Mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia) akisalimiana na Mgombea urais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, walipokutana uwanja wa Ndege wa Mwalimu Nyerere wa Jijini Dar es Salaam leo mchana wakati Dk. Shein, akiondoka kuelekea Visiwani Zanzibar na Dk. Bilal, akiwasili jijini kutoka Visiwani humo kwa ajili ya kufanya mkutano wa kampeni leo. Kulia ni ni mke wa Dk. Bilal, Bi Zakia Bilal.
Mgombea Mwenza wa urais kwa tiketi ya CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia) akizungumza na Mgombea urais wa Zanzibar kwa tiketi ya CCM, Dk. Ali Mohamed Shein, walipokutana uwanja wa Ndege wa J.K. Nyerere wa Jijini Dar es Salaam leo mchana wakati Dk. Shein, akiondoka kuelekea Visiwani Zanzibar na Dk. Bilal, akiwasili jijini kutoka Visiwani humo. Mgombea Mwenza wa urais wa CCM, Dk. Mohamed Gharib Bilal (kulia) akizungumza na Mgombea urais wa Zanzibar, Dk. Ali Mohamed Shein, walipokutana uwanja wa Ndege wa J.K. Nyerere wa Jijini Dar es Salaam leo mchana wakati Dk. Shein, akiondoka kuelekea Visiwani Zanzibar na Dk. Bilal, akiwasili jijini kutoka Visiwani humo. Kushoto ni mke wa Dk. Shein, Mama Mwanamema Shein, akizungumza na mke wa Dk. Bilal, Zakia Bilal.Picha na Muhidin Sufiani

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Mmekosea jina la maa Shein anaitwa Mwanamwema na siyo Tunu

    ReplyDelete
  2. Nkonongwa, MafiaOctober 27, 2010

    Uncle, mke wa Dk. Shein anaitwa Bi. Mwanamwema Shein na sio Tunu.
    Bi TUNU ni mke wa mtoto wa mkulima mwoga Bw. Mizengo Pinda

    ReplyDelete
  3. Ankali mke wa Dr. Shein anaitwa Mwanamwema na siyo Tunu

    ReplyDelete
  4. Wekeni CV ya mgombea-mweza wa Dr. Slaa, jamani! Hivi hamjui kuwa anaweza kuwa Rais endapo mabaya yatampata Slaa?

    Sijui jina lake!

    ReplyDelete
  5. nyie nao!!! wapeni pole kwa kazi ngumu ya kampeni. kwani kukosea jina kunasaidia nini au kunabadilisha kwamba wameshabadilishana hao wanawake?. yaani unapinda mngogo dakika tano kudonoa eti mke wa nani ni nani. BADILIKENI WATANZANIA. ala!

    ReplyDelete
  6. Watu weninge sijui mnashida gani, unaacha kujadili shida na adha zinazowasonga watanzania unaanza kung'ang'ania kuwa ooohh jina la mtu limekosewa, sasa kama limekosewa shida ni nini? unatakiwa kuwaza watanzania wenzako wanaolala kwa kula mhongo na maisha ya tabu. Fikiria suluhisho la jambo kama hilo. sawa eeh

    ReplyDelete
  7. nyie hapo juu mna akili kweli?? kukosea jina la mtu is a serious wrong na ni misconduct kwa mwandishi.hivi nyie mko dunia gani?si unaona wamemsaidia kabadili, nini jina, spelling tu katika jina inaweza kuleta tatizo, mtu anaweza hata kupelekwa mahakamani. alaah

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...