Meneja Mkazi wa Synovate, Aggrey Oriwo (kati) akiongea na wanahabari leo.
Kushoto ni Meneja Huduma Jane Meela na kulia ni Bw. Ernest.

Ikiwa ni takribani siku tatu zimepita tangu REDET kutoa matokeo ya utafiti ya uchaguzi nafasi ya Urais kuwa Raisi wa sasa, Jakaya Kikwete ndiye anayeongoza katika kura hizo, Kampuni nyingine ya kimataifa ya utafiti ya SYNOVATE wametoa matokeo ya utafiti wao kuhusu nafasi ya uraisi ambao imeonesha kuwa iwapo uchanguzi ungefanyika leo, mgombea uras wa Chama Cha Mapinduzi, DK. Jakaya Mrisho Kikwete angepata asilimia 61 ya kura zote.

Dk. Wilbroad Slaa wa CHADEMA yeye angeshika nafasi ya pili kwa kupata asilimia 16 na kufatiwa na Prof. Ibrahim Lipumba wa CUF ambaye angepata asilimia 5.

Utafiti huo umeonesha pia kuwa kuna asilimia 13 ya waliohojiwa ambao hawakuweka wazi maoni yao na ambao kama watapiga kura leo, JK angeweza kupata asilimia 70, Dk Slaa asilimia 18 na Lipumba asilimia 6.

"Waliobana maoni yao katika swali hili ni wengi sana asiilimia 13% ya wahojiwa wote. Ikiwa watapiga kura ilivyodhihirika hapa basi 70% watampigia Jakaya Kikwete,Wilbroad Slaa 18%, Lipumba 6% wengine 6%," ilismea sehemu ya taarifa hiyo iliyotolewa mchana huu na Meneja wa Synovate Tanzania, Aggrey Oriwo, mbele ya wanahabari ofisini kwake Mikocheni jijini Dar es salaam.
Chanzo cha habari hii

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. Utafiti wa Redet ulisema kama uchaguzi ungefanyika mwezi uliopita basi Kikwete angeshinda kwa asilimia 70. Utafiti wa Synovate unasema kama uchaguzi ungefanyika leo Kikwete angeshinda kwa asilimia 61. Ila Kikwete akipewa na kura zilizoharibika basi anapata ushindi wa asilimia sabini.
    Ndugu wapiga kura, hizi tafiti zote hazina maana kwako wewe na kura yako. Fuatilia kampeni kwa makini na tumia kura yako ya siri kwa busara. Msifuatilie kampeni za Kikwete, Lipumba na Slaa peke yao, kuna wagombea wengi. Pimeni kwa busara maana kura zenu ndizo zitakazowaacha na kilio cha mbwa meno juu kwa miaka mitano.

    ReplyDelete
  2. Kwahiyo hawa jamaa walikuwa wanasubiri paka wa kumfunga kengele? Ni majuma mangapi yamepita tangu habari za wao kuchakachua matokeo yao kupita? Nadhani kwa sasa wameshapoteza imani ya wateja wao, akina sisi!!

    ReplyDelete
  3. Mimi nawasifu wabongo kwa ubunifu siku hizi.
    Na hawa jamaa, nawasifu zaidi kwa perfect Publicity, maana hamna kipindi kizuri kutangaza shughuli zako haswa kama inahusiana na mambo ya uchaguzi.
    Mpaka tukipata katiba mpya, Tume ya Uchaguzi ya Ukweli. Siweli kulaumu sana kama nyanda nyingine hazifanyi kazi vizuri.

    ReplyDelete
  4. Bro Michu mbona hawa jamaa ni wachaga tupu.nina wasiwasi na hiyo organization.

    ReplyDelete
  5. Hizi tafiti ni za kinafiki tu, na endapo matokeo yangeonyesha vyama pinzani kushinda basi hizo tafiti nina imani zingepigwa marufuku. Watanzania tuangalia kura zetu na si mtokeo ya tafiti zinazoibuka kila kukicha.

    ReplyDelete
  6. ukimuangalia huyo jamaa mwenye Tshirt nyekundu kwa makini unamuona kabisa kuna aibu usoni kwake,kwamba kinachoelezwa hakiko sawa moyoni kwake. angalieni vzuri hyo body language

    ReplyDelete
  7. Ni bora wangeficha hio ripoti maanake ni takataka na inaonesha haikupikwa ikaiva vizuri. Sijui kwa wanaowafanyia kazi za kitafiti za biashara itakuwa vipi. Mimi sitaweza kuwapendekeza kufanya tafiti kwenye biashara zangu. Ripoti haieleweki, inajichanganya, imejaa makosa ya uchapaji, majedwali yamekosewa, achilia mbali Njia waliosema kuwa walitumia kufanyia utafiti. Yaani inasikitisha kama hawajui hata maana ya "Margin of error", "marginal error", "significant level" "standard error" na "confidence level".
    Pole watanzania manake mmeishakuwa mambumbumbu wa kupakuliwa ripoti takataka. Hatutaendelea hivyo kama watu na kampuni kama hizi hawatadhibitiwa mapema
    Mimi hapa natafuta ndoo manake imenichefua kiasi chake

    ReplyDelete
  8. Hawa watafiti wanapoteza tu muda wa watu. Kwa nini kuandikia mate wakati wino upo? Wasubiri hapo tarehe 31 Oct wananchi wakapige kura fullstop.

    ReplyDelete
  9. Kweli siku ya kufa nyani.....! Sasa kama watoa maoni wote hawa hapa juu hawakubalinai na tafiti zenu nyie mmepata wapi hizo takwimu? Hivi chama cha kijani huwa kinatoa ruzuku kwa tafiti kama hizi? Kama ndiyo hapo mtakuwa mmevuna bingo ya kutosha. To be honest takwimu zenu sio sahihi mnafanya ili kunyoosha mambo yenu binafsi na ukweli mnaujua kuwa Dr Slaa hakamatiki.

    ReplyDelete
  10. Wewe mchangiaji uliyesema hao ni wachagga watupu!! Una hakika?? Acha ukabila na uchangie kitu cha msingi, ukabila got nothin to do with anything ok? Nyie ndo mnasababisha mambo ya kikabila yaendelee TZ,nakukemea kwa nguvu zoteee!! Get a life n leave ukabila n most of all dnt associate kabila la mtu na kile afanyacho!!
    Yaani umeonesha jinsi gani ullivo-mvivu wa kufikiria n staight away rush to kabila la mtu!

    ReplyDelete
  11. UTAFITI WENYEWE UMETUMIA SAMPLE YA WATU 3000 KATI YA WATU MILIONI 19. HAHAHAHAHA, WIZI MTUPUUUUUU

    ReplyDelete
  12. Kikwete atashinda tu. Majority ya Watanzania (over 65% ya Watanzania wapiga kura) tutampigia kura; nyinyi kyadema mtabaki na alnacha zenu za wishful thinking. Venceremos!!!!!!!!!!!!!!!!!

    ReplyDelete
  13. Chadema wacheni ubishi. Taasisi zote za opinion polls zinaonyesha kuwa JK atashinda: Na hiyo ndiyo halisi. Anzeni kuzoea kuwa si lazima watu wote tz tuwe watumwa wa matakwa ya chadema!!! Copy & paste that.

    ReplyDelete
  14. Loo!!!! Sijaona watu wabishi kama hawa wapinzani wa Tanzania. Bado wako katika upinzani wameanza udikteka. Fortunately CCM itawagaragaza wapinzani wote 31/10/2010 na ku-abort udikteta wao.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...