampeni leo.
Msanii wa kikundi cha Burudani cha New Vission cha Mererani, Sifuni Justine (miaka 18), akicheza na kupeperusha kipeperushi cha Mgombea urais kwa tiketi ya CCM,Dr. Jakaya Kikwete, wakati wa mapokezi ya mgombea mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, alipowasili kwenye uwanja wa CCM katika Jimbo la Simanjiro kufanya mkutano wa kampeni leo.
Mgombea mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal, akipokea kadi ya mwanachama wa Chadema, Ernest Joanes, aliyejiengua katika chama hicho na kujiunga na CCM, sambamba na Wanachama 247 kutoka Vyama vya upinzani ambapo wote walikabidhiwa kadi za CCM wakati wa mkutano wa kampeni wa Dk. Bilal leo.
Sehemu ya wanachama wa vyama upinzani kati ya 247, wakinyoosha kadi zao za CCM wakati walipokuwa wakiapishwa baada ya kukabidhiwa kadi za CCM, waliporejesha kadi za vyama vyao kwa mgombea mwenza wa urais wa CCM, Dk Mohamed Gharib Bilal katika mkutano wa kampeni uliofanyika kwenye Uwanja wa CCM Mererani Wilaya ya Simanjiro Mkoa wa Manyara leo. Picha na Muhidin Sufiani

chama chetu cha mapinduuuuuuuuzi chajenga nchi, chai chapati marage mchuzi vyaaaaaaajenga mwili. kikweeeete aaaaah na shein wajenga nchi. dah bongo tumetoka mbali sana. hivi hadi leo ipo ile ukiona bendera inashushwa unasimama hata kama ulikuwa unawahi msalani? vipi kosa la uzembe na uzururaji?
ReplyDeletemdau ndani ya maisha utani
Kwa nini Serikali ya CCM isimsaidie huyu dogo anayeonyesha ni mkereketwa na mpenda chama kuliko wote "arefuke" awe kama wengine.Zimebaki siku mbili tupige kura kumpata rais wa awamu nyingine wa taifa letu kubwa la tanzania.Naiombea Amani na utulivu to my Great country in the world Tanzania.
ReplyDelete