Marehemu Leticia Kaijage enzi za uhai wake.
Waombolezaji katika msiba wa Leticia Kaijage wakiwa katika msiba nyumbani kwa kaka wa marehemu Tabata Segerea nyumbani kwa kaka wa marehemu.
Waombolezaji ambao baadhi yao walifanya kazi pamoja na Marehemu katika Kampuni za PR wakiwa msibani.
Jamaa na marafiki wa marehemu
Sanduku lililouhifadhi mwili wa Marehemu Leticia likiwa tayari kwa misa maalum ya kumuombea.
Waombolezaji wakitoa heshima za mwisho kwa mwili wa marehemu.

Marafiki wa marehemu,Celine Njuju na Betrice Singano walishindwa kujizua na kujikuta wakibubujikwa na machozi kwa huzuni ya kuondokewa na mwenzi wao.
Mwili ukiingizwa katika gari na baadhi ya waombolezaji tayari kwa safari ya kwenda uwanja wa ndege ili kuweza kusafirisha mwili wa marehemu kwenda kijijini kwao Nyakigando Kata ya Kaibanja Wilaya ya Bukoba Vijijni kwa mazishi.
Gari likiwa tayari kuanza safari ya kuelekea Uwanja wa Ndege.
Mungu ailaze Roho ya Marehemu Mahala Pema Amina.Picha na Mroki Mroki

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 11 mpaka sasa

  1. Very sad news! Hard to believe. May she Rest in Eternal Peace.

    ReplyDelete
  2. oh maskini what happened to letti?
    may she rest in peace, amen

    ReplyDelete
  3. Michu please lazima uelewe kuwa hii blog wasomaji wake wengi ni wa Abroad,kwa hiyo unapotokea unagusia habari ya either msiba au harusi ya wanamaarufu wa ndani lazima ufafanue zaidi unasihi wake.
    sasa huyo letti ni nani?
    Mola umlaze mahali pema peponi

    Mdau Istanbul

    ReplyDelete
  4. May Almighty God rest her Soul in eternal Place, I worked with Leticia Kaijage at former THB(Tanzania Housing Bank)Computer Section before she became a Journalist, She was very charming and hard worker, my condolences to Kaijage's Family.

    BEN SIZYA. London UK.

    ReplyDelete
  5. Jamani huyu ni nani?

    Kafa na nini?

    Yaani habari imeandikwa utadhani kafa rais ambae wote tunamfahamu?

    Tupewe taarifa kamili sio picha tu

    Rest in peace Leti

    ReplyDelete
  6. Leticia Kaijage ni mwandishi wa habari wa siku nyingi! Amefanya kazi business times na The African, akawa Head of PR FCB(PR Consultant wa Vodacom enzi hizo, baadae akawa SCANAD na hadi mauti inamkuta alikuwa PR Head, ZK Advertising Agency(PR Consultant Zian. Kuwa maarufu si lazima uwe Raisi mdau, kwa walioko kwenye tasnia ya uhandishi wa habari na ambao walikuwa wanasoma The African na Business times late 1990s wanamfahamu vizuri huyu dada, sasa marehemu! Rest in Peace dada yetu.

    ReplyDelete
  7. R.I.P Leticia KAIJAGE. Nilimfamau mwaka 1999 wakati nikiwa Chipukizi sana kwenye fani ya Uandishi wa Habari pale Habari House. yeye alikuwa Mwaidishi wa The African na mimi wakati huo, nilikuwa Mwandishi wa Bingwa. tuliendelea kufahamiana kama waandishi wa Habari hadi majuzi tu akiwa pale ZK na mimi nikiwa FEMINA HIP. Binafsi nilimfahamu kama mwanadada mchapakazi na muwazi hasa kwa kuwa sikuwahi kumfahamu zaidi nje ya harakati za kazi.
    MUNGU AILAZE ROHO YAKE MAHALI PEMA. AMIN

    ReplyDelete
  8. Huyu ni nani na kafa na nini mi nadhani haihusu.

    Wewe mdau unayetaka taarifa kamili zipi zaidi ya zilizopo? na ili iweje?kama humfahamu unataka umfahamu baada ya kufa? ili ikusaidie nini?

    Asante kaka michu kwa taarifa, kazi nzuri na Mwenyezi Mungu ailaze Roho ya Dada yetu Leticia Kaijage mahali pema. Amen!

    ReplyDelete
  9. Poleni ndugu wote MLiofiwa.
    Kaka michuzi tuelezee wasifu wa dada Lett hatumfahamu.
    Rest in peace Lett

    ReplyDelete
  10. Bushasi bungi muno,poleni sana Familia ya Leticia me ckukujua ila baada ya kusoma kuwa unatoka Kaibanja ambayo ni kata yangu na shule yangu ya msingi ilikuwa Kaibaja kweli nimeumia,Rest in Peace.

    ReplyDelete
  11. Poleni sana wafiwa,Mungu awape nguvu.Letty alikua jirani yani Banana,nimesikitika sana,lakini ni safari ya wote,May her soul rest in peace
    Mdau USA

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...