askari wa usalama barabarani pamoja na mashuhuda waliokuwepo katika eneo hilo wakiliangalia lori hilo likiwa ndani ya daraja.
lori lililopatwa na mushkeri na hatimae kuingia ndani ya daraja na mto msimbazi lililopo katika barabara ya mandela rodi,eneo la matumbi leo.winchi ikiwa tayari tayari kutoa msaada wa kuinyanya lori iliyoingia katika daraja la matumbi leo.
hapa magari yakipita katika upande wa pili wa barabara ya mandela rodi baada ya kutokea kwa ajali hilo.


Kaka Salama ?

Pole na kulizungusha Durudumu (GURUDUMU), Leo wakati nimechelewa kwenye foleni naelekea kwa ofisi kulizungusha DURUDUMU Nilikutana na hili.

Na ndo raha ya kutembea na hivi vimweku mweku vyetu, Ila itabidi nije unifundishe jinsi ya kutumia Bulakiberi, Yangu inachukua snapu, lakini sijuagi ata kutuma kwa EM EMU ESI, walahi tena.

Ukitoka Unguja basi niambie nije hata ofisini au pale sehemu yetu ya ghahawa japo unikochi kwa sekunde, maana uwa nakutana na ma iventi kedekede, lakini yahe sijui kuitumia, mie nilinunua kwa ajili ya kupokea na kupiga tu, kumbe walahi Hii Bulaki beri yangu ina manjonjo kedekede, wlahi mpaka inachanganya ati.

Hii lori imetumbukia kwenye daraja, yaani sijui Vipi, hata sielewi, Sasa cha ajabu REDIO FM MBAO hazikosekani Sehemu kama hii, nilipohoji majibu yalikuwa kama Ifuatavyo

Wa Kwanza,

“Hapana dreve Alikuwa amechoka akamuachia UTINGO aselebuke, yeye akawa auchapa Siti ya nyuma, Halafau si unajua Bwana usingizi unaambukizwa, UTINGO naye akaanza kuuchapa huku anasuka steringi, loo Kuhamaki Yuko chini ya daraja MATUMBI”

Wa Pili

“ Hapanaaa, Dreve aliona MALUWE LUEW yanavuka barabara , ndo kusema ayakwepe, hamadi, chini ya Daraja Matumbi"

By

Mdau Addo

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 9 mpaka sasa

  1. Afu ndo mnalilia wawajengee barabara za juu kwa juu na madaraja ya uhakika.Vitu vidogo kama hivi mnashindwa kuvitumia kwa uangalifu sasa wakijenga hizo "sky-way" Rd na madaraja si ndo vifo vya kishenzi vitaongezeka kila siku.

    ReplyDelete
  2. mdau wa kwanza umenena, tutakuwa tunaporomokewa kila siku!cjui tuwekage na ngao kwa juu ili walau iwe inadhurika gari walau sisi tusizikwe bila kutambuliwa. loh!barabara za juu?sasa hili likishuka unafkiri wanaenda wangapi? madereva wajinga na ubovu wa magari vitatuua hata tukijenga barabara alfu angani

    ReplyDelete
  3. sasa hili black mamba mbona jana halikwenda kibaha jamani maiti 4 zililaliwa na roli masaa kibao hadi zikapondeka?turudi kwenye hii ajali sasa dereva kama ulichoka si mngepaki pembeni mkapumzika jamani usingi na kuendesha gari wapi na wapi jamani.

    ReplyDelete
  4. Kaka mtoa maoni wa mwanzo big up sana!

    Skyways hazina maana kwa nchi kama hii kutokana na sheria kutofuatwa na vyombo husika kama nchi jirani tu, yaboreshwe maisha ya mtu wa kima cha chini halafu skyways baadaye 2050 au zaidi. Ulizia madereva wa bongo wa magari ya masafa marefu wanavyotwangwa faini nchi jirani kwa makosa ya kizembe. Hili lori litakuwa limetumbukia darajani usiku wakati magari yakiwa machache mno barabarani, nini tatizo - uzembe? ulevi? ubovu wa gari?

    KK
    Magamba coast

    ReplyDelete
  5. Hizi leseni za kununua.

    ReplyDelete
  6. Eti watanzania tunataka barabara za kupita juu kwa juu, mbona itakuwa mauaji ya kila siku!!

    ReplyDelete
  7. Matunda ya kutuma SMS-text barabarani!

    ReplyDelete
  8. Hatuko serious na usalama barabarani hata kidogo.
    1 leseni nyingi ni fake na
    zinatolewa na polise hao hao
    2 zaidi ya nusu yamagari bara
    barbarani ni mabovu kabisa
    3 kagua bima za magari, mengi
    hayan bima, mbele ya macho yetu
    4 piki piki ndio usiseme,watu
    wanadiriki kuendesha pikipiki
    za namba ya chassis mbele ya
    traffic officer bila
    kuchukuliwa hatua yoyote
    5 SHERIA ZA USALAMA BARABARANI
    ZIMEPITWA NA WAKATI NA HAFIFU
    MNO

    ReplyDelete
  9. Simlaumu dereva hawana REST AREA sasa gari kubwa namna hii angeli park wapi?

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...