Habari Kaka Michuzi,
Naomba unitundikie hiki kichefuchefu ili wadau wa Globu ya Jamii waweze kuij
adili kidogo maana hii hali imekithiri sana hapa mjini.
Watu wengi wanapenda kuvaa mtindo wa carwash!!! na kutembea mabarabarani. Kupanda daladala hapa mjini hili ni tatizo sugu, wakati umefika sasa wadau tuanze kukemea jambo hili.
Na hasa wakikosa siti, aibu inakuja pale wanaposhika bomba!! ni (KICHEFUCHEFU) utaona kwapa ni chafu,manyoya yameganda na jasho,harufu tupu mengine siyasemi. Je? watu kama hawa wengine ni wababa na wamama, wengine ni wasichana warembo kabisaaa, wavulana ndio usiseme wakitoka kwenye mishughuriko yao ni hatari hiyo,kuvaa mavazi hayo mbele ya kadamnasi
ni ungwana kweli?
KAZI HII NAWAACHIA WADAU WA GLOBU YA JAMII
Mdau aliekerwa na tabi hii.
Naomba unitundikie hiki kichefuchefu ili wadau wa Globu ya Jamii waweze kuij

Watu wengi wanapenda kuvaa mtindo wa carwash!!! na kutembea mabarabarani. Kupanda daladala hapa mjini hili ni tatizo sugu, wakati umefika sasa wadau tuanze kukemea jambo hili.
Na hasa wakikosa siti, aibu inakuja pale wanaposhika bomba!! ni (KICHEFUCHEFU) utaona kwapa ni chafu,manyoya yameganda na jasho,harufu tupu mengine siyasemi. Je? watu kama hawa wengine ni wababa na wamama, wengine ni wasichana warembo kabisaaa, wavulana ndio usiseme wakitoka kwenye mishughuriko yao ni hatari hiyo,kuvaa mavazi hayo mbele ya kadamnasi
ni ungwana kweli?
KAZI HII NAWAACHIA WADAU WA GLOBU YA JAMII
Mdau aliekerwa na tabi hii.
Hiyo ni kero mpaka huku Marekani. Huku mtu akivaa hivyo, baadhi ya maenea hawezi kuingia, kwa mfano benki nyingi na hata restaurants haziruhusu watu kuingia. Waambie angalau watumie deodorant kuondoa harufu.
ReplyDeletemichuzi ndo uvaaga hivyo akitoa ze fulanazzz au yule nabii marehemu yohana mashaka. naye pia. waambie wakaoge
ReplyDeleteMoja kati ya sababu zinazochelewesha maendeleo ya Tanzania ni tabia ya kufuatilia mtu kavaa nini. Kama muda huo tungeutumia kwa shughuli za maendeleo tungekuwa mbali sana.Tunatumia muda mwingi kufuatilia mambo ambayo hayatuhusu. Kama mtu kavaa nguo mbaya au nzuri wewe inakuhusu nini?Huyo ni mtu mzima anaelewa anachokofanya na ana uhuru wa kuvaa anchopenda kulingana na uwezo wake. Mbona wamasaai wanavaa lubega, au mababu zetu wa asili walivaa majani kufunika sehemu za siri na waliishi vizuri tu kabla ya wageni kuingia Afrika. Kama jambo halikuhusu achana nalo. Unapoteza muda wako bure ambao ungetumika kufanya mambo mengine ya maendeleo.
ReplyDeletemdau uliyetuma article acha hizo tanzania ni nchi huru mtu anatoka na pamba anazotaka yeye kama wewe unaona karaha basi nunua gari lako acha kutumia public transport
ReplyDeletenjia muafaka ya kukomesha tabia kama hiyo tulitakiwa tanzania tuwe na msimu wa winter kali kama huko usa na canada joto linapokuwa NEGATIVE automatically hakuna kwapa nje kwani unatoka nje asubuhi unakuta nyumba imefunikwa na barafu hapo no mjadala bro
ReplyDeletemarekani ya wapi hiyo wanayokataza wanaopangia watu mavazi ya kuendea benki, au Alaska? ACHA URONGO!!!
ReplyDeleteJamanin haya mambo ya kuifananisha TZ na USA haifai. Huku vijijini sisi tumezoea watoto wetu wanacheza poa tu bila kaptula wala hatushtuki na huko pwani wamama kuvaa nusu Kanga ni kawaida. Kama hampendi hizo tabia huko mjini wanunulieni mashati nasikia mjini maisha magumu unaweza kuta hana fedha za kununua nguo nzuri zaidi ya hapo.
ReplyDeleteWhen we grow up, we leave them…only come to them when we need something or when we are in trouble.
ReplyDeleteNo matter what,
parents will always be there and
give everything they could
just to make you happy.
You may think the boy is cruel to the tree, but that is how all of us treat our parents.
We take them for granted we don't appreciate all they do for us, UNTIL it's too late.
May Allah forgive us of our shortcomings and may He Guide us,
Insha'allah Ameen.
Love & Honour your Parents
And your Lord has decreed that you worship none but Him. And that you be dutiful to your parents. If one of them or both of them attain old age in your life, say not to them a word of disrespect, nor shout at them but address them in terms of honour.
And lower unto them the wing of submission and humility through mercy, and say: "My Lord! Bestow on them Your Mercy as they did bring me up when I was small."
"Rasulullah (Sallallaahu Álayhi Wasallam )said that Jabreel said that"Woe unto him in whose presence his parents or either one of them attains old age, and (through failure to serve them) he is not allowed to enter 'Jannah". To this Rasulullah(Sallallahu Alayhe wassallam) said Ameen!
Hatukatazi mtu kuvaa apendavyo ila uvae usiwakere wengine.Nyie mnaotetea ni miongoni mwao na hoja imewauma.Hakuna mtu anayependa harufu mbaya ya mwenzake.Kwa wengine ni ukosefu wa utashi na kujitambua
ReplyDeleteHuyu jamaa msimlaumu nahisi kinamchomkera ni nywele za kwapani hajui hizo ni kachumbali ktk mapezi naona yeye hakubarikiwa kuwa nazo mpeni pole maana amekosa kitu cha MUHIMU SANA.
ReplyDeleteBaadhi za Hekima na Methali za Kiarabu
ReplyDelete1) Si vigumu kujitolea kwa kumsaidia rafiki yako,lakini ni vigumu kupata rafiki ajitolee kwa ajili yako.
2) Usiache ulimi wako ukafuata macho yako kwa kueleza aibu za watu, kumbuka kuwa watu nao wana macho na ulimi kama wewe.
3) Mambo yasiyokuwa na umuhimu huzungumzwa kwa muda mrefu kwani sote tuna yafahamu kuliko mambo muhimu.
4) Ikiwa una mikate miwili kula mmoja na mwingine utowe sadaka.
5) Mtu akisifiwa watu wachache huamini,lakini akikashifiwa wengi huamini.
6) Hakuna mtu ambaye hakufanikiwa kabisa,bali ameanzia na sifuri akabakia hapohapo.
7) Binaadamu ambaye amefaulu ni yule anaye nyamaza kabla ya watu hawaja ziba masikio yao, na anafunguwa masikio yake kabla ya watu hawajafunguwa midomo yao.
8) Kabla ya kuzungumza chaguwa neno la kusema, na uchukuwe muda wa kusema ili maneno yako yachipuwe kama linavyo chipuwa tunda.
9) Jihadhari na mtu ambaye ni mkarimu ukimdharau,na mtu mbaya ukimkarimu,na mwenye akili ukimkosowa na mjinga ukimrehemu.
10) Ukifikia kilele mwangalie jambazi ili upate mtu wa kukusaidia,na angalia mbinguni ili Mwenyeezi Mungu akuweke imara usianguke.
11) Si kufaulu kugunduwa mambo wanayo yapenda watu,lakini kufaulu ni kuwa na ujuzi wa kuwafanya watu wakakupenda.
12) Shujaa anaye jitahidi kutatuwa matatizo yake,anafaidika na uwezo wake
13) Ukipanda jabali angalia kilele chake,wala usiangalie upande wowote na ulipande kwa makini,wala usiruke ukavunja mguu wako.
14) Shujaa ni yule ambaye anauwezo wa kukuza ujuzi wake,na kuweza kukuza ujuzi wa watu na pengine kuwabadilisha.
15) Usiache utajiri ukakufanya ukakosana na watu,kwani kuwa pamoja na watu ndio njia ya kuupata utajiri.
16) Badali ya kukaa na kutukana kiza,jaribu kutengeneza umeme.
17) Ukitabasamu tabasamu kwa mtu masikini, kwani kunakuongezea malipo mema kwa Mwenyeezi Mungu.
18) Mwanamke humsubiria mume wake kwa umasikini wake,ubaya wake na kutokumjali kwake ,lakini hamsubirii kwa tabia mbaya yake.
19) Mtoto ni kama udongo(wa ufinyanzi) tuna mlea kwa jinsi tunavyo ona sisi.
20) Watendee watu kama wao ni binaadamu si kwa sura zao wala pesa zao wala vyeo vyao.
21) Uzuri wa mtu ni ndani ya nafsi yake,si sura yake.
22) Ukisema neno litakumiliki,na usipolisema utalimiliki.
23) Anaye ishi na sura mbili,hufa bila ya sura
24) Adui yako akikuomba ushauri mpe nasiha,kwani ukimpa ushauri ataondosha uadui wake kwako na kukusaidia.
25) Ukizungumza wakati ukiwa na hasira,utasema neno ambalo utajutia maisha yako.
26) Usijadiliane na mtu mjeuri wala asiyekuwa na haya, kwani jeuri hutomuweza na asiye na haya atakuudhi.
27) Tabia njema ina sitiri mambo mengi mabaya,na tabia mbaya ina ziba mambo mengi mazuri.
28) Mwenye kumuamini Mwenyeezi Mungu humpa,mwenye kutawakal kwake humtosha,mwenye kumuogopa huacha aliyo yakataza na mwenye kumjuwa humuenzi.
29) Kunyamaza ni dalili ya kukubali jambo.
30) Jihadhari na ulimi wako,usiiponze shingo yako.
31) Fimbo ya muongo ni fupi.
32) Si kila wakati mtu husalimika na jirani.
33) Ulimi wako ni kama farasi wako,ukiuchunga vizuri nao utakuchunga na ukiuachia nao utakuponza.
34) Ndege mmoja aliye mkononi mwako ni bora,kuliko kumi waliyoko katika mti.
35) Kila kimya kina jambo lake.
36) Ukitaka kutiiwa,amrisha mambo yanayo weza kufanywa.
37) Wezi wawili wakigo mbana ,vitajulikana vitu vilivyo ibwa.
38) Jihadhari na shari hata kwa mtu uliye mfanyia mema.
39) Upanga umeshinda kanuni.
40) Mwanzo wa mavuno ni tone la mvuwa.
AHsante ankali kwa nafasi ya maoni. Kwa kifupi tuwe wasafi tusiwakere wengine. Sina sababu ya kuhukumu umevaa nini. kama huna aibu walimwengu watakupa vidonge vyako. ni hayo tu ankali.
ReplyDelete'Smartness knows no weather!'
michuzi..., mada za kibwegebwege kama hizi usituwekee kwenye blog yetu.
ReplyDeletenafikiri kama watu wakiwa wasafi na kunyoa nywele vizuri, pulizia perfume au km hauna uwezo hakikisha umenawa vizuri na sabuni kabla ya safari yoyote.
ReplyDeletejamani ni vizuri kuambiana, kwani maana ya Kitchen party ni nini, sikufundishana wanawake? sasa nafikiri na wanaume nao wawe wanapewa mafunzo fulani ama ndo maana vikwapa hivyooo. wanawake wengi siku hizi wameelimika k'sababu ya K parties, lkn wanaume ni baaado sana kwa kweli, nashauri wanaume nao wawe wanapewa mafunzo jamani, kwanza ni wagumu mno na wengi wanafikiri majukumu ya nyumba ni wanawake tu.
ebwana we kama huwezi chukua texsi usitupigie kelele humu na wewe mdau wa marekani ambaye ukiwa mchafu huwezi ingia restaurant ni muongo unaweza ukawa restaurant akaja fundi garage akastua anachokitaka ila sema tu hawezi kukaa ila cio kama anakatazwa kuingia acha uongo wote tuko marekani labda wewe uko mbagala unajifanya marekani mdau wa madison,wi
ReplyDeleteNazungumzia tank tops, nyie waswahili mnaziita "car wash", haziruhusiwi kuuingia nzao bank au restaurant Marekani. Uliza uambiwe.
ReplyDeletewatanzania ni wabishi sana, waongeaji sana na wanaojifanya kuwa maisha wameyapatia, kumbe hamna lolote nchi yenyewe haina mbele wala nyuma sasa mnatetea nini upuuzi mtupu ndo maana mtaishia nafasi ya ...... kutoka mwisho kwa nchi zilizo maskini duniani kwa upuuzi wenu na ubishi kwa kutaka kujiliganisha na nchi ambazo ziko mbele kwenu x......
ReplyDelete..."Moja kati ya sababu zinazochelewesha maendeleo ya Tanzania ni tabia ya kufuatilia mtu kavaa nini. Kama muda huo tungeutumia kwa shughuli za maendeleo tungekuwa mbali sana.Tunatumia muda mwingi kufuatilia mambo ambayo hayatuhusu. Kama mtu kavaa nguo mbaya au nzuri wewe inakuhusu nini?Huyo ni mtu mzima anaelewa anachokofanya na ana uhuru wa kuvaa anchopenda kulingana na uwezo wake. Mbona wamasaai wanavaa lubega, au mababu zetu wa asili walivaa majani kufunika sehemu za siri na waliishi vizuri tu kabla ya wageni kuingia Afrika. Kama jambo halikuhusu achana nalo. Unapoteza muda wako bure ambao ungetumika kufanya mambo mengine ya maendeleo...".
ReplyDeletehivi msg hii inafundisha nini? kwani kunuka kwapa nako ni maendeleo? suala si uvaaji bali ni namna vazi hilo linavyoleta kero, usafi ndo maendeleoooooooooo