TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
YAH: UCHUNGUZI KUHUSU TUHUMA ZA RADA
Tunapenda kuujulisha umma kuwa uchunguzi na ushahidi uliokusanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Shirika la Upelelezi - SFO la Uingereza kuhusu tuhuma za Rushwa katika ununuzi wa Rada, umeshindwa kumhusisha Bw. Andrew Chenge katika tuhuma hizo.
YAH: UCHUNGUZI KUHUSU TUHUMA ZA RADA
Tunapenda kuujulisha umma kuwa uchunguzi na ushahidi uliokusanywa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) pamoja na Shirika la Upelelezi - SFO la Uingereza kuhusu tuhuma za Rushwa katika ununuzi wa Rada, umeshindwa kumhusisha Bw. Andrew Chenge katika tuhuma hizo.
TAKUKURU inawaomba wananchi waendelee kutoa ushirikiano kwa chombo hiki kwa kutoa taarifa za kuwafichua wale wote wanaojihusisha na Rushwa kwani jukumu hili ni la kila mmoja wetu.
Imetolewa na
Doreen J. Kapwani,
Afisa Uhusiano-TAKUKURU
Novemba 08 , 2010
S. L.P. 4865,
Dares Salaam.
Imetolewa na
Doreen J. Kapwani,
Afisa Uhusiano-TAKUKURU
Novemba 08 , 2010
S. L.P. 4865,
Dares Salaam.
Simu: 2150043-6/2150360
Nukushi: (022) 2150047
Baruapepe:dgeneral@pccb.go.tz
Mtandao www.pccb.go.tz
Mtandao www.pccb.go.tz
Weldone TAKUKURU!!!! watanzania tumezoea saana kuamini bila ushahidi kama kuna mtu ana DATA awapelekee TAKUKURU now! CHENGE Hongera and Go a head for the speaker's seat
ReplyDeleteKama ni kweli akuhusika ktka kesi hii basi hatuna cha kusema.ila waliousika wapewe adhabu kali sana
ReplyDeleteweweeeeeeeeeeeeeee! chenge for speaker! go CCM!
ReplyDeleteIngekuwa vizuri PCCB wangeweka hiyo ripoti ya SFO ya Uingereza nasi wadau tukaisoma kujiridhisha na utendaji wa PCCB(Takukuru).
ReplyDeletemmmh,mmeanza sasa!mbona hankusema kabla ya uchaguzi!
ReplyDeleteSAWA wazee tumesikia!
ReplyDeleteLakini vile vijithumni mmebahatika kujua vimetoka wapi?!
au na hilo pia mmefeli?
maana vile ndo chanzo ya vyote.
tunahitaji maelezo yaliyokamilika and not muhtasari tu.
Kumekucha..who is next? Bongo tambarare .....
ReplyDeletehii ndio chama CHUKUA CHAKO MAPEMA never learn from mistake sasa watawafishwa wote
ReplyDeleteNIMEOTA NDOTO TANZANIA IMEKUWA NA ADABU,UAMINIFU NA HESHIMA,HAKUNA MTOA RUSHWA WALA MPOA RUSHWA,VIONGOZI WANATIMIZA AHADI ZAO BILA YA KUWADANGANYA WANANCHI ILA KABLA YA NDOTO HII KUTIMIA NIMEOTA NDOTO BAHARI YA HINDI SAMAKI WAKIELEA ELEA KILA UPANDE KWA FURAHA WAKILA NYAMA ZA MIILI YA WANADAMU WALIOKUFA KWA KUTOKUWA WAAMINIFU NA NCHI,WATOTO NA NDUGU YA WALE WALIOUAWA WAKILIA KWA UCHUNGU WAKISEMA TUNGEJUA TUSINGE MEGA MKATE AMBAO SIO JASHO LETU WALA JASHO LA BABA ZETU BALI NI JASHO LA MTU AMBAYE HAKUPEWA HAKI!!!KISHA NIKASIKIA SAUTI IKISEMA KWENYE NDOTO HAYA YANAPASWA KUTOKEA KARIBUNI ILI HIYO ADABU,UAMINIFU NA HESHIMA VIJE!!!MWENYE MASIKIO NA ASIKIE
ReplyDeleteAny suspect will remain INNOCENT until proven guilty in the competant court of law.
ReplyDeleteTatizo letu Tanzania, vyombo vya habari na vyenyewe vimeacha kufanya kazi zake kwa misingi ya maadili badala yake vinafanya kazi kwa ushabiki. Jambo hili linawanyima wananchi/wasomaji habari sahihi na hatimaye kuwajaza wasomaji hao na wananchi mambo ambayo ni ya upotoshaji.
Kwa mfano, taarifa za kutohusishwa Chenge na tuhuma za rada zipo, lakini hakuna mwandishi ambaye alifanya juhudi za kufuatilia kwa wakati mwafaka na kuwajulisha watanzania kuwa Mh Chenge hakupatikana na dai lolote, badala yake tumeendelea kuachwa kwamba anahusika.
Tuliona wakati wa uchaguzi mkuu jinsi ya baadhi ya vyombo vya habari vilivyofanya kura za maoni zilizo ratibiwa nje ya utaalam na kumpa hisia mgombea fulani wa urais kuwa ile ndiyo projection sahihi ya matokeo ya uchaguzi. matokeo yake mmempa kiwewe hadi leo anashindwa kuamini matokeo ya kura halisi.
Vyombo vya habari vinatakiwa vifanye kazi kwa misingi ya uadilifu na si ushabiki.
Htas off Doreen...tunataka uwazi jinsi hiyo...maana mngeendelea kukaa kimya watu wasiomtakia mema wangeanza kuleta hoja za rada na vijisenti ili mradi tu kutaka kumzibia nia yake ya kuwania uspika...binafsi nina imani kubwa naye...naamini anao uwezo..namkumbuka alipokuwa mjumbe wa bodi yetu ya rift valley Seed zama hizo..MUNGU akujaalie kaka Andrew
ReplyDeleteVIONGOZI WOTE WA TANZANIA KUNA SIKU MTAUWAWA HAZARANI MAPINDUZI YAKITOKEA WASHENZI SANA NYIE WADANGANYE MALIMBUKENI TUMECHOKA NA MWISHO WENU UNAKARIBIA
ReplyDeleteDoreen, hebu elezea vizuri kuhusiana na hizi tuhuma...haya maswali humu ndani yalijibiwa kweli??
ReplyDeleteRipoti ya SFO hii hapa...
http://www.scribd.com/doc/11490017/SFO-Report-on-the-Radar-Saga
BAE Systems plc
ReplyDelete05 February 2010
BAE Systems plc
The Serious Fraud Office ("SFO") and the US Department of Justice ("DoJ"), have both announced settlements with BAE Systems plc, in a ground breaking global agreement. The DoJ agreement involves BAE's business dealings in a number of countries, whilst the SFO agreement concentrates on the company's operations in Tanzania.
The SFO has today reached an agreement with BAE Systems that the company will plead guilty in the Crown Court to an offence under section 221 of the Companies Act 1985 of failing to keep reasonably accurate accounting records in relation to its activities in Tanzania. The company will pay £30 million comprising a financial order to be determined by a Crown Court judge with the balance paid as an ex gratia payment for the benefit of the people of Tanzania.
In conjunction with this agreement the SFO has taken account of the implementation by BAE Systems of substantial ethical and compliance reforms and the company's agreement with the DoJ announced today, and has determined that no further prosecutions will be brought against BAE Systems in relation to the matters that have been under investigation by the SFO.
SFO Director Richard Alderman said, "I am very pleased with the global outcome achieved collaboratively with the DoJ. This is a first and it brings a pragmatic end to a long-running and wide-ranging investigation. I would like to thank the Ministry of Defence Police for their support and contribution. Furthermore, I'd also like to acknowledge the efforts made by BAE to conclude this matter and I welcome its declared commitment to high ethical standards".
Zaidi:
http://www.sfo.gov.uk/search.aspx?search_two=tanzania
Nawakilisha kaka Mithupu!
"Amen".
ReplyDelete"Amen".
ReplyDelete