Kikosi kazi cha timu ya soka ya Tanzanite FC

Timu ya Soka ya Watanzania Waishio Atlanta Georgia (Tanzanite FC), leo itaanza tena kujaribu kampeni yake ya kupanda daraja katika ligi ya soka ya ADASL kwa kupambana na FC Silverbacks ya Atlanta.

Timu hiyo ambayo almanusura ipande daraja miaka miwili iliyopita ilishindwa kushiriki katika ligi hiyo kwa sababu za Ukata. Katika msimu huu imeamua kujipanga upya na kusajili vijana kadhaa wadogo kutoka state nyingine.

Baada ya kukimbiwa na viungo wake machachari kama Khamza Liganga na Muzindwelah Ghanize ambao wamesajiliwa na timu ya daraja la pili ya Sting FC.

Pia timu hiyo itawakosa wachezaji Hadji Helper ambaye atakwenda Australia kwa majaribio na timu ya Melbourne FC. Katika listi hiyo pia yupo kiungo Edgar Kisoka ambaye amenyakuliwa na Chuo Cha Christian Brothers huko Memphis Tennessee.

Timu hiyo imenyakuwa vijana watatu hatari kutoka State za Illinois, na North Carolina. Kutoka Illinois ni mshambuliaji Fredy John na kutoka North Carolina ni ndugu wawili walinzi wa kushoto na kulia ambao ni Abel na Joel Mundo.

Habari kutoka katika uongozi pia zinasema timu hiyo iko katika mazungumzo na Mshambuliaji Dennis Imani Geofrey kutoka chuo kikuu cha Greensboro ili aweze kuhamia Mjini hapo ili kuipa nguvu timu hiyo.

Ikumbukwe kuwa mshambiliaji huyu alileta balaa la usajili kati ya Timu ya Yanga na FC Arusha.

Mungu ibariki Tanzanite FC.

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 2 mpaka sasa

  1. gud lak guyz na pia gud lak kwa huyo anayekwenda ktk majaribio.i hope is not some kinda of a joke sababu 2nataka sana mafanikio ya wachezaji we2.

    ReplyDelete
  2. Michuzi matokeo ya Bwawa la Maini mbona siku hizi hatuzioni wengine tuko Siberia hatujui matokeo, tafadhali tujulishe!! Mdau Siberia

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...