Tukiwa tunaelekea kwenye Uchaguzi Mkuu Tanzania ambao utafanyika October 31, 2010, Watanzania wazalendo wanachama na wapenzi wa Chadema mnaombwa kuchangia kwa dhati harakati za Chadema ili tuweze kuwafikia Wananchi wengi zaidi katika kila kona ya Tanzania tukitafuta ridhaa yenu ya kuweza kujenga nchi yetu; nchi yenye usawa, uzalendo, maadili na uwajibikaji katika miaka mitano ijayo.

CHANGIA CHADEMA KUPITIA BANK:
CRDB BANK
CHADEMA - M4C
Account Number: 0J1080100600

National Microfinance Bank [NMB]
CHADEMA
Account Number: 2266600140

Unaweza kuweka pesa kupitia tawi lolote la Benki hizi Tanzania.


CHANGIA CHADEMA KUPITIA SMS (MESEJI):
Tuma neno:

"CHADEMA" kwenda namba 15710
"NAJIUNGA" kwenda namba 15710
"SLAA" kwenda namba 15710

Unaweza kutuma meseji mara nyingi kadri unavyoweza na kila ujumbe utagharimu TZS 350/= tu.
HII NI KWA MITANDAO YA ZAIN, TIGO NA VODACOM TU.

CHANGIA KUPITIA M-PESA:
Kwa watakaotaka kuchangia kwa M-Pesa wanaweza kutumia namba zifuatazo:
0758 223 344
0764 776 673

CHANGIA KUPITIA ZAP:
Kwa watakaotaka kuchangia kwa ZAP wanaweza kutumia namba hii:

0789 555 333

"Ndugu Zangu Watanzania, tunawaomba kwa dhati kabisa tushikamane, tushirikiane bila kujali itikadi zetu kuchangia harakati hizi, tunawashukuru sana. - Dr. Wilbroad Peter Slaa"

CHAGUA MABADILIKO YA KWELI.
CHAGUA CHADEMA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Cha wajinga huliwa na matapeli. Siwachangii ng'oo. Badala yake napeleka milioni mbili CCM leo.

    ReplyDelete
  2. Annonmous. Nakubaliana na wewe. Mimi na wenzangu tumeishapeleka USD 10000! SItanii naapa kuwa kweli tumepeleka. Muulizeni Slaa kwanini asiwaombe KAVIWASU Karatu na KAKOBE wamchangie.

    ReplyDelete
  3. nimeshachangia asbh hii kwa ZAP....
    MAONI: naomba mhusika utumie nick name CHADEMA badala ya kuacha namba kama ilivyo....ili kuonyesha kuwa nimetuma kunakotakiwa,nikipata reply kuwa umetuma pesa kwenda CHADEMA inasound vyema zaidi....wakati huohuo mimi naforward information hii kwa watu wengine ili kuproove watataka feedback hiyo ya neno CHADEMA.....
    pamoja mpaka kieleweke!!!

    ReplyDelete
  4. hii account ya crdb iko sawa kweli hii? 0J1080100600 naada ya 0 ya mwanzo haifati 1 au?
    na zinaingia ofisi ya uhasibu au kwa nani?

    ReplyDelete
  5. Huna Fedha wewe!

    ReplyDelete
  6. MIMI NITACHANGIA KWA AJILI YA UKOMBOZI. HATA NYERERE ALICHANGIA UKOMBOZI WA NCHI ZA AFRIKA.

    ReplyDelete
  7. Mzee Ndesa amefulia au.....mara mnataka michango...sisi tulipoomba michango mlituitaje? Mabadiliko ya kweli mi yale endelevu, yenye misingi tayari...na CCM tumeshaweka misingi tunasonga mbele...

    ReplyDelete
  8. wewe mchangia mada wa kwanza nikukumbushe kuwa Chadema hawapokei fedha za wizi kwa hiyo usisumbuke kueleza hapo kuwa unapeleka wapi wewe peleka pale wezi wenzio wanapokea

    ReplyDelete
  9. nani achangie,alafu hela mkajenge moshi,sahauni,labda nccr au cuf nitachangia lakini sio chadema.

    ReplyDelete
  10. Anony wa2:12 pm, Nani kasema chadema hawapokei hela za wizi. Unaishi dunia gani ndugu yangu?

    ReplyDelete
  11. Mwaka jana ruzuku ya Chadema walipata milioni 818; mwaka huu wamepata milioni 750; kada wa CCM Sabodo kawachangia milioni 100 na bado michango kibao kutoka kwa wanachama ndani na nje ya nchi, kuna watu wanawachangia mamilioni kila siku. Hizi pesa zimeenda wapi wakati Chadema ofisi hamna, hata gari hamjanunua?Na helikopta mnayotumia ni ya Ndesamburo kajitolea bure sana sana ni mafuta tu ndiyo mnanunua?

    Isitoshe wagombea Ubunge na Udiwani wa Chadema ambao si WACHAGA walioko vijijini sehemu mbali mbali Tanzania wanalia ukata mmeshindwa kuwanunulia hata baiskeli, je mapesa yote mmepeleka wapi?

    Waibieni hap hao wajinga wasiotaka kujua mapato na matumizi hakuna cha demokrasia bali ni DOMOKRASIA, Kuchangia ulaji tu kwa watu wachache.

    Halafu mnakumbuka shuka wakati kumeshakucha?

    ReplyDelete
  12. Cirrus mahimbiOctober 05, 2010

    Jaman kugombea urais maandalizi mgombea amekurupuka hata mke alikuwa hana kapora wa wa2 2mesema 2kae kimya sasa na pesa tena ili akalipe hlo deni kwa bwana mahimbo? Kwa kweli 2nahtaji mabadiliko ila co yakuzidi kutiana umaskini mke upewe,pesa unataka msaada na kura 2kupe ce 2baki na nini? Hapana chadema kajipangeni mpaka uchaguzi ujao... asante michuzi

    ReplyDelete
  13. Chadema kudai "mabadiliko ya kweli" ni uongo mkubwa!

    Kamwe, hakuna mabadiliko ya kweli!

    Wanafunzi wa siasa (husasan wanaosomea "political propaganda") mmpata mfano mzuri wa kuweza kuchambua vigezo vya "political propaganda"!

    ReplyDelete
  14. eheeee kumbe mnataka mkamalizie ile barabara ya rombo mwika no no mlizonazo zinatosha hamna hela hapa sasa hivi tunaangalia zile sehem ambazo hazina kabisa ndio tunachangia, nyerere wa juwabeba safari hii hayupo, tunampa huyo MKWERE akimaliza kujenga kwao, next time sisiem tena tunampa mwakyusa nae akajenge kidogo huko kwao kyela tukuyu nk . then baada ya hapo tunatafuta wa kigoma mkapa kisha jenga kwao lile daraja kubwa la kihistoria so 2025 tunahamia kiggoma naona hao kidogo wamesahaulika so may be wachaga tena itakua 2045 ndio tunaweza kuwafikiri, maana naona moshi sasa hivi imechakaa kama kigoma hahahaha!!!!!!!anyway see u in 2045
    thanks mboni na shicha

    ReplyDelete
  15. Nyie CCm na Tano yenu mmetawara miaka hamsini na wananchi bado masikini. si afazari wajaribu chama kingine chenye mwelekeo nacho ni CHADEMA.

    ReplyDelete
  16. Mchangieni atese na bibi Josephine..leo unaomba sisi walalahoi pesa za kuingia ikulu?, mkipada madaraka mnasahau mara moja..sitoi hata shilingi moja, kwa jambo gani la maana mnaloweza fanya?? Siwezi kumchangia mzinzi hasiye na haya..

    ReplyDelete
  17. Mimi nimetoka chadema na kurudi CCM wiki mbili tu zilizopita. Swali langu ni: Je zile shilingi bilioni mbili na nusu chadema walizoanza nazo kampeni tarehe 1 Septemba zimeyeyukia wapi baada ya wiki tano tu? Lesson one: chadema jifunzeni "ku-balance the budget" katika chama chenu kabla ya kutoa ahadi zisizotekelezeka za bajeti ya matumizi ya shilingi trilioni 22 kwa miaka mitatu ya mwanzo! Na ndiyo maana chadema kitashindwa. Njia ya mwongo fupi.

    ReplyDelete
  18. wajinga kweli waliwao,kitugani kinawafanya mfikiri kuwa hawa CHADEMA kweli wanauchungu na nchi hii na kwamba wakiingia madarakani wataleta maendeleo kwa Mtanzania?Waliona mgombea walokuwa wanamnadi kwenye chaguzi zilizopita hakubaliki,hata wafanyakazi wake anashindwa kuwalipa mishahara wakaona wamuweke Slaa!hatudanganyiki!humohumo ndani mnapigana wachaga kwa wachaga,mnawaza pesa tu!nani awachangie!!!Mtanzania fungua macho,acha kubabaishwa na mbwembwe za kisiasa,mchaga siku zote anatafuta pesa tu hana shida na maendeleo yako!!MWENYE MASIKIO NA ASIKIE.

    ReplyDelete
  19. Ni kweli hawa chadema hawaoni mbali, wenzao sisiem waliona mbali toka zamani na wakaanzisha kampeni ya michango mapema kwani walijua kuwa kila kitu ni maandalizi mazuri kwa ajili kupata kitu kizuri. hata ukitaka kuoa lazima ijiandae mapema usisubiri mwishoni ndio uanze kuhaha patakuwa hapatoshi!? na sasa chadema hapatoshi, kumekucha ndo wanakumbuka shuka ikowapi?!!!!!!!!!!!!!!! ukizingatia kwamba sasa hivi hela imekua ngumu kupatikana.

    mbali na hayo pia wakati wenzao sisiem wanaanzisha harambee walisema mengi sana lakini sisiem hawakujali waliziba masikio na kusonga mbele kwani walijua nini wanakifanya sasa leo kwao nao pia wamefuata mkondo wa MZAZI WAO (CCM). mie nilijua wao (chadema)sio omba omba kama sisiem kumbe na wao wamo du!!!! makubwa!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...