Wilson Elisha Khambaku akiongea kwa hisia kwenye mkutano wa kampeni Ikungi kuhusu siku 29 alizokaa Chadema baada ya kuanguka kwenye mchakato wa CCM.
Wilson Elisha Khambaku akiongea na wana Ikungi katika mkutano wa kampeni.

====================

  • Alikaa Chadema siku 29
  • Atoa siri, Chadema hakuna sera
  • Wapinzani zaidi ya 50 warudi CCM
  • Wasanii watoa buradani ya kishindo

Aliyeshindwa kura za maoni jimbo la Singida Magharibi na kuhamia Chadema kwa siku 29, Bwana Wilson Elisha Khambaku, ameeleza kilichomsibu akiwa kwenye chama hicho pinzani.

Akitoa ushuhuda kwenye mikutano ya kampeni Puma na Ikungi, Khambaku alikiri kughafilika na kukimbilia upinzani baada ya kuanguka kwenye kura za maoni.

Akishangiliwa na umati wa watu pale aliposema kwamba aliomba sera za Chadema kwa wiki moja bila mafanikio na hatimaye kushindwa kupata muelekeo wa chama hicho kwa ajili ya kampeni.

Alisema chama hicho ni matapeli kwani baada ya kumzungusha wiki mbili walimpa sera za matusi na kubeza mafanikio thabiti ya CCM.

Akiongelea mafanikio ya CCM kwenye upanuzi wa elimu ambapo hata Umoja wa Mataifa umetambua na kuipa Tanzania tuzo ya kukidhi malengo ya milenia kwenye upande wa elimu kwa asilimia 95.

Akizungumza kwa hisia kubwa, Khambaku alisema siku 29 alizokaa Chadema zilikuwa za mateso na upweke mkubwa, akizifananisha na nyumba yenye kunguni na chawa ambazo humuwasha mtu anayelala kwenye malazi yake.

Amesema sababu kubwa zilizomfanya yeye kurudi CCM ni amani na utulivu iliyodumishwa na CCM tangu uhuru hadi leo. Amewasihi wananchi wa Singida wasifanye makosa ya kuchagua upinzani, ni wasanii, wana chuki na wanabeza hata mafanikio halali ya CCM.

"Mwisho nawasihi msifanye makosa niliyofanya mimi, msihangaike na wapinzani. Hawana sera hao, nimejionea mwenyewe! Naomba mchague chama madhubuti, CCM"

Alimaliza Khambaku huku akishangiliwa na umati mkubwa wa watu.

Na kwenye mkutano wa kampeni wa Ikungi, wapinzani zaidi ya 50 kutoka Chadema na CUF walirudisha kadi zao na kuingia CCM.

Aliyehama kutoka Chadema, alitoa ushuhuda kwa kusema alipochukua kadi ya Chadema aliambiwa kwamba yeye ni mwenyekiti.

"Nikawauliza mwenyekiti wa nini, wakasema wa kijiji hiki. Nikawahoji nani kanichagua? na ninamuongoza nani? Sikupewa jibu, sasa narudi CCM" Alisema Mzee huyo akishangiliwa na umati wa watu.

Nao wasanii wa muziki hawakuwa nyuma kwenye kutoa hamasa kwenye mkutano huo. Mwanamuziki Flora Mbasha akisindikizwa na wanamuziki wengine mashuhuri Ray C na Bushoke walitoa hamasa kubwa kwa wananchi wa Ikungi waliohudhuria kwa wingi mkutano huo wa kampeni.

Naye mshairi maarufu kutokea hapa Singida alitumbuiza kwa shairi lake lililomshukuru Mheshimiwa Kikwete kwa kuleta wilaya mpya ili kusogeza shughuli za maendeleo karibu na wananchi.

Mshairi huyo alisifia umahiri wa Chama Cha Mapinduzi haswa kuwatayarisha viongozi wa nchi na utawala mzima wa chama. Alisema kutoka umoja wa vijana kuna jumuiya ya wazazi na wanawake ambazo zote zinalenga kuwalea wana CCM kuongoza chama na nchi. Alihoji wapinzani wanapikwa namna hiyo hadi kutaka kugombea uongozi wa juu wa nchi?

Akishangiliwa na umati wa watu, mshairi huyo alisihi pia kudumisha amani na mshikamano haswa kipindi cha uchaguzi. Aliwasihi wana Singida kujitokeza kwa wingi kupiga kura ili mkoa uongoze kwenye kura nyingi kwa wagombea wote wa CCM.

Kabla ya Mkutano wa Ikungi - Singida Mashariki, Mheshimiwa Kikwete alifanya mkutano wa kampeni Puma Singida Magharibi ambapo mgombea ubunge wa jimbo hilo Mohamed Missanga alimshukuru Mheshimiwa Kikwete kwa kuwapatia wilaya mpya na jimbo jipya la uchaguzi.

Baada ya hapa, msafara wa Mheshimiwa Kikwete utaelekea Itigi, Manyoni, Kitinku na hatimaye Dodoma Mjini kwa mkutano wa mwisho wa kampeni kwa siku ya leo.

kwa habari hizi na zingine nyingi katika kampeni ya JK

BOFYA HAPA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. Jamani huo ni unafiki, tena amwogope na Mungu, angepita hizo kura za maoni kupitia Chadema angerudi CCM? Naona watu wanatufuta ulaji kwa njia yoyote!! Na akikosa CCM atahamia CUF...!!! natumaini wananchi wanasikiliza hotuba za mwl. Nyerere, wasije wakachagua bora viongozi.

    ReplyDelete
  2. We Elisha rudi darasani kwanza - Kamalizie LLB yako OUT. Siasa waachie akina Tundu Lisu.

    ReplyDelete
  3. Umeona huwezi kuiba CHADEMA ndo maana umeamia CCM kwa mafisadi waliobobea. Fisadi Mkubwa weeeeeeeee.

    Mdau USA

    ReplyDelete
  4. Hana lolote huyu anatafuta huruma ya kugawiwa japo ka ukuu wa wilaya. Wilaya zenyewe chache, walioanguka ndani ya chama wapo kibao tena wenye profle nene na wanahistoria ndefu ya kukitumikia chama kwa uaminifu na uadilifu tena kwa muda mrefu na wewe profile yako ni ndogo sana. Pasipo wewe kujijua utapewa muda wa matazamio wa miaka kumi hivi ili uangaliwe kama hutahama tena na kwenda kuropoka badala ya kujenga hoja. Ingawa mtu anahaki ya kuhama lakini hapo umechemka bro! Sababu zako haziniingii akilini

    ReplyDelete
  5. TRAITOR IS A TRAITOR!!MSALITI NI MSALITI TU!!
    WANA CCM INABIDI TUWE MACHO NA MTU HUYU.IPO SIKU ATATUSALITI PIA.Hatakiwi kuaminiwa kwenye dili yeyote ile.....

    ReplyDelete
  6. Mtu mzima unapanda jukwaani na kusema CHADEMA hakuna sera, hivi ni kweli CHADEMA hakuna sera? Kama wana sera sasa wewe unayesema hawana sera si unaonekana tu umepungukiwa na vitu fulani kwenye akili yako.

    ReplyDelete
  7. MICHUZI KWA TAARIFA YAKO, WATU WENGI WANAFUATILIA GLOB HII NI WATU WASOMI NA WENGI WAO WANAELEWA KINACHOENDELEA NCHI NA WAHAFURAHII HALI ILIVYO. KWA HIYO UNAVYOWEKA HABARI ZA MTU ANASEMA CHAMA FULANI HAKINA SERA WAKATI SI KWELI WEWE MICHUZI UNASHUSHA BLOG YAKO CHINI.

    ReplyDelete
  8. Ametumwa tu huyo, kama majini ya nanihii.

    ReplyDelete
  9. Baba mwomba kibaba amefanya kazi nzuri sana kuomba kura nchini.

    ReplyDelete
  10. Mr. Khambaku must be true to himself first before he goes before his possible voters and show emotion. He is thinking of what will he do if he lose the election and that is why he gets emotional. Nothing more!

    ReplyDelete
  11. naona michuzi umeanza tena kutuaalibia hewa na watu wako uchoki na habari zako za upande mmoja mbona ujawauliza chadema kama kweli hawana sera maana wewe unajifanya blog jamani kwa kutembea na kikwete kila mahali kweli kampeni lakini cuf na chadema huna mpango nao au jamii una maana ccm
    habari za maji taka hizi

    ReplyDelete
  12. mimi nafiri vyeo kama mkuu wa mkoa na mkuu wa wilaya vingefutwa kwani watu hawa ndio wanajifanya kurudi ccm ili wapatiwe vyeo hivyo,ni bora RAS & DAS wakapewa hata hayo majukumu wanayofanya hawa rc&DC

    ReplyDelete
  13. njaa tu kaka inakusumbua!! usidhani wote tuna uwezo mdogo wa kufikri kama wewe. sisi tutaipigia kura Chadema no matter how. afterall ur just tiny object to grab our mind. go to hell u idiot

    ReplyDelete
  14. Hivi wewe michuzi huna aibu kutundika kila mda maneno yanayoudhi upande flani?Kwasababu mimi sikuelewi hata kidogo.Au blog umeshaigeuza chama flani!samahani kama silijui hilo,kwasababu unajuuua vizuli blog yako sio chama flani lakini kama hii habali ya huyu bwana hatukuelewi hata kidogo maana yake!! au na wewe unakubaliana naye kwamba Chadema haina sera ??Blog hii inaongozwa na wewe lakini bila sisi haitapendeza,,jitahidi sasa habali kama hizi uziweke ukiwa umeziangalia kama hazitaudhi upande flani hapa ndani.

    ReplyDelete
  15. Kwanza wewe Michuzi ni CCM sikupendi maana hauweki habari za CHADEMA kwanini CCM imesha tosha sisi hatujaribu tinafanya kweli naomba hii ijulikane hivyo na hawa najeshi wanyamaze Tanzania ni nchi ya amani ila kama CCM wataiba kura kama walivyozoea hatutakubali patachimbika
    Tanawakae wakijua kama hatuwaogopi hatakidogo alafu wewe michzi CHADEMA ikishinda ujue chakwnza ni kuifungia hii blog yako maana mbona ya chadema imefungwa sasa subiri

    ReplyDelete
  16. Jamani watanzania wenzangu siasa ni sera ndio maana hata hivi vyama vikakubaliwa kuingia kwenye kinyanganyiro hakuna chama kisicho na sera, kama hukuzipenda wewe basi ulienda kufanya nini kama sio kwamba ulitumwa na walikuona sio mwaminifu ndio maana hawakukupa siri zote yaani umekaa siku ishirini tu ulitaka uwe kama mbowe mwenyekiti. watu wa hivi kama ccm wanawakumbatia basi waliwatuma kufanya hivyo kama sio ni hatari sana hata kwa maendeleo ya nchi
    sisi tunataka hata kama chadema anashinda basi asibweteke upinzani ni chachu ya maendeleo sasa kama hakuna upinzani kura za nini.
    kama chadema hawana sera nani kawaruhusu kuingia kwenye kugombea.

    ReplyDelete
  17. Hivi huyu jamaa amekwenda darasa mbali na kusikia anasoma LLB hapo OUT na kama ni akili hiyo hataiweza. Michuzi wewe ni mwandishi wa habari, unajua Chadema wana website yao, yeye kweli kama kaenda darasani anaweza kufungua website akakukta sera, katiba, ilani ya uchaguzi kila kitu kipo. Halafu fikiria mtu anakakosa ubunge nakimbilia Chadema, uko nako waliona hafai ndio maana walimtania na kumpa uenyekiti wa kijiji japo nacho cheo hicho hasitaili. Siku 26 mara huyo kakimbilia alikotoka anatapayuka kuwa hakuna sera. Je tujiulize angepata kile alikimbilia Chadema angeyasema? Huyu ni mtu wa kuogopa kama ukimwi. Nawaomba CCM wamwangalie sana atawaharibia mambo. Na hata hivyo keshaharibu. Chadema si mahali pa kukimbilia na kupewa cheo, wanangalia uhadilifu wako, historia yako, elimu yako na uelewa wako. Ni chama makini na chenye watu wa kujua kuchambua

    ReplyDelete
  18. msameeni kwa hilo najua ni upeo mdogo alionao na ufinyu wa mawazo ukijumlisha na uhaba wa elimu ndio ilipelekea yotew haya naimani akiyasoma haya maoni atajuta sana na atajisikia vibaya sana kiasi hata cha kutaka kunywa sumu pole sana CHADEMA OYEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEEE

    ReplyDelete
  19. Mh.Jk
    Acha kuwanadi hawa watuhumiwa wanakuchafulia. Hasa Lowasa,Chenge,Mramba,Dewji, kwa kweli ni watuhumiwa sawa lkn hawajafanya vizuri,mpaka sisi wasoni tunakusutukia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...