Sporah Njau wa Sporah Show akiwa na kikosi
kazi cha Urban Pulse leo jijini London

Salam Ankal

Urban Pulse Creative leo ilipata fursa ya kuingia kwenye Kipindi Sporah show kinachorushwa hewani na Ben TV hapa UK pamoja na Star Tv Tanzania ili kufanya kampeni ya Urban tour kwa ajili ya kusaidia na kuchangia vita dhidi ya Malaria. Ugonjwa huu unaua mamilioni ya watu wengi duniani kuliko Ukimwi, kitu cha kushangaza na kusikitisha ni kwamba unaweza kutokomezwa na kuangamizwa milele ikiwa kila mtu akielimika na kuamua kuchukua majukumu ya kuviangamiza vijidudu hivi hatari kwa kuanzia kusafisha na kutunza mazingira bila ya kulaumu wala kunyooshea vidole serikali pekee wala Taasisi zozote.

Urban Pulse Ikishirikiana Na Aset pamoja na Tanzania Community inawaletea Msanii Daimond kutoka Tanzania pamoja na Mish the Fyah Sis Kutoka urban Pulse ili kuwapa burudani murwa. Baadhi ya mapato yatakayo patikana yatakwenda kuchangia Kampeni ya kupambana na Malaria in Africa. Wote Mnakaribishwa. Tafadhali wahi mapema. Terehe na ukumbi ni kama zifuatavyo:

6th Nov. 2010
CLUB OPUS
Theatre Distric
Savoy Cresent
Milton Keynes MK9 5UP

12th Nov 2010
THE CLUB
179 – 183 London Road
Croydon, London
CRO 2LR

27th Nov 2010
PANAMA BAR
Gas ST
Birmingham
B1 2JT

WOTE MAKARIBISHWA,
Frank Eyembe
URBAN PULSE CREATIVE MEDIA

Michuzi Blog

Tanzanian blog operating since 2005, covering International news and Local News, including Politics, Fashion, Social Scenes, Interviews, Movies, Events, personalities and anything positive happening worldwide. Written in Swahili and English targeting both Swahili and English readers.

Toa Maoni Yako:

Kuna Maoni 4 mpaka sasa

  1. Diamond labda upige muzic wako uko London ambako kumejaa watoto wa Vigogo wa CCM vinginevyo nakwambia umeharibu soko lako kwa tamaa zako za muda mfupi

    ReplyDelete
  2. Hi Sporah, mi ni fan mkubwa sana saaana wa show yako, nataka tu kukupa hongera kwa kutuelimisha kupitia kipindi chako. Karibu Bongo, We love you.

    ReplyDelete
  3. Sporah naona vimashavu vinachomoza du, mambo sio mabaya dada angu. Karibu Texazzzz Dada.

    ReplyDelete
  4. Hao vijana wameliwa, leo wako kwenye Movie, Kesho wanaidia Watoto yatima waathirikiwa na Gonjwa la Ukimwi! na sasa wana fight Maleria!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
    Wabahatishaji Au MIZEGWE tu hii Ankara.

    ReplyDelete

Hii ni Blog ya Watanzania popote walipo duniani kwa ajili ya kuhabarisha, kutoa/kupokea taarifa na kuelimisha mambo yote yaliyo chanya kwa Taifa letu. Tafadhali sana unapotoa maoni usichafue hali ya hewa wala usijeruhi hisia za mtu/watu. Kuwa mstaarabu...