Ndugu wapendwa,
Sisi familia ya Salukele tunapenda kutoa shukurani zetu za dhati, kwenu wote mlio jumuika katika kuwezesha kufanikisha kumsafirisha Marehemu baba yetu Mzee Mathew Salukele nyumbani Tanzania. Marehemu alizikwa siku ya Jumamosi tarehe 10/16/2010.
Wakati tukiwa na mshangao,majonzi na uchungu mkubwa kwa kumpoteza baba yetu mpendwa kwa ghafla, Jumuiya ya watanzania hapa Columbus wameongoza shughuli zote za sala na michango ya hali na mali na tungependa kuwashukuru kwa moyo wote.
Tungependa pia kutoa shukrani zetu za dhati kwa Jumuia za Watanzania kutoka nje ya Columbus na majirani zetu kutoka Kenya, Uganda na Zambia kwa misaada yao ya hali na mali.

Hakuna neno la kusema ambalo tunaweza kufananisha na upendo wenu usio na kikomo ambalo tutalinganisha na ukarimu wenu katika kipindi hiki kigumu. Wengi wenu mlisimamisha kazi zenu, masomo yenu, biashara zenu na shughuli zenu mbalimbali kwa ajili ya kutufariji. Uwepo wenu na maombi yenu yameweza kutufariji kwa kiasi kikubwa na kututoa ukiwa nakujiona kama familia moja. Tungependa tuendelee kushirikiana kwa moyo huu, na hii iwe changamoto kwa jumuia zote.
Jina la Bwana litukuzwe na Mungu awe nanyi daima.
Asanteni sana
Mungu awabariki
Familia ya Salukele.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 3 mpaka sasa

  1. Mzee KifimbochezaOctober 20, 2010

    Poleni kwa kufiwa na mzee wenu. Mungu azidi kuwafariji kwa majonzi ya kuondokewa na baba yenu.

    Naomba niwakosoe kwenye lugha. Katika Kiswahili, marehemu hawezi kuzikwa 10/16/2010. Hakuna tarehe 10 mwezi wa 16 katika Kiswahili chetu. Nadhani ulimaanisha 16/10/2010 (tarehe 16 mwezi wa 10).

    Tarehe 10/16/2010 inawezekana tu katika Kiingereza tena cha Kimarekani (ambacho kusema ukweli si sanifu). Kama tunaongelea Kiswahili basi ni cha Congo DR au Kenya au Uganda si cha Tanzania. Ama kama ni Kifaransa si cha Paris, bali cha Quebec au Kama ni Kichina si cha China ila cha Wamalaysia waliozaliwa Malaysia baada ya babu zao wa zamani sana kuhamia huko wakitokea China.

    Tusiharibu Kiswahili chetu kwa kukinyambulisha neno kwa neno kutoka katika Kiingereza. Kiswahili ni lugha inayojitegemea kisarufi. Kama tunavyowacheka wanaongea Kiingereza kilichotafsiriwa moja kwa moja kutoka Kiswahili, basi pia tuwacheke nyie mnaotafsiri Kiswahili neno kwa neno kutoka Kiingereza.

    Sehemu nyingine za tangazo zimeandikwa vizuri. Naamini wewe ni "Mswahili" mzuri ila una tatizo la kisaikolojia tu la kuthamini Kiingereza zaidi.

    ReplyDelete
  2. We kifimbocheza nini tena na wafiwa badala ya kuwafariji watu wa watu ndo nini hiyo ka umeshaelewa unafikiri ni wewe tu umeelewa hata sisi tumeelewa hiyo tarehe ilikuwa hakuna haja ya kuwaattack wafiwa wa watu.

    POLENI WAFIWA, ACHANENI NA HAWA WANAOCHAFUA HALI YA HEWA YA GLOB YA JAMII

    ReplyDelete
  3. Mzee Kifimbocheza, usikurupuke tu nakuandikia usichokijua. Kwa huku marekani hivyo ndivyo tunavyoandika tarehe, so 10/16/2010 ni very correct. Na kwa kifupi tu, hao wafiwa wanaishi marekani na hiyo barua ya shukrani imetumwa all over the world sio bongo peke yake.

    Jamni tuweni wastaarabu wkat mwingine.

    Rest In Peace Mzee Salukale. Poleni sana, Happy, David na Jumuiya ya Columbus, Ohio.

    Tupo pamoja.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...