Mgeni rasmi, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Muhammed Seif Khatib akibandika stika kwenye ramani ya Tanzania kuashiria kuwa kampeni kubwa ya kuhamasisha watanzania waweze kujitokeza kwa wingi kuishangilia timu ya taifa katika mchezo wake muhimu dhidi ya timu ya timu ya Taifa ya Morocco hapo jumamosi,Oktoba 9 2010 imezinduliwa rasmi.kati ni Meneja Mkuu wa Uhusiano, mawasiliano na Jamii kutoka kampuni ya bia ya Serengeti Dada Teddy na Rais wa TFF, Leodga Tenga wakishuhudia tukio hilo mchana huu.
Rais wa TFF,Leodga Tenga akitoa ufafanuzi kuhusiana na kiingilio cha mchezo huo utakaofanyika siku ya jumamosi,mbali ya hiyo Tenga amewahimiza wananchi kujitokeza kwa wingi katika mchezo huo na kuwapa moyo wachezaji wa timu ya Taifa na hatimaye kushinda.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. huyu jamaa alikuwa the most beutiful defender to watch mkimweka na mohamed tall bakari, jella mtagwa jamaa wa west africa kama vile nigeria,ghana walikuwa hawaoni goli, golden era of soccer on TZ

    ReplyDelete
  2. Enzi za huyu cool defender na wenzake kwenye late 70's ilikuwa balaa. Wee uliza AS VITA ya DRC ya akina Mayanga, Ibadan Shooting stars ya Nigeria ya akina segun odegbani, Marehemu Mudashiru Lawal waliona cha moto.
    Ukweli ni kwamba Mr. Tenga akitaka kitu anazingatia sana malengo, bidii na nidhamu ya hali ya juu hivyo lazima afanikishe lengo lake kwa kiwango cha juu. Sii Mtu wa mzaha anapotaka kufanikisha azma yake.

    Naomba sana wachezaji wetu wawe wanazingatia anayowaasa wataona matunda yake.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...