Marehemu Abdallah Ramadhani
Picha na habari kwa hisani ya
Kituo cha Televisheni cha Channel TEN na Redio ya Magic FM cha jijini Dar es salaam kimepata msiba kwa kuondokewa na mmoja wa watangazaji wake mahiri na vijana, Abdallah Ramadhani (Pichani) ambaye amefariki dunia katika ajali ya gari Ijumaa wiki hii.

Marehemu Abdallah Ramadhani alipata ajali hiyo akiwa njiani mjini Beira, Msumbiji akitoka Afika Kusini kurejea Tanzania Alhamisi tarehe 7 mwezi huu.

Taarifa zaidi zinasema kuwa marehemu alikuwa kwenye gari aina ya Toyota Prado ambayo ilipasuka tairi la mbele na kupinduka mara kadhaa na hivyo kusababisha kifo chake mara baada ya kufikishwa hospitalini.

Mara baada ya kutokea kwa ajali hiyo iliyompasua kichwa, familia yake ilifahamishwa ambapo mdogo wake aitwae Hussein alikwenda kumuangalia hospitali alikolazwa kabla ya kufariki.

Abdallah atakumbukwa na watazamaji wa Channel TEN kwa usomaji wake wa taarifa za habari kwa umakini na ufasaha na kwa wasikilizaji wa Magic FM. Kabla ya kufikwa na mauti, alikuwa katika mapumziko ambayo aliyatumia kwenda nchini Uingereza kwa siku kadhaa kabla ya kupitia Afrika Kusini ambako alipumzika kwa siku chache na baadaye kuamua kurejea nchini Tanzaniakwa njia ya barabara kupitia Msumbiji.

Pole kwa ndugu, jamaa na nyote mlioguswa na msiba huu.
Apumzike pema Abdallah Ramadhani.
AMEN.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 19 mpaka sasa

  1. nilipenda jinsi alivyokuwa anatangaza,nakumbuka tabasamu lake,
    R.I.P Abdallah

    ReplyDelete
  2. Inna lillahi wa inna ilayh raajiuun,

    Masud

    ReplyDelete
  3. Inalah wainalilah rajuina,Mungu ailaze mahali pema peponi roho ya marehemu,
    Amina

    ReplyDelete
  4. R.I.P, its soo sad. Mwenyezi Mungu amsamehe zambi zake apumzike kwa amani, amen. Poleni sana wafiwa, hasa kwa mjane na mtoto wake, inatia huzuni sana.

    ReplyDelete
  5. Tunakukumbuka Abdulla Ramadhan kwa usomaji wako mahiri wa taarifa ya habari.

    Kwa kweli tumepokea taarifa ya kifo hiki kwa mstuko mkubwa kwani ni kijana mdogo sana ambaye angeweza kuwa na a bright future.

    Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema ailaze roho ya Marehemu pema peponi. Amin.

    ReplyDelete
  6. R.I.P Abdallah

    ReplyDelete
  7. Abdallah alikuwa makini sana katika kazi. Sisi wapenzi wa habari tunafahamu umahiri wake na usikivu. Ni pigo kwetu vijana wapenda maendeleo. Wapenzi wa asubuhi njema tutamkumbuka sana.

    ReplyDelete
  8. KELAND NURSERY & PRIMARY SCHOOLOctober 11, 2010

    POLENI SANA NDUGU JAMAA NA MARAFIKI MUNGU AWAPE FARAJA YA KIPEKEE WAFIWA BWANA ALITOA NA BWANA AMETWAA JINA LAKE LIBARIKIWA.AMEN

    ReplyDelete
  9. innah lillah waina ilaih rajiun!aisse tusijisahau kwakweli tumkumbuke mungu jamani tufanyeni ibada kifo ni siri kubwa mungu alituwekea broo alikuwa mahiri kwenye kazi yake anaonekana hakuwa m2 mwenye majivuno wala kujisikia kwa jinsi anavyoonekana ijapokuwa simfahamu zaidi ya kumuona kwenye tv mungu amlaze mahali pema peponi na ampe kauli thabit inshaallah amin,moud tall tanga.

    ReplyDelete
  10. INNA LILLA WA INNA ILAIHI RAAJIUUN... KWAKE YEYE MWENYE EZ MUNGU NA KWAKE TU NDIO MAREJEO YETU ... ALLAH AMSWAMEH DHAMBI ZAKE, AMNG'ARISHIE KABURI LAKE KWA NURU YA QURAAN NA AMPUMZISHE MAHALI PEMA PEPONI ALLAHUMMA AAAMIN THUMMA AMIIN..POLENI WAFIWA MIMI SI NDUGU YANGU WALA SIKUWAHI KUMUONA USO KWA MACHO ZAIDI YA KWENYE CHANNEL TEN LAKINI CHOZI LIMENITOKA NA NAUMIA NDANI KWA NDANI....

    ReplyDelete
  11. R.I.P Dulla...pole sana family Mungu atawapa comfort na marafiki tupo daima kushikana mikono.

    Krom Mozes

    ReplyDelete
  12. I knew him when he was working for Vodacom (T) Ltd

    Rest in Piece Bro..

    ReplyDelete
  13. Tunakukumbuka Abdulla Ramadhan kwa usomaji wako mahiri wa taarifa ya habari.

    Mwenyezi mungu amwangazie mwanga wa milele na ailaze vema roho ya marehemu Abdulla Ramadhan mahala pema peponi.Amin

    ReplyDelete
  14. Mungu Amlaze mahali pema peponi, Amina.

    ReplyDelete
  15. Dah, Ukweli Kazi ya Mungu haina makosa, R.I.P Abdallah, Ukweli sijaamini ila Mungu ailaze mahali pepa roho yake. .

    Julius Kanwa

    ReplyDelete
  16. Ni dhahiri kila nafsi itaonja mauti kwa wakati wake; Abdallah yeye amepumzika, kikubwa ni kumuombea mapumziko ya amani na Mungu amsaidie aingie peponi, poleni sana mke na mtoto wa Abdallah, mlimpenda sana ila kila nafsi ni mali ya Mungu na kwa Mungu itarudi. Mshukuruni Mungu kwa kipindi chote alichoruhusu nyinyi kuwa na Abdallah mkimkumbuka kwa mema yote mliyoshiriki pamoja. Maneno hayatoshi kuwafariji ila Mungu mwenyewe aliyeruhusu Abdallah arudi kwake mapema kiasi hiki awape faraja ya kweli. Mtegemeeni Mungu pekee katika jambo hili gumu kwa kila mwanadamu. Rest in peace Abdallah and may God protect and guide your family - mother, wife, son, brothers and sisters.

    ReplyDelete
  17. Tunakumisi Broo katika habari na mapitio ya magazeti.
    Kila kilicho na uhai kitaoncha mauti.

    ReplyDelete
  18. Mungu akusamehe dhambi zako, Abdallah. na ulale pema peponi. Aaamin. We didn't know each other personally, but I am so touched.

    ReplyDelete
  19. R.I.P. Brother........Nimepata tarifa sasa hivi nikizungumza na watu Tanzania. Wako R.H. Tambwe

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...