Marehemu Monica Hansson Chuwa wakati wa uhai wake.

Kwa niaba ya Familia na ukoo wa Chuwa wa Stockholm SWEDEN,tunasikitika kutangaza kifo cha ndugu na dada yetu mpendwa MONICA HANSSON CHUWA kilichotokea usiku wa kuamkia leo tarehe 03/10/2010 nyumbani kwake ,Msiba na Mipango ya mazishi inafanyika nyumbani kwake hallonevägan 4 Bromma,Stockholm SWEDEN.

MAOMBI NA USHIRIKIANO:

Kwaniaba ya Familia na Marafiki wa marehemu,Tunaomba michango ya hali na mali kutoka kwa watanzania wote walowahi na wasiowahi kumfahamu. Michango yenu ya hali na mali inahitajika ili kutuwezesha kufanikisha shughuli hii nzito ya msiba wa mpendwa wetu MONICA.

KWA MCHANGO WAKO TAFADHALI TUMIA DETAILS ZIFUATAZO:
PAYPAL ACCOUNT(International tranfer): thelatemonica@hotmail.com

AU

Kwa waliopo SWEDEN

ACCOUNT NAME: DEVOTA SEBUYOYA
ACCOUNT NUMBER: 4155 0201 073
BANK: NORDEA BANK
CONTACT DEVOTA @ +4676 863 6248

Tunatanguliza shukurani za dhati,Kwaniaba ya Familia ya Chuwa

FRED ZG SSEBUYOYA.

"Bwana alitoa na bwana ametwaa, Jina la bwana libalikiwe"

AMEN.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 14 mpaka sasa

  1. We are all left with a large hole from our loss. We will have to trust God to fill it.
    We will all miss you MONICA a good friend of ours.Rest in peace
    from A F vuai

    ReplyDelete
  2. Pole sana devota, kweli inauma sana lakini tushukuru Mungu sisi sote tuko safarini, R.I.P dada monica

    ReplyDelete
  3. Kwa ndugu zetu wa Sweden, Mohi, Tanzania na ulimwengu mzima, poleni sana kwa msiba huu. ni kweli kwa "twatoka mavumbini na tutarudi mavumbini". Rambi rambi toka NY.

    Masao

    ReplyDelete
  4. pesa alizokuwa marehemu anadhurumu watu zinatosha kufanikisha shughuli yake ya mazishi
    Amen

    ReplyDelete
  5. Dah wewe Mdau hapo juu uliye sema kuhusu pesa yani ur so mean , hata kwenye msiba bado unakumbuka chapaa?

    ReplyDelete
  6. Salaams,

    Poleni wafiwa,

    Ndugu yangu hapo juu,

    Kifo ni kifo, kama alikudhulumu muachie MWenye Ez Mungu apitishe hukumu yake kwa kuwa yeye ameenda mbele ya haki, na wewe angalia yako, usimseme maiti vibaya maana na wewe bado unaishi inaweza kuja siku ukawa mmoja wa wanaodhulumu, so wewe mwahie Mola kama aliwahi kukudhulumu basi yeye ndio anajua cha kuhukumu, usifanye mzaha na kifo ni cha uchungu sana , jiweke kwenye position ya waliofiwa halafu mtu aseme maneno hayo ulosema wewe , yanauma!!! pole kama ulikuwa mmoja wa waliodhulumiwa , RIP

    ReplyDelete
  7. wewe uliyesema mambo ya kudhulumu nadhani huna dini mtu akifa hazungumzwi kwa mabaya yaaaani ndugu yangu dhambi zake zote umebeba wewe sasa kazi kwako yeye atakuwa kasamehewa!mungu amlaze mahali pema peponi dada yetu mpendwa

    ReplyDelete
  8. Juma Ndambile NAPENDA KUWAFAHAMISHA KWA WALE MNAOMFAHAMU TONY DRAFT AMEFARIKI INDIA JANA KWA AJARI YA GARI ALIKUWA ANAENDESHA GARI ANATOKA KWENYE SHEREHE YA WATANZANIA WANAOISHI INDIA AKAGONGA MTI NA KUFARI MIPANGO YA KULETA MWILI WAKE INAFANYIKA NA MSIBA UKO SINZA NYUIMBANI KWA BABA YAKE

    ReplyDelete
  9. Hakuna cha kubeba dhambi wala nini anayeongelea dhuluma mwacheni aongee si uonge... yule mvulana wa watu kule ilala/kariakoo anavyouza chipsi mnaona safi? Mambo mengine yanasikitisha sana so hakuna cha maiti kuongelewa vibaya or so and so waacheni watu waseme ukweli... pesa ya mtu ni mbaya sana jamani jasho la mtu halafu ukamchukulie kisichokuwa kwako bali ni cha kwake? Tuacheni mambo ya dhulma... R.I.P dada na wengine tuliobaki tujifunze..

    ReplyDelete
  10. RIP Monica,
    @Anonymous wa 4...Yaani mnamuonea wivu na kumzushia mtu mpaka anapokufa jamani?
    Marehemu alikuwa ana roho nzuri saaana!
    Alikuwa na uzuri wa nje na ndani!
    Habagui wala hachagui... Na ndio maana alikuwa anafaniwa sana!!
    Poleni sana wafiwa.

    ReplyDelete
  11. ni ajali na sio ajari

    ReplyDelete
  12. We nonbinadamu wa 9 tumeshakustukia, ndio wewe yule yule wa 4. Sema jina lako kama umkweli, na kama una malalamiko njoo na vidhibiti au nenda kwenye vyombo vya sheria!
    N:B
    Bwana akikukataa makosa ya nani?
    Michuzi ebu toa uchafu wake hapo juu. Mtu kama hajui kufiwa!

    ReplyDelete
  13. JAMANI TUNAJUA KIFO KINAUMA NA SOTE TUNAELEKEA HUKO ILA DHULUMA SI KITU KIZURI HATA MBELE YA MUNGU. NA HAO WANAOSEMA SI VIZURI KUZUNGUMZIA MAMBO HAYO WAKATI HUU NI KWA KUWA HAWAJUI NI MATESO NA DHIKI KIASI GANI MAREHEMU AMEMSABABISHIA YULE KIJANA. KWA KAWAIDA MAREHEMU HUWA HAZUNGUMZIWI VIBAYA ILA JAMBO ALILOFANYA HUYU HALISTAHILI KUKAA KIMYA NA NDUGU ZAKE WANAJUA YOTE COZ NAO WALISHIRIKI KTK KUFANIKISHA HIYO ISSUE.

    ReplyDelete
  14. jamani tujifunzeni kutokuhukumu.iko siku na sisi tutahukumiwa.walionamachungu na waliofiwa tusameheyane.tuombe MUNGU ampumzishe aliyetangulia.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...