Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikata utepe kufungua rasmi jengo la Chama Cha Waalimu Tanzania Mkoa wa Ruvuma leo asubuhi.Wapili kushoto ni Rais wa Chama Cha waalimu Tanzania Bwana Gratian mkoba na watatu kushoto ni Waziri wa Elimu Profesa Jumanne Maghembe.
Mwanafunzi wa shule ya msingi Samora mjini Songea mkoani Ruvuma akimkaribisha Rais Jakaya Kikwete kwa saluti maalumu muda mfupi kabla ya Rais Kikwete kufungua rasmi jingo la Chama Cha waalimu mkoa wa Ruvuma leo asubuhi
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwasalimia baadhi ya watoto waliomlaki muda mfupi baada ya kuwasili katika uwanja wa ndege wa songea ambapo alikuwa mgeni rasmi katika maadhimnisho ya sherehe ya siku ya mwalimu duniani.
Sehemu tu ya mamia ya waalimu toka mikoa yote nchini waliohudhuria sherehe za siku ya mwalimu duniani wakimsikiliza Rais Dr. Jakaya Mrisho Kikwete alipowahutubia katika uwanja wa michezo wa Majimaji mjini Songea. Rais Dr.Kikwete alikuwa mgeni rasmi katika maadhimisho hayo kwa mwaliko wa Chama cha Waalimu Tanzania
Mamia ya waalimu waliohudhuria maadhimisho ya siku ya mwalimu duniani wakiingia kwa maandamano katika uwanja wa michezo wa Majimaji mjini Songea ambapo Rais Dr.Jakaya Mrisho kikwete alikuwa mgeni rasmi na kuwahutubia.

kaka michuzi hongera kwa blog bomba!
ReplyDeletelangu ni moja tu muwe waangalifu mnapo-post vyeo vya watu! Mtu huwezi kutambuliwa kama Dr kwa PhD ya kupewa (honorary Phd). U-Dr ni strictly academic qualification, please!...
Haya ibanie na hii maana unabania nyingi za kwangu!