Hapa ni wakati wa mapumziko kwani nyimbo hizo hazikuwa
tayari kabla ya kuanza kwa mchezo. Ilikuwa bonge la noma na TFF inabidi wapigwe memo kwa kufanya madudu haya mbele ya Rais
Timu ya Taifa ya Morocco imeweza kujipatia pointi muhimu na goli la ugenini baada ya kuifunga Taifa Stars bao 1-0 katika mchezo wao uliopita katika Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Alikuwa mshambuliaji Mounir El-Hamdaou wa Morocco aliyefunga bao hilo pekee la mchezo kwa shuti kali toka mguu wa kushoto, lililomshinda mlinda mlango Juma Kaseja, dakika mbili tu kabla ya kumalizika kwa kipindi cha kwanza.
Hii ilikuwa ni mwendelezo wa ratiba ya mechi za kufuzu kucheza fainali ya kombe la Mataifa ya Afrika ambapo katika mechi iliyotangulia iliyochezwa nchini Algeria hapo Septemba 3, 2010, Tanzania walipata pointi muhimu ya ugenini japo walitoka sare ya bao 1 - 1 dhidi ya wenyeji wao.
Tanzania imepangwa kundi moja la D, na timu za Algeria, Morocco na Jamhuri ya Afrika ya Kati.
Mgeni rasmi katika mechi hiyo alikuwa Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mdau mkubwa wa michezo, Jakaya Mrisho Kikwete ambaye alisitisha kampeni za uchaguzi mkuu ili kuhudhuria mechi hiyo.
credit source: http://www.wavuti.com
sisi watanzania bado hatujawa na uzalendo wa kweli timu inacheza nyumbani halafu inakosa kabisa sapoti ya washangiliaji kwa mfano mzuri ilipocheza kule ALGERIA wanafunzi wanaosoma kule waliweza kishangalia kwa nguvu zao zote kuanzia walipofika uwanja wa ndege hadi uwanjani wakiwa na bendera za taifa na hatimaye wakapata sare ya 1-1 walikuwa wakiimba ONE,TWO,THREE VIVA LA TANZANIE leo tumecheza hapa nyumbni uwanajani hapakuwa na bendera za kutosha.kimpira tumecheza vizuri ila ni vyema tuka mtimua kocha mapema kabisa kwani mechi ya tatu hajashinda hata moja halafu mbona wachezaji wa simba anawabania kulikoni?
ReplyDeleteMzigo wote wa makosa inabidi tumtwishe Maximo. Taifa Stars itapataje ushindi bila Chuji na Boban?
ReplyDeleteMaximo hafai!
Kama team haifanyi vizuri twende uwanjani 4 what?? hiyo ni kila sehemu timu ikiwa inafanya vibaya mashabiki hawaendi uwanjani. Check out Oakland kwa miaka kadhaa mechi zake zimekuwa blackout coz hawauzi ticket za kutosha, timu haifanyi vizuri
ReplyDeleteWabongo bwana kwa lawama.Kila kocha mnataka mumtimue sababu timu yenu yenye wachezaji wasio na uwezo kimpira inashindwa kuwin game mnalaumu kocha.Sasa ulidhani kocha alitakiwa aingie uwanjani kufunga magoli?
ReplyDeleteWewe Anon #1 acha unazi eti wachezaji wa Simba.Nani kakwambia ile ni Simba.Pumbafu sana ni timu ya Taifa na wachezaji wanaonekana wana uwezo kimpira ndo wanateuliwa kuvaa jezi za Blue/njano/nyeusi/kijani.Peleka akili zako za nineteen kweusi kwenu.
Hivi ndivyo atakavyopigwa goli JK TAREHE 31/10
ReplyDeleteMh rais kaacha kampeni kwenda KUISAPOTI nchi michezoni,majuzi mtandaoni alionekana wakati wa birthday yake anazungumza na wanamuziki pia inapotokea misiba jamaa anaenda,jana MremaLipumba na Slaa walishindwa nini kwenda taifa?MBON AKWA bURKINA fASO WALIENDA?INAFIKA WAKATI UZALENDO TUUWEKE MBELE
ReplyDeletejamano eeh mpira haukuonekana tanzania tu mjue hivyo. ukweli wachezaji wamecheza kiwango cha juu
ReplyDeletekiasi chao nagoli limefungwa wenzetu wametumia nafasi waliopata.
makosa yakurekebishwa nimadogo.
mbele hatuna mashambulizi yakuosha
lazima wachezaji wetu wapewe ujanja
wakushambulia.tena tuombe pia
wapatikane wachezaji mbele walioshiba kimwili nakatikati basi raha tutaiona mbele ya safari huko miaka ijayo mitatu tu ninaimani. tukija katika kamati ya ushindi mliangushwa kweli na washangiliaji
wetu tumeona sie huku wa mbali.mpira unazi yani.FITNA. bila hilo ngumu uchawi hakuna kabisaa.
huku tunaona fitna hata uefa wanafanya unafikiri champion bila Milan.Real.Barc.Bayern.Man u. kuna champion?inafanywa fitna timu zinaingia humo. ukweli wachezaji
wetu wamejitahidi sana sana.good luck taifa stars. watanzania mpira sio draft jamani. angalieni zamani miaka 80 huko kuna mtu Omar hussein mdogo kama ngasa alikuwa
lakini kashiba sehemu zote.kina mohd salim thuwen ali weee hapatoki mtu hapo.kubwa tusivunjike moyo timu inahitaji marekebisho kidogo.
Duh poleni wadau....
ReplyDeleteNaskia nksi lilianza kwa nyombo za Taifa kugoma kimba kwa ama mitambo feki ama mipango ya kula cha juu kwanza - kumleta msanii mbovu ambaye mitambo yake haisomi cd ya My National Anthem yetu111 TFF Haooooooo Aibu yenu daima
Mdau nambari moja, hapo umegonga msumari kwa kichwa. Hilo pia nililiona.
ReplyDeleteNi ushamba mwepesi mwepesi huoo ndugu yangu. Ka taarifa yako, nionavyo mie - na niko sahihi surely, ni kuwa pale kila mtu yaonekana alienda kuangalia mpira. Yaani kufaidi matunda ya hela alizolipia kuingia uwanjani, na si vinginevyo. Wabongo hawakulipa ili waende kuishangilia timu yao, la hasha!
Watu walikuwa wamenung'unika utadhani wako msibani? Au utafikiri BURMA ilikuwa ikicheza dhidi ya THAILAND? Inatia uchungu sana, naumia, naumia, ... naumiaaaa.
Hivi wabongo hawajui umuhimu wa uwanja wa nyumbani? Ni kweli hii? nauliza tena ni kweli? Kama ni hivyo, basi vichwa vimejaa konokono badala ya ubongo!
Hii si mara ya kwanza kwa timu kufungwa nyumbani, lakini kwa hali niliyoiona kwao, nimekatishwa tamaa na watanzania. Tunajifanya kuwa juu katika mambo ya inteneshnoo hasa mpira lakini kumbe ni ziro kabisa.
Inasikitisha kuona jinsi watu walivyolipa hela nyingi na kwenda kuishangilia BRAZIL ule mwezi wa JUNI, halafu timu yao wanaiacha kama hivi.
Faida ya uwanja wa homu ni kuwa mashangilizi huwatia m'washawasha wapinzani na kuwafanya washindwe kukonsentreti, na kuanza kuluuz mwelekeo.
Tumeshindwa kuitumia nafasi hiyo, tutaijutia. Ni nafasi nzuri ambayo ingetuweka pazuri kimataifa, nalijua hilo nd'o maana nalisema.
Inaniuma sana ... ngoja niachie hapa.
Chiaaz Mchiiz
wabongo sasa tuumpe kocha nafasi kidogo ili akamilishe mipango yake, na hivi sasa TFF inaongozwa na Leodgar Tenga naamini ana akili zaidi ya yule mfisadi mkuu rage. msomali wa dom
ReplyDeletekulikuwa na haja ya askari gani ya askari jeshi kuongoza waamuzi na wachezaji hadi uwanjani?
ReplyDeletePoor guys....its like some stranger coming to your house and gives you a BIG slap on your face in front of your wife and kids. Painful...
ReplyDeleteMdau wa tatu umeongea pointi lakini suala la kuwepo la watu wenye mawazo kama mdau wa kwanza wamelipandikiza waandishi wetu wa habari. Kwenye mechi ya Aljeria mimi sikujua timu iliyopangwa uwanjani ilikuwa haina mchezaji wa Simba mpaka niliposoma gazetini. Baada ya kusoma gazetini nikajiuliza waliocheza walikuwa wanawakilisha klabu zao au taifa letu? Ni upuuzi. Mtindo huu ukiendelea baadae watu wataanza kuandika kwamba timu ya taifa iliundwa na Wanyakyusa watupu/Waislamu watupu, au hata wachezaji warefu watupu. Bure kabisa!
ReplyDeleteKwa nini Maximo hakuwapanga Chuji na Boban? Ndio sababu tumefungwa.
ReplyDeleteYah! Kwa mara nyingine Tanzania tumajitahidi. Sidhani kupata zaidi ya hapo ni ndoto kwa timu yetu. Kuna mambo mengi yanahitaji kuangaliwa ili tupate matokeo mazuri zaidi.
ReplyDelete1. Zile kelele za Kaseja Kaseja naona sasa zitafika mwisho. Golikipa pekee habadili matokeo ya timu. Kwa maoni yangu Kaseja anafaa zaidi kuchezea Simba na si timu ya taifa kwa sababu ni mfupi na mdogo. Ukiangalia kwa makini goli kutokana na ufupi wake hakuufikia mpira. Maximo was right.
2. Tuwekeze kwa wachezaji wenye maumbo makubwa. TS ilikuwa kama timu ya watoto kwa wa Morocco. TFF fanyeni tathmini. Timu ya enzi za kina Tenga ilikuwa ni mipande ya watu. wako wapi hawa hivi sasa.
3. Ni aibu uwanja kuwa mtupu. tatizo ni ninini!!!!!! kiingilio au nini. Uwanja ulitakiwa kuwa ni sale out. inakuwaje haukujaaaaaaaa!. Kama ni kiingilio, kwanini kuwa mtupu wakati timu yetu inacheza. Ni aibu.
4. Ushangiliaji! hapa TFF inatakiwa kuhamasisha ushangiliaji. Watazamaji wanatakiwa kuhamasishwa au kufundishwa namna ya kushangilia. Usitegemee hali ya ushangiliaji hujitokeza bure. Mbona kwenye mikutano ya siasa/ sherehe za harusi nk. washereheshaji huwaelekeza watu namna ya kushangilia na wote huitikia. Inatakiwa kufanyika hivyo. Punguza viingilio kwa masharti ya kuja kwa wingi na kuishangilia timu. Kama kuna wenye pesa Zao (wadhamini) wagawe vibendera kwa kila anayengia, nk.
4. Ubunifu na committment inatakiwa. Mungu ibariki Tanzania.
Kama hao walioteuliwa wana uwezo .mbona hawajashinda au kutoa droo?.
ReplyDeleteMashabiki Bongo bado ni washamba kwa kuwa wanaufanya ule uwanja kama sehemu ya kustarehe,wao hawataki kushangilia kabisa ,dawa yao ni kuwa mechi nyingine ya Stars unawapeleka uwanja wa Uhuru ili tupate vijana wa mzunguko na jukwaa la Kijani wanaojua kushangilia.
Hapa kocha ni wa kulaumiwa kwa kuwa timu ilikuwa inajilinda zaidi kuliko kushambulia.Halafu timu haina winga wa kushoto.Kwenye kiungo cha kati ulinzi(6) na ushambuliaji(Namba 8)alitakiwa aanze na Nurdin Bakari(Namba 8) na Henri Joseph(Namba 6)yeye kawapanga Henri Joseph ambaye ni mzuiaji na Shabani Nditi naye mzuiaji,hii ikasababisha timu iwe inazuia zaidi kuliko kushambuliaMwenzake Maximo alilitambua tatizo hilo akaamua kama anaanza na Nditi namba 6,Henri Joseph alikuwa akipangwa namba 7 na Boban au Nizar namba 8.Kwa nini timu ijihami wakati iko nyumbani.???
Angalia kwa mtindo huo ikamlazimu Ngasa kuwa akirudi kutafuta mipira,timu haikucheza kwa malengo haikuwa na nia ya kutafuta goli.Kocha inabidi atafute kiungo wa kushoto halafu ajue yupi wa kuanza na yupi wa kuingia Angalia Bocco anaingia kufanya nini Khaaa nina maneno mengi ya kuongea ila nimechoka inauma inauma sana ,wakati mwingine nawaza bora tuwasomeshe makocha wetu wazalendo waongoze timu.
Wadau wa mpira mnaonaje Timu ya taifa ibadilishe jina labda itasaidia!
ReplyDeleteJina taifa stars haliwatishi wapinzani,ukizingatia kisoka tunajiita taifa stars wakati hatufanyi vizuri kwenye level ya kimataifa,tunaonekana wendawazimu na wachezaji wanaonekana comedian kwa kujiita taifa stars wakati hawaachieve chochote kwenye international level.Tunahitaji jina tofauti ambalo lipo aggressive kimtindo ambalo litafanya squad yetu iwe na moral ya ku fight kiume.
Mi napendekeza taifa stars iitwe 'SIMBA WA MASHARIKI'(eastern lions)
kwani tuna mbuga za wanyama na simba pia tunao na tupo mashariki mwa afrika.
Taifa stars halifai tena.
yaani kila mtanzania mchezo pekee anaoujua ni mpira wa miguu tu na kila siku tunashindwa. kuna michezo mingi tunaweza kucheza na kufanikiwa. tusahau kutegemea michezo kupeperusha bendera yake na badala yake tuanze kuitumia kama njia ya kuboresha afya, kuimarisha urafiki, udugu na mawailiano.
ReplyDeleteSun Oct 10, 08:03:00 PM, umeongea point nyingi sana ukasahau moja nitaiongelea mwishoni mwa mchango wangu.
ReplyDeleteKuhusu suala la maumbo nafikiri niwakati muhafaka kuanza kukubali ukewli huu ingawa unauma. Mimi nilikuwa safarini morogoro, nikaenda kushuhudia mechi kati ya Kagera Sugar na African Lyon. Kagera sugar walikuwa wanaongoza na kuonekana wanacheza vizuri kutokana na Mwaikimba aliyekuwa na umbo kubwa na kuonekana kama vile anacheza na watoto wa chekechea. Magoli yote mawili yalitokana na urefu wake. Mipira ya kona na direct kick. Kama si kipa wa Kagera sugar kuleta bangi na kusababisha penalti na red card kwake dk za mwanzao kagera sugar ingeshinda kwa Magoli mengi tu.
Upande mwingine wachezaji wetu wanakuwa kama hawana malengo vile, wanashangaza sana. wanapigiana pasi nzuri kati bila kuwa na lengo la kufunga magoli. Nafikikri hata wapinzani walisoma hilo ndipo wakaanza kutushambulia dk za mwisho na kupata goli. Vile vile team work sometimes inapotea, inawezekana mchezaji mmoja akawa anakabiliana na adui na ikaonekana kuhitaji msaada lakini mara nyingi anaachiwa yeye tu hadi aporwe mpira.
Upande wa uwanja kutojaa nafikiri ni mambo mengi pia. Miundo mbinu na foleni ni kazi kweli kweli hasa wakubwa wakiwepo uwanjani, barabara zinafungwa baada ya mechi hivyo kama unakaa mbali na unategemea usafiri wa daladala unasumbuka sana, unakuwa huna amani moyoni wakati wa mpira, mawazo yote utafikaje nyumbani.Hivyo inatakiwa uwe mkeleketwa kweli kweli ndiyo uende huko.
Nakumbuka wakati wa ufunguzi wa uwanja huo mpya kulikuwa na mechi dhidi ya Uganda. Nilikuwa nakaa Sinza, baada ya mechi barabara zikafungwa ili viongozi wapite kwanza, baada ya kufunguliwa kulikuwa na foleni ya kufa mtu ilibidi nitembee kwa mguu, pamoja na watu wengine hadi Magomeni ndipo nikapata gari ya kwenda sinza. Hivyo inabidi kuwe na mkakati wa kuondoa tatizo hili ikiwewzekana rais awe anaondoka kwa helikopta na watu kama sisi wajue hivyo ndipo tutaenda vinginevyo ni costly kwa watu interms of time
TAAAABUUU AAAAAIIIIBUUUUU.
ReplyDelete#
NDIO KAWAIDA YETU. KAMA KAWAIDA HAMNA CHA AJABU KWA KUFUNGWA WALA T.F.F KUHARIBU.
KWANI ULE MSEMO MTOTO UMLEAVYO NDIVYO AKUAAVYO. KUCHEMSHA MBELE YA RAISI NI SAWASAWA NA MTOTO KUTUKANA MBELE YA WAGENI.
TUMEWALEA T.F.F WALICHOKIFANYA SIJAKISIKIA KWENYE LEVEL YEYOTE YA KIMATAIFA DUNIANI.
MAXIMI MAXIMO, MAXIMO, HAYA KAONDOLEWA NDIO NINI KIMETOKEA. KIWANGO KIDOGO TU SI KOCHA. TUMFUKUZE NA HUYU TUMLETE WENGER. YATAKUA YALEYALE TU HATA ASHUKE MALAIKA......
KASEJA KASEJA KASEJA YALEYALE TU. BWANAAA WEE NIMECHOKA.
Mchangiaji namba mbili, maximo hayupo hivi sasa, kuna kocha mpya, huyo naye sijui mtasemaje
ReplyDeleteSISI BWANA MDUNDIKO,SINDIMBA......BONGO FLAVOURS
ReplyDeleteMAPENZI ....NDIYO ZETU.