Hayati Monica Hansson Chuwa

Ukoo wa Chuwa uliopo Stockholm SWEDEN, Unapenda kuwataarifu ndugu na jamaa wote kwamba Mazishi ya MONICA HANSSON CHUWA yatafanyika Jumatano ya tarehe 13/10/2010 saa 10:00 AM (Asubuhi) kwenye makaburi ya SKOGSKYRKOGÃ…RDEN "heliga kapel" SANDSBORG.

Baada ya shughuli za mazishi ndugu na jamaa wote tutajumuika kwa pamoja kwenye ukumbi uliopo SKARPNÄCKS ALLE 33-35 kwaajili ya rambirambi.

Ukoo wa Chuwa unachukua nafasi hii kuwashukuru wale wote waliojitokeza na waliotoa michango yao ya hali na mali katika kufanikisha shughuli hii ngumu ya msiba.

Tunaomba wale wote watakaokuwa na nafasi wajitokeze kwa wingi ili kwa pamoja tuweze kuusindikiza mwili wa ndugu yetu mpendwa MONICA.

Kwa niaba ya Ukoo wa CHUWA,
FRED ZG SSEBUYOYA.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 7 mpaka sasa

  1. Devota, na dada zako wakubwa poleni saana. Sasa kaswali kadogo tu, najua unafahamu kuwa si siri marehemu alimtapeli Leopord hela nyingi za kibali, sasa kuna mpango gani kumrudishia angalau kifutia jasho tu?

    ReplyDelete
  2. We fara Leopord or whatever the name acha mambo ya usen!e kwenye mambo ya misiba....kama ulitapeliwa kimpango wapo bwana....nani mwenye akili chafu kuandika upuuzi kama huo kama si wewe mwenyewe....kama ulitapeliwa fuata taratibu zinazokubalika....Fara wewe!

    ReplyDelete
  3. Msiba huu umekuwa kama ndio sehemu ya kujitafutia kipato au mtaji , marehemu anazikwa hapa stockholm sasa itakuwaje hawa wafiwa kutaka michango ya hali na mali kutoka kwa watu ? hapa sweden kuna taratibu kuwa kama wewe ni mswedi basi serikali ndio itachukua jukumu lote la mazishi , nashindwa kuwaelewa Devota na Fred kwa kuomba mchango wa hali na mali katika msiba huu KULIKONI ?

    ReplyDelete
  4. mimi nafikiri dunia hii kuna watu wenye roho ya kipekee yani mbaya sana. Hivi hadi kwenye misiba watu mnahoji upuuzi kama huu? Lakini inawezekana sio kosa lenu mungu awasamehe tu.

    na wewe mbumbumbu wa mwisho unafikiri michango ni kwaajili ya kusafirisha mwili tu?

    Kwani huyo Devota na Fred ndiyo nani wasiombe michango kama watu wengine?

    Labda kama hujui Marehemu ni Dada mkubwa wa Devota na sioni sababu yoyote ya kumsimanga mfiwa eti kwakuomba michango kama watu wengine ili kufanikisha msiba wa dada yake..Acheni roho za kutu haswa nyinyi mnaoishi sweden. Inasikitisha kuona Jinsi mnavyochukiana hadi kwenye misiba.
    Yani mnaishi kama wanyama.

    ReplyDelete
  5. Hii si kumtendea haki Leopord kwani hata nyumbani mtu akifa ndugu wa marehemu huuliza kama mtu alikuwa anamdai marehemu na kama marehemu pia alikuwa anadai ili malipo yafanywe. Sasa Leopord kakosa nini? kuwa marehemu haina maana hata madhambi yote yazikwe na uuitwe mtakatifu.

    ReplyDelete
  6. nyie watoto mliekuja juzi hapa stockholm.kama hamna hela za michango kwa ndungu na jamaa wanaofiwa hapa stockholm ni afadhali mshamaze kimwa.matusi na dharau zenu hazitawasaidia chochote.nyie mnalala wengi mpaka jikoni huko tensta hakuna anaewajali wala kuwafuata.kama mnaushahidi kuna aliyezulumiwa fikisheni madae kwa ndugu na jamaa wa marehemu ili muyajadili,kuliko kumtukana mtu alikwenda mbele ya haki muacheni abumzike kwa amani.toka zamani tunayomadili yakutoa sadaka na mchango wa ubani kwa wafiwa wote bila ya kujali dini wala tabaka.kuweni nyie.acheni mambo ya kiswahili kama ni wakweli mbona mnajificha?acheni unafiki.kama hamtaki kuja kwenye misiba kaeni kimwa subirini muitwe kwenda kula maandazi na bilau kwenye majumba ya watu.tafadhalini msimtukane marehemu.wacheni wenye moyo wa kutoa watoe.nyie wekeni kwenye chupi zenu.

    ReplyDelete
  7. HENDRY MWORIAOctober 13, 2010

    Ndugu zangu wote mlioko sweden na mlioko Tanzania nawapeni pole sana kwa msiba huu mkubwa wa ndugu yetu na mama yetu, sina cha kuchanga ila nawatatakia shughuli njema za mazishi na tupo pamoja katika shughuli hizi za mazishi. Imenibidi niandike msg hii kwa machungu sana, jamani tuwe na roho ya kibanadamu Monica amefanya mengi sana mema katika kipindi alichokuwa hai hivyo tuache kashfa zisizo na maana sababu njia yetu ni moja, yeye ametangulia tu na sisi tutafaya hivyo tumuombee mungu amlaze mahali pema peponi badala ya kumsema vibaya. Mimi leo hii nafanya kazi naheshimika sababu ya Monica na wako wengi wanaishi vizuri sababu ya msaada wake. Tulimpenda sana Monica ila mungu kampanda zaidi, Amen. NAWATAKIA MAZISHI MEMA, Fred na Devotha mnapaswa mjue walimengu hawakosi la kusema. HENDRY MWORIA, ARUSHA TANZANIA>

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...